Adui wa mwanamke ni mwanamke

Adui wa mwanamke ni mwanamke

Naona wapo kimya,wanajua huu ndyo ukweli 96%,si unaona hata wabunge kina mama wanatukanana kupitia mitandao,hawajali hata heshima ya nafasi zao.Hawa viumbe ni noma eti,na yote hiyo chanzo ni mabuzi.
 
Hamna tofauti na sisi wanaume. Adui wa mwanaume pia ni mwanaume. Nenda ofisini, mhudumu mwanaume atashughulikia mwanammke akuache we we mwanaume mwenzake. Nenda kutafuta kazi, mwanamke mwenye vigezo vya chini kukuliko atapewa wewe unyimwe kama mhajiri ni mwanaume. Kapande mat (daladala), concodi (taniboi) atamuongelesha mwanamke kwa heshima na we we atakuharakisha kama mtoto.


Hanna tofauti. hata wanaume ni maadui wa wanaume wenzao.
 
Wanawake wanapotetea haki yao wanakua na umoja sana,lakini linapokuja suala la haki/maendeleo ya mwanamke mmoja wanakua wanapingana na kupigana majungu na fitina, mfano cheo kazini,uzuri,kipato na hata kwenye kugombea uongozi wako tayari kumpa mwanaume kuliko mwanamke mwenzao.

Mfano hai mkubwa wa maisha yote- mwanaume anapoona rafiki yake wa kiume ana mke/binti mzuri sana na yeye atatafuta mwanamke mzuri zaidi au kama yule, lakini mwanamke walio wengi mwenzie akiwa na mwanaume mzuri na mjuvi basi atafanya juu chini amuibe na kutembea nae.

Je kweli adui wa maendeleo ya mwanamke ni mwanamke mwenzie majibu tafadhali- muongozo; majibu ya kilusinde lusinde hayaruhusiwi.

mkuu nishawahi kuja na sred hapa ikisema sumu ya mwanamke ni mwanamke mwenzie, msemo huu niliupata toka kwa wazee wa kiisilamu wakipongeza uisilamu kuoa wake hadi wanne, wakasema mwanamke akijua kuna mwenzake lazima akiri irudi sawa tu.
 
Back
Top Bottom