Adhari ya kurudiana na mpenzi wa zamani

Adhari ya kurudiana na mpenzi wa zamani

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Madhara ya kurudiana na mpenzi wa zamani:

Kwa kawaida watu walioishi kwenye mahusiano wanajua mazuri na mabaya waliyokutana nayo, wanajua kila aina ya changamoto walizopita..
Uzito wa mapenzi yao wanaujua wao.
Kuachana kwenye mahusiano ya kimapenzi ni jambo la kawaida lakini linaacha madhara makubwa ndani ya moyo wa mtu.

Kitendo cha kuachana na baadae kurudiana siyo kosa na ni hatua nzuri zaidi ya kujifunza mlipokuwa mmekosea.

Mpaka kufikia hatua ya kurudiana maana yake kuna mmojawapo ameleta hoja na nia ya kutaka kuurudisha uhusiano huo au kuna mtu amekuwa kiunganishi cha kutaka mrudiane,anaweza kuwa mtoto mliezaa au rafiki,ndugu au mchungaji...

Zipo sababu nyingi zinaweza kuwafanya mrudiane japo mlikuwa mmeachana muda mrefu..

Lakini kabla hujafanya maamzi hayo lazima ujiulize maswali yafuatayo:

1.Je, kwanini anataka mrudiane tena?
Ni vigumu sana kujua nia yake ya kutaka kurudiana,huenda kuna vitu alikuwa anapata kutoka kwako amevikosa huko alipokuwa amekimbilia,
Lakin pia huenda huko amepigwa chini ,au tabia za huyo alipokimbilia anaona bora ya zako,au kuna kitu anataka kulipa kisasi kwako au kukufanyia kibaya dhidi ya huyu ulienae ili umkose,au huenda kweli mwanzoni alipitiwa amekuja kwa nia ya dhati au kashauriwa na watu.
Yote haya ni ya kujiuliza na yanawezekana...

2. Je, ni kipi kilisababisha mwanzoni mkaachana?
Hili pia ni swali la msingi ili ufanye ulinganifu kama kweli ilikuwa sababu ya msingi kwake kukuacha. Mfano, kama alikuacha kwa kufumania SMS ya mapenzi kny simu yako, je, akija kuifumania tena kwa bahati mbaya na penyewe atakuacha?
Sababu iliyowaachanisha mwanzoni ifanyiwe ulinganifu .

3. Je, ni madhara gani yalikupata kipindi anakuacha?
Huenda kuna vitu mlikuwa mmefanya kwa maendeleo yenu hatimae vikasambaratika kwa sababu ya kuachana,uliumia,ulidhalilika,ulijutia muda wako uliopoteza nk..hayo yote yatazame...

4. Mlipoachana hapo kati kati amekutana na wangapi na kwann ameachana nao?
Kumbuka nae kama binadamu mlipoachana huenda aliingia kny mahusiano mapya..

Baada ya kujiuliza maswali yote hayo iruhusu akili yako ifanye maamzi yatakayofaa kwa usalama wa moyo wako...

MADHARA YAKE:

1. UAMINIFU KUPOTEA

Pamoja na kurudiana kwa ahadi nyingi na zenye mbwembwe za kila aina, ni vigumu kumwamini tena kama zamani kwa sababu ya kurudisha kumbu kumbu juu ya kile kilichowafanya muachane mwanzoni hasa pale mtakapokoseana tena.

2. KUPOTEZA HESHIMA YAKO.

Heshima yako inaweza kupotea au kushuka kwa yeye mwenyewe kukudharau na kukuona ulikosa soko ndo maana umekubali kurudiana nae..
Lakin pia jamii na wazaz wanaweza kukudharau na kukushushia heshima iwapo chanzo cha kuachana mwanzoni kilikuwa cha fedheha na walikijua.

3. KUUKARIBISHA UMASIKINI.

Huenda ulikuwa umefika hatua nzuri ya kimaendeleo ndo maana anataka mrudiane ili azitumie mali zako kupitia mlango wa kurudiana kimapenzi.
Kama alikuwa mwenye tamaa ya Mali ,amini utarudi kny umaskini wa kujitakia..

4. UWEZEKANO MKUBWA WA KUUMIZWA TENA.

Kutokana na sababu zake mwenyewe za kuamua kurudiana na wew,anaweza kukuumiza zaidi kwa sababu huenda hao aliokuwa nao kipindi mmeachana bado mapenzi yao yapo hai kwa hiyo kukuumiza kimapenzi tena inaweza kuwa rahisi kuliko hata mwanzo.

5. KUPOTEZA MUDA.

Siku zote wanasema muda ni Mali,kama alishindwa kuthamini muda wako uliotumia kwake mwanzoni, amini hata sasa ni nahisi kukupotezea tena muda wa kufanya mambo yako mhimu na kukuachanisha na waliokuwa na mapenzi ya dhati kwako

6. UWEZEKANO WA KULETEWA MAGONJWA.

Ni mara chache sana wapenzi wanaorudiana kukumbuka kupima afya tena,wanaporudi kwenye ulevi wa mapenzi husahau kuwa huenda ameshapata magonjwa humwamini moja kwa moja na kwenda kichwa kichwa kumbe kashaoza.

