Afande Mbuzi ndani ya jeshi la Uingereza

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,341
Reaction score
15,842
Jana kwenye BBC Swahili ilitangazwa hatua ya myama mbuzi kuajiriwa kwenye jeshi la uingereza na kupewa cheo na namba.

Mbuzi huyo mweupe alioneshwa akipita kwenye gwaride lililoandaliwa huku akiwa ametinga Uniform zake za kijeshi huku akipigiwa saluti na wanajeshi wa gwaride. Afande Mbuzi huyo anaishi kambini na wanajeshi wenzake na anasehemu yake maalum ya kukaa.

Aidha afande huyo aliepatikana kwa msaada wa familia ya kifalme alionekana mtulivu na mwenye bashasha wakati anakagua gwaride hilo huku wanajeshi wengine wakimshangaa na wakati huohuo wakimpigia saluti.


 
Mbuzi ni alama ya shetani, jaribuni kucheck alama na nembo za illuminates utaona wanavyomtumia mbuzi....!
 
Kwa baadhi yetu hapa mtu atakuja ku refer hapa mbona uingereza walifanya hivi!
 
Nikuwaga siamini haya mambo ya freemasons sasa kama napata hisia hivi...alama ya pembe za mbuzi na kichwa chake
 
Tena walisema mbuzi huyo mjeshi ataleta bahati njema jeshini!
 
Hii sio ajabu kwani hata jeshi moja la Spain Lina mbuzi/Kondoo na wanafanya nae paredi siku ya majeshi. Legion de Melilla ni jeshi lenye Kambi 2 , Melilla mji uliopo afrika ila unatawaliwa na Uhispania,na Kambi yao ya pili ipo Almeria. Kikosi hichi maalum ni jeshi lenye mchanganyiko wa mataifa, kama Legionnaire ya Ufaransa. Jina lao la utani wanaitwa " el novio de la muerte " mchumba wa kifo ......tafuta YouTube ....le legion de Melilla
 
Huyo mbuzi anaitaji kisu tu..Ushetani unazidi duh!!...
 
Ni utamaduni wa Uingereza ambapo tangu karne ya 16 Malkia hutoa mbuzi kwa jeshi la Uingereza ambaye hupewa nambari ya jeshi na cheo.
Kazi yake kubwa ni kushiriki magwaride
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…