Afande Ndomba,askari wako wa JKT wanaadhirika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afande Ndomba,askari wako wa JKT wanaadhirika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ruhazwe JR, Sep 28, 2012.

 1. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwanza nianze kwa kukupa pongezi ya kupanda cheo sambamba na kupanda madaraka kutoka Ukuu wa JKT hadi kuwa Mnadhimu wa Jeshi kwa ujumla.

  Nimepata kupitia habar/tetesii zinazotapakaa baada ya wewe kuondoka JKT,kwa ujumla askari wengi hasa wanyonge(na maanisha wale wa cheo cha chini)wamesikitishwa na kuondoka kwako JKT.Ingawaje mimi naamini nafasi uliyo nayo kwa sasa ni nzuri mno kutatua matatizo ya askari kwa ujuimla kwa kuwa taarifa zinasema umekua mstari wa mbele katika kutatua matatizo ya askari wanyonge ambao ndio ni wengi.

  yapo mengi ulitatua na hasa kulazimisha mishahara ya askari wa JKT kulipwa kwa kupitia bank badala ya Cash kama ilivyokua awali.Zoezi hili limegusa maslah ya watu mafisadi ndani ya JKT,kitu ambacho kimefanya zoezi kuendeshwa kwa kusuasua na kusababisha askari wengine kutokupata mishahara yao kwa kipindi cha zaidi ya miezi minne na hasa Ration Allowance.

  Umeondoka JKT umeacha baadhi ya askari wakiadhilika kwa kukosa mishahara yao kwa muda mrefu hali ambayo imepoteza matumaini kwa askari wako hasa wanapoona kuwa hakuna atakaye weza kutatua tatizo hili kwani tatizo lenyewe linaitaji mtu mwenye uzalendo wa kweli katka kazi.

  Taarifa zinasema kuwa kuondoka kwako kumewafanya baadhi ya askari wa ngazi ya juu na hasa walioko idara ya fedha na idara ya SUMA walifanya sherehe ya kufurahia kuhama kwako kwa kijificha kwakua ulikua unawabania minya yao kufanya ufisadi.lakini hili kwangu si lililonifanya nije hapa jamnvini,lililonifanya nije jamvini ni juu ya swala zima la malipo ya mishahara na Ration Allowance za askari wako walioko JKT,Je unafahamu kuwa kuna askari hasa wa cheo cha chini hawalipwi mishahara kwa muda mrefu sasa?na kama unafahamu Tatizo ni nini?na je unataka tuamini kua serikari kupitia wizara ya ulinzi imewakopa askari wako wafanye kazi kisha malipo badaye?

  Afande ndomba ikiwezekana wape askari wako wa chini number za simu ili wakumwagie uozo ambao hata wewe wanaamini huujui.

  Ni haya tu kwa leo.zaidi nakutakia kazi njema matika madaraka yako mapya
   
Loading...