Afande Kova Haya Mamlaka ya Kutafsiri Hisia za watu Kuandamana Umeyatoa wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afande Kova Haya Mamlaka ya Kutafsiri Hisia za watu Kuandamana Umeyatoa wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by INFORMANT, Dec 27, 2010.

 1. I

  INFORMANT Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesikia Clouds FM Afande Kova amekataa kutoa the so called Kibali cha maandamano ya kesho saa mbili asubuhi na kusema kuwa hakuna kiongozi wa juu wa Serikali aliyeyakataa madai ya katiba mpya hivyo hakuna haja ya kuandamana.

  Hivi?????

  Huyu ndugu haya mamlaka kayatoa wapi?

  Polisi huyu, kamanda huyu, haya mamlaka ya kutafsiri hisia za wananchi na kuyafanyia maamuzi kana kwamba yeye ndio mahakama kayatoa wapi????

  Huu kama si ukuadi kwa serikali nini?

  Ninavyoelewa na kwa kadiri katiba ya nchi inavyoelekeza, kinachoombwa kwa polisi si kibali bali ni wananchi kutoa taarifa ya dhamira yao kufanya maandamano (kueleza hisia) na polisi wanawajibika kutoa ulinzi na kuhakikisha amani inatamalaki katika hiyo shughuli ya kutekeleza uhuru wa kikatiba na si vinginevyo...

  Majukumu ya polisi yanaishia hapo kulinda amani basi!!!

  Huyu ndugu huu upupu kautoa wapi?

  Nawasilisha
   
 2. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hapa huwa ndo nachoshwa na hawa watu(police),hivi huko ccp huwa wanafanywa nini hasa hata wanakosa busara ktk utendaji wao wa kazi?Haiingii akilini kuzuia haki ya kuandamana eti kwa kuwa wakubwa wamekubali suala la katiba mpya,si ujuha huu.Inavyoonekana huyu bwana hafahamu lolote juu ya suala hili,nani amemwambia kuwa serikali imesharidhia hoja hii?
   
 3. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Wananchi wakiandamana na kudai ni haki yao kula kinyesi polisi wanatakiwa wawepo kutoa ulinzi, si kuanza kutafsiri kwamba bwana afya kasema kinyesi si chakula!!!! Maneno aliyoongea Afande Kova si yake, amejazwa mdomoni, nina hakika na hilo..angekua na busara angekataa amri ya wanasiasa, ila kwa vile aliwahi kusema, na nanukuu....."mimi hata ndugu yangu wa darasa la saba namtafutia nafasi, nchi hii bila kujuana hali ni ngumu...", sitashangaa kwamba alishindwa kuiga mema ya Basilio...nina tofauti za kimtazamo na Julius Mtatitro, hasa kwenye wakati gani hasa umma unatakiwa ushirikishwe kudai haki, lakini katika hili nipo nae 100% na kesho nitaenda kweny maandamano!!!!
   
 4. M

  Msenshe Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Kova labda karogwa,hana hata hoja ya msingi kwa sababu kuandamana ni kutaka yafanyike mabadiliko ya katiba haraka wala sio wenyewe wakitaka hao waliomtuma. Akili ndogo aliyonayo hafai kuwa alipo.
   
 5. T

  Taso JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,652
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  hapana

  wao wamesema wanataka kuandamana kudai haki yao ya kula kinyesi, yeye kasema hatoi kibali kwa sababu hakuna aliyekataliwa kula kinyesi. Sio kwa sababu bwana afya kasema kinyesi si chakula.

  yani, hamuwezi kusababisha mji kurindima na songombingo za maandamano mkidai kitu ambacho Waziri Mkuu keshasema hakijakatazwa.

  Kova kakosea nini
   
 6. M

  Msenshe Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usipotoshe, waziri mkuu angekuwa na nia angekuja na ratiba ya mchakato utakavyoendeshwa sio kutuambia atamshauri rais. Kwa nini wasingekutana kwanza then ndo aongee na wahariri,au kulikuwa na haraka ya nini?? Hao wote wasanii,watu waandamane jumuiya ya kimataifa nayo isikie kilio itusaidie kuthga presha. VIONGOZI WETU HAWAAMINIKI.
   
 7. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ifahamike kuwa Pinda hakuueleza umma wa watz msimamo wa serikali,bali msimamo wake binafsi,pia akasema atamshauri rais juu ya suala hili.mara hii mmeshasahau jamani,lol!
   
 8. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Unajitahidi, lakini kumbuka kama wanataka kula kinyesi, si kazi pia ya Kova kusema hawajanyimwa, sio msimamizi wa zoezi la wao kupewa kinyesi...ataje ratiba basi ya mabadiliko ya katiba basi, si anajidai anajua mchakato!!! Pili, kuandamana kwa amani ni haki ya wananchi, mji kurindima na songombingo ni suala jingine, kama vp unabaki nyumbani ili kuepuka hizo songombingo...otherwise basi na sisi tuendao City Centre tuanze kugoma kwa vile foleni imezidi, au foleni sio songombingo??
   
 9. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Unajitahidi, lakini kumbuka kama wanataka kula kinyesi, si kazi pia ya Kova kusema hawajanyimwa, sio msimamizi wa zoezi la wao kupewa kinyesi...ataje ratiba ya mabadiliko ya katiba basi, si anajidai anaujua mchakato!!! Pili, kuandamana kwa amani ni haki ya wananchi, mji kurindima na songombingo ni suala jingine, kama vp unabaki nyumbani ili kuepuka hizo songombingo...otherwise basi na sisi tuendao City Centre tuanze kugoma kwa vile foleni imezidi, au foleni sio songombingo??
   
 10. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi... Maandamano hufanywa kwa vitu vilivyokatazwa tu???!! Maandamano yanaweza kufanywa hata kwa ajili ya kuunga mkono kitu au jambo fulani!!!! Au kudai jambo fulani lifanyike kwa kasi au haraka zaidi!! Kumbuka Justice delayed is justice denied!!! Mimi hata kinachokufanya uone Kova hajakosea sikioni!!! "Oppression of freedom of expression".
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Kingekuwa chama cha upinzani kinataka kufanya maandamano kingepewa kibali, sasa CUF wapo serikalini si wakaongelee huko ikulu kama kuna mahitaji wanataka!!!!
  Huu mimi naona kama ni mchezo wa kuigiza tu, viongozi wa CUF wamejaa unafki mtupu, eti Mtatiro Anasema kesho lazima waandamane na yeye ndio atakaeongoza hayo maandano! shame on Mtatiro.
  Ushauri wa bure kama kuna mwana CUF anaesoma thread hii sasa hivi halafu atafakari wananchi waliouwawa pemba kwa ajili ya mwehu mmoja kuwachochea wenzake nao wakaingia mkenge wakizani huyo bwana alikuwa na uchungu nao, kumbe alikuwa na uchungu na tumbo lake, hawezi kumsikiliza mwehu mwingine leo kumshawishi upumbavu.
  Ukweli ulio wazi ni kwamba CUF imepoteza uhalali wa kuaminiwa tena na Watanganyika.
   
 12. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  For lol, lini kova umechaguliwa au kuteuliwa kuwa mwanasiasa?
   
 13. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Kali kuliko....kumbe hata huku Bara CUF ni watawala??? So tetesi kwamba Lipumba analipwa na serikali ni za kweli??
   
 14. z

  zamlock JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  jamani maandamani yataanzia wapi na mimi nataka nikashiriki
   
Loading...