Afande "SAIDI MWEMA" Njoo tuongee kidogo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afande "SAIDI MWEMA" Njoo tuongee kidogo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAZETI, Dec 13, 2011.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa mimi sio askari ni bora nikupe haki yako. Shikamoo!

  Majukumu ya kazi yanaweza kukufanya uchoke kusoma thread ndefu hivyo naona bora niende kwenye point moja kwa moja bila kufuata taratibu zilizozoeleka sana za Uandishi.

  MFUMO WA AJIRA KWENYE JESHI LA POLISI:

  Naanzia hapo. Ni mfumo mbaya ambao unawaingiza watu wakorofi na wasio na sifa za kinidhamu za kuweza kuwa Askari. Nina ushahidi wa wazi kuwa wanaoingia wengi ni wahuni na wavuta bangi, hii inatokana na wengi wanaoingia kuwa ni ndugu wa polisi ambao wamekosa nafasi za kuendelea na masomo n.k.

  Ajira za undugu na kujuana ndizo zinazopelekea jeshi la polisi kukosa watu wenye sifa na mwisho wa yote kuzalisha askari wanafiki ambao wako tayari hata kutoa siri za mtoa taarifa kwa wahalifu jambo linalosababisha wananchi kukaa kimya bila kutoa taarifa kwa kutambua wazi kuwa kuna ushirikiano mkubwa wa wahalifu na Polisi.

  Nina ushahidi wa wazi wa watu ambao walikuwa wanavuta bangi huku mtaani na hatimaye wameajiriwa na jeshi la polisi. Ni afadhali ajira ya mtu ambaye ameghushi cheti kuliko watu kama hao. Nasema afadhali walioghushi kwa sababu ninao ushahidi wa watu wawili ambao wameghushi lakini ni wanafanya kazi vizuri mno.

  USHAURI: MFUMO WA AJIRA UANGALIWE UPYA

  IDARA YA UPELELEZI

  Idara ya upelelezi ya jeshi la Polisi inaonekana kutofanya kazi yake kitaalamu na kwa kutumia akili. Pengine hili linaweza kutokana na tatizo lile lile tulilolitaja awali la ajira za kutozingatia. Mbinu zinazotumika za kuwatesa watuhumiwa si sahihi kwani mtu anaweza kukubali tu ili aepukane na mateso hayo.

  Pia kumekuwa na matukio mengi ambayo mwisho wa yote tunaambiwa tu Polisi wanaendelea na upelelezi mkali ambao hautoi matokeo yoyote. Pengine hili linaweza kutokana na udhaifu mkubwa wa watu waliopo katika Idara hii. Wapelelezi gani hawa ambao hata ukikutana nao tu unatambua moja kwa moja kuwa huyu mtu ananichunguza - hatuendi hivyo. Wakati sasa umefika kwa watu wanaoajiriwa katika idara ya upelelezi kutofautiana na wale wa ajira ya askari wa kawaida. Hawa wa idara hii nyeti ni vizuri wakiangaliwa uwezo wao na wepesi wao kiakili. Tena si vibaya hawa watu kama watachunguzwa na kufuatiliwa kuanzia mashuleni mpaka vyuoni.

  UBAHILI: Pengine ubahili unaweza kuwa chanzo cha Idara hiyo kukosa taarifa muhimu. Hivi kuna hasara gani mkitangaza dau la milioni 5 kwa mtoa taarifa zitakazosaidia juu ya watu waliovunja na kuiba Benki? Sio kusema zawadi nono itatolewa. Semeni kuna milioni 10 au 15 hapo hata wapelelezi binafsi wataingia kazini si unajua Tanzania njaa ni kali?

  USHAURI: Idara ya upelelezeiangaliwe upya kwa kuajiri watu wenye uwezo wa kuhoji, kuchunguza na kufuatilia na si wababe wajuzi wa kutesa na kulazimisha mtu akiri kitu ambacho hajafanya.

  WASI WASI WANGU:
  Uwezo wa askari wa kufikiri ni mdogo ndio maana wako tayari kuwapiga kwa virungu watu wanaoandamana kudai maslahi yao wakati hata wenyewe pia wana matatizo yao. Kama huamini zunguka uangalie nyumba wanazokaa askari. Nyingi zinapendeza zaidi kwa kufugia kuku wakati nyingine zingefaa zitumike kwa kuhifadhia mazao. Kama huamini nenda Kota za askari zilizopo pale Usalama Magomeni, Zinatofauti gani na magulio?

  HITIMISHO: Askari badilikeni, fedha ambazo zilitakiwa zitumike kujenga nyumba zenu ambazo ni bora ndio zile ambazo watu wanagawana kule Bungeni.

  GAZETI (P.I)
   
 2. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni maoni mazuri kwa hakika,
  Nadhani mlengwa akiyapata na kuyachuja kwa manufaa ya Taifa
   
Loading...