AET | Nigeria 0-0 Morocco (Pen 2-4) | AFCON 2025 | Nusu Fainali | Stade Prince Moulay Abdallah

AET | Nigeria 0-0 Morocco (Pen 2-4) | AFCON 2025 | Nusu Fainali | Stade Prince Moulay Abdallah

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Nigeria vs Morocco katika Nusu Fainali ya AFCON 2025 mchezo uliopangwa kufanyika kwenye Stade Prince Moulay Abdallah, Rabat ni pambano la kihistoria kati ya nchi mbili kuu za soka barani Afrika ambazo zote zimefika kwenye hatua hii bila kupoteza mechi yoyote katika mashindano haya.

Nigeria ina rekodi ya kushinda mechi zote tano walizocheza kwenye fainali hizi, ikifunga angalau mabao mawili kila mchezo kiashiria nguvu zao za kikosi mashambulizi wakiongozwa na nyota kama Victor Osimhen.

Wenyeji Morocco pia wako kwenye kiwango kizuri, wakiwa na safu thabiti ya ulinzi na washambuliaji bora kama Brahim Díaz aliyeonyesha ubora kwa kufunga mechi zote tano za timu yake hadi sasa.

Hivi hapa vikosi vya timu zote:

NIGERIA


1768418605511.png


MOROCCO

1768418955366.png
Updates

Mechi imeanza kwa speed ya kawaida ikiwa ni dakika ya 5

Dakika 11, ya mchezo milango ya timu zote 2 bado ni migumu 0-0

Dakika 20, bado 0-0 mechi ni firee

Dakika 31, mechi ni ya moto sana ila hakuna magoli hadi sasa

Dakika 40, bado hakuna goli hadi sasa

Dakika 45, za kipindi cha kwanza zimekamilika

Dakika 45 za kipindi cha pili zimenza

Mechi inazidi kuwa tamu dakika 60 ya mchezo

Dakika 85, Ngoma bado ngumu 0-0

Morocco waleeeeeeeeeeee.......fainali. Tukutane Januari 18, 2026

AET (After Extra Time) Nigeria 0-0 Morocco (Pen: 2-4)
IMG_0572.jpeg
 
Back
Top Bottom