Mwisho:
Simaanishi haitakiwi kurudiana na wapenzi wa zamani lakin ni vema ukafahamu baadhi ya madhara yanayoweza kukupata baada ya kurudiana..
Ni vema ukatafakari kwa kina kabla ya kufanya maamzi ili ujiridhishe kwa hiari usiende kwa mihemko ya maneno na misaada anayokupatia...
 
Hapo Namba 6.
Kuletewa Magonjwa, Ndo Kitu Kinachonifanya Kamwe Nisirudiane Na kambi Pinzani.
 
Kupasha viporo kuna madhara kwa Afya. Kwanza nirudiane na ex kwa lipi?
 
Nilimuacha maana wakati nipo nae hela haikai mfuko ulikua kama vile umetoboka ila alikua na papuchi ya moto moto hatari sana hio kitu
 
Mamamamamaamamae,yaani nilirudie lile shetani lenye mguu mmoja,halifai hata kidogo lile janamke.sijui limo humu.
 
Hii mada imekuja wakati husika usithubutu na wala usirudiane kamwe na mwenza ambaye mliachana kwa sababu yoyote ile endapo hakuna kinachowaunganisha kama mtoto.
Binafsi ni mhanga wa hili swala, maana nilimpenda sana classmate wangu wa primary kwa Kipindi tukiwa level ya shule ya msingi sikuweza kurusha ndoano, ikafikia secondary tukawa twawasiliana kwa barua maana ilikua miaka ya 2000's. Alipomaliza nikawa najiendea kwao maana wazazi wake walikua hawashindi nyumbani, siku ya siku nikarusha ndoano nikatolewa nje. Kumbe Kuna jamaa anakujaga hapo kwao hata mimi nikiwepo kumbe ndio alikua anahudumia mzigo hapo ilikua 2007 hivi jamaa akapewa cha mtoto.
Urafiki ukaendelea tukaja potezana, 2011 mwanzoni nashangaa namba geni inanipigia, akawa ni huyo classmate. Nikaingiza gear ikakubali nakumbuka ilikua pasaka nikawa nimetunukiwa tunda nami japo tayari alikua anajilinda na kutopata tena mtoto kwa kinga ya njiti, mchezo ukaendelea wee hadi mid of 2013 nikabagwa kwa sababu isiyo na kichwa wala mkia nikaumia zangu miez kadhaa nikasahau.
Mwaka jana mwezi wa kumi mwishoni naona namba mpya tena akawa ni yeye, kwa kuwa nilikua nimemmiss na nilikua sipo na mtu baada ya kumbwaga ambaye nilikua nae kama august hiyo hiyo mwaka jana nikaona hapa sasa nishapata pa kuponea. Akaandaa appointment tutaonana akalipia bills japo nilikua na zangu mfukoni akaniambia nikimwita sehemu ndio hatojinunulia hata chewing gum itakua juu yangu.
Siku zikasonga kama week mbili tokea anitafute nikaanza gusia kupasha kiporo maana nae wakati tunaonana aliniambia bado hajabahatika kupata mwanaume anayeeleweka, nikamwambia anidhihirishie kwa kunipa tunda wala hakutia shaka japo aliomba nitumie kinga maana tuna muda hatujakutana na kila mtu alikua na mapito yake nikaona sio mbaya.
Lengo langu ilikua nipige na kuondoka Ila kwa huduma ile niliyopewa nikajikuta nazama kabisa japo alishaniumiza mwanzoni, gemu zikaendelea japo kuanzia ya pili ngoma ilikua dry. Tulikumbushana mengi akaomba samahani nyingi nikaona kashapevuka akili zaidi kumbe bado ana mambo mengi nyuma ya pazia, maana jamaa ambaye aliniambia walikua wapenzi na washaachana bado mawasiliano yapo na jamaa kaseviwa jina la kike. Na kila nikiwa nae Jioni baada ya kazi simu inazimwa, nikafanya upekuzi huu mwez uliopita tukiwa tumelala nikawasha sim yake Si ndio meseji zinamiminika nilichoka nikajikaza kukakucha. Asubuhi mapema nikamwambia nimepata dharura natoka akiondoka aniachie funguo kwa jirani, Jioni yake nikawa nishatuliza mawazo nikafanya mahojiano nae nikamweleza kuwa yeye ni mtu mzima simpangii maisha ya kuishi ndio ikawa goodbye.

Nilitumia muda na kiasi kingi kukuza biashara na vikundi vyake kumbe bado utulivu wa mahusiano hana.

Wakuu mnisamehe kwa urefu huu wa comment japo nimejaribu ku summarize.
 
Back
Top Bottom