Adhabu za wanajeshi

Adhabu za wanajeshi

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
7,149
Reaction score
28,858
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.

Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!

MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.

Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!

Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.

Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
 
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.

Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
 
Kwenye pitapita zangu nikaingia kwenye eneo la Jeshi kukata majani ya kulisha ng'ombe. Mbele yangu kulikuwa na maembe dodo yanatamanisha sana. Sasa mimi sikujua kama ni eneo la jeshi.

Nikaenda chini ya embe dodo nikaanza kuyapopoa maembe.

Muda kidogo naona pale nilipoacha mkokoteni wa kubebea majani kuna mtu amekaa na magwanda, huku anazuga anaongea na simu.

Oya, siisahau ile siku.
 
35a3ab62-2d1f-461a-9fb1-4b67d97c5de9.jpg

Nilipewa maembe mabichi nile yote
Wale wajeda walaaniwe
 
Mimi nimesoma shule ya jeshi pale jitegemee jkt mgulani.
1. kuna siku moja kuna captain × alinichapa bakora nne kisa ninamzidi urefu! Yani alikuwa anafundisha nikamwambia sir naomba ruhusa niende chooni! Yani hapo hapo akabadilika kabisa, ety kwann unanizidi urefu alafu mimi nina nyota tatu???

Mzee zilitembea bakora, kuanzia siku hiyo nilikuwa namshangaaa sana yule afande.

02.Tukio la pili ni siku ya kwanza kwenda pale shuleni! Ilikuwa form five!
Aisee kwanza nilienda shule saa mbili ahsubui, nikamkuta MP anaitwa MSENGI. Akaniweka bakora nne, huwezi amini day one.

Nikaanza kwenda mdogomdogo, kuna sehemu wanaita smart area hurusiwi kutembea yani unatakiwa kupita nduki.. sikuwa najua.
Alooo alikuwa afande mmoja anaitwa kiyarunzi ni coplo hapo hapo nilikula bakora sita.

Aisee nikaanza kuona hii shule sio machozi yananilenga, huyo mdogomdogo mpaka class.
Kufika class namkuta captain shemahonge anafundisha kwa machungu nikagonga mlango mfululizo akasema unatutukana akampigia afande dani akaja mbio na bakora nne.akamwambka huyo kaja hapa anatukana

Mpige sjta....huwezi amini nikasema nikitoka humu ndani sirudi tena.. nikala sita kila mtu ananishangaaa nalio kisa mboko sita.

Nikaingia class nakakutana na wana nikawaadisia msanga.basi saa nne ikafika tukaenda canteen.

Sasa mwisho wa kuingia canteen na kutoka ni saa nne na nusu.
Mimi nilikuwa nakunywa supu mpaka saa nne na 40 aloooooh

Nilipigwa bakora za mgongo nikamwaga supu mbio nikasema huu ni usenge..nkasepa class
Nashukuru Mungu sikifuata.

Siku ya kwanza nilipigwa zaidi ya bakora 16
 
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao,utajuta kuwafahamu.

Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini,kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande

Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
 
Nakumbuka 2009 nikiwa ndani ya kigoma, nilipewa adhabu ya kujaza pipa kwa kijiko...

Ntaludi kumalizia but usiombe ujae angle za hao jamaa.
Naona mnajifagilia siku hizi hatuwashobokei ni wa kawaida sana,,,migwanda tu mpaka mashoga wapo jeshini cku hz,,,vijana wengi wengi saizi unfit jeshi limekuwa ajira kama ajira nyingine
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Unasema tu
Watu kamaa nyie ndio popo kishenzi.
Utapigwa mpaka usemee mimi ni mwanamke natafuta mme
 
Mimi nimesoma shule ya jeshi pale jitegemee jkt mgulani.
1. kuna siku moja kuna captain × alinichapa bakora nne kisa ninamzidi urefu! Yani alikuwa anafundisha nikamwambia sir naomba ruhusa niende chooni! Yani hapo hapo akabadilika kabisa, ety kwann unanizidi urefu alafu mimi nina nyota tatu???

Mzee zilitembea bakora, kuanzia siku hiyo nilikuwa namshangaaa sana yule afande.

02.Tukio la pili ni siku ya kwanza kwenda pale shuleni! Ilikuwa form five!
Aisee kwanza nilienda shule saa mbili ahsubui, nikamkuta MP anaitwa MSENGI. Akaniweka bakora nne, huwezi amini day one.

Nikaanza kwenda mdogomdogo, kuna sehemu wanaita smart area hurusiwi kutembea yani unatakiwa kupita nduki.. sikuwa najua.
Alooo alikuwa afande mmoja anaitwa kiyarunzi ni coplo hapo hapo nilikula bakora sita.

Aisee nikaanza kuona hii shule sio machozi yananilenga, huyo mdogomdogo mpaka class.
Kufika class namkuta captain shemahonge anafundisha kwa machungu nikagonga mlango mfululizo akasema unatutukana akampigia afande dani akaja mbio na bakora nne.akamwambka huyo kaja hapa anatukana

Mpige sjta....huwezi amini nikasema nikitoka humu ndani sirudi tena.. nikala sita kila mtu ananishangaaa nalio kisa mboko sita.

Nikaingia class nakakutana na wana nikawaadisia msanga.basi saa nne ikafika tukaenda canteen.

Sasa mwisho wa kuingia canteen na kutoka ni saa nne na nusu.
Mimi nilikuwa nakunywa supu mpaka saa nne na 40 aloooooh

Nilipigwa bakora za mgongo nikamwaga supu mbio nikasema huu ni usenge..nkasepa class
Nashukuru Mungu sikifuata.

Siku ya kwanza nilipigwa zaidi ya bakora 16
Msalimie Capt alando
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Unapatikana wapi
 
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.

Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
Mpaka umuone mkubwa wao labda iwe tu ni bahati yako

Kama askari tu anazinguliwa na akitaka zinapigwa na hakuna anaefukuzwa kazi(kuna mjeshi alizinguliwa na polisi,akaenda kambini akawashitua wana,wana wakavamia kituo cha polis kikapigwa),na sikusikia mtu katimliwa
 
Mimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja

Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
kwa ulevi huo usingetofautisha kati ya askari na kibaka
 
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.

Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
Hayaja kukuta wewe🤣 ushawahi kuibeba dunia
 
Back
Top Bottom