Adidas yatoa mpira wenye sensa (smart ball)

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
[h=1]ADIDAS YATOA MPIRA WENYE SENSA (SMART BALL)[/h]
  • user.png
    By Mwandishi Wetu
  • date.png
    23:30

​
Kampuni ya adidas wametoa mpra wa miguu ambao una uwezo wa kutoa takwimu za mchezaji na kupeleka kwenye gajaeti za iOS, yaani iPhone, iPad na iPod Touch kwa kutumia app ya Micoach. Mpira huo unajulikana kama Micoach Smart Ball una sensa mbali mbali ikiwemo bluetooth.

Mbali na mpira huo kuchukua takwimu kwa ajili ya kuchambua uchezaji wako, kasi ya mashuti, jinsi unavyopindisha free kick na kadhalika app ya mpira huo pia hutoa maelekezo mbali mbali ambayo yatasaidia jinsi unavyocheza mpira, hasa katika mambo kama vile freekick kona na kupiga mashuti. Miongoni mwa mambo maalum yanayofundishwa na app ya Micoach ni jinsi ya kuumudu mprira (ball mastery), kupiga mpira (ball striking), kupiga mashuti (striking with power) na jinsi ya kupindisha au kuvusha mpira kwenye ukuta wa freekick (around the wall na over the wall).

Hivyo takwimu ambazo utazipata zinakuwa kama vile kasi ya shuti lako ni 70 mph ma spin ni 48 rpm. Hivyo hii Micoach smart ball pia itakuwezesha kujua ni kiasi gani unaweza ku-spin mpira na kwa kasi gani. Mbali ya hayo pia inataoa takwimu zinazoweza kuonyesha umahiri wa kipa na hata ubora wa pasi zako. Mpria huo una chaji isiyo na waya na pia una kisahani (cradle) cha kuchajia.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mshambuliaji wa Spain na Man City Alvaro Negredo akiwa na Micoach Smart Ball[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Adidas ndio kampuni rasmi itakayotengeneza mipira itakayotumika kwenye Kombe la Dunia huko Brazil mwaka huu. Micoach smart ball utauzwa kwa $299 za kimarekani. Mipira hii itauzwa na Adidas wenyewe pamoja na maduka karibu mia nne ya Apple.

[FONT=Oswald, sans-serif]Chanzo: [/FONT]http://www.gajetek.com/2014/05/adidas-yatoa-mpira-wenye-sensa-smart.html

Kwa mpira kama huu ya nini kutumia wireless charging huku wangeweza kabisa kufanya conversion ya kicks into electricity.. unavozidi kucheza ndivo unavozidi kujichaji.. Ni vizuri kuona wenzetu kila siku wamekaa wanafikiria kufanya mambo mapya, sasa hili kila kitu kinakua smart... fridge, wallet, hadi meza, kiti, tv, taa, jiko, kitanda, miwani, milango, dirisha hadi hanger za nguo, tunaenda pazuri sana
 
Hawa wanataka kuharibu dhana ya mpira kwa taarifa yako,wewe fanya technologia ya marefa, kamera na viwanja lakini unapogusa mpira wenyewe unaweza ukaharibu ladha yake,mfano kwa kuweka technlogia hiyo yumukini mpira huo unaweza ukabadili speed ama hata velocity yake.Haya yangu macho utaanza kusikia complain very soon kuhusiana na mipira hiyo
 
Unadhani vyote hivo havijafikiriwa? ni kitendo cha kubalance pressure tu na mpira utaruka kama mpira mwingine...
 
Sawa kabisa hata mimi nilitaka kuongelea suala hili, technology itahalibu mpira kabisa
 
Unadhani vyote hivo havijafikiriwa? ni kitendo cha kubalance pressure tu na mpira utaruka kama mpira mwingine...

Unakumbuka mpira wa Jabulani uliotengezwa na hawahawa Adidas kipindi cha kombe la dunia South Africa 2010.Si unakumbuka magolikipa walivokuwa wanalalamika kuwa ulikuwa umekaa vibaya maana walisema kuwa ulikuwa unateleza na sometime unafanya deflection pasipo wao kutegemea?Tegemea malalamiko ya namna hiyo hata hii mipira mipya ya Brazil 2014 kwa sababu haijatestiwa na watumiaji bali imetestiwa na watengenezaji.Huamini ntakuja siku moja humuhumu kukukumbusha
 
Nipo nasubiri uje unikumbushe
 
Back
Top Bottom