Adhabu ya viboko mashuleni bado ni muhimu?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,331
Reaction score
17,582
Viboko/mijeredi vimetumika kwa miaka mingi kama nyenzo muhimu ya kufundishia mashuleni hasa katika elimu za msingi na secondary. Mwalimu haamini kama kuna njia ingine nzuri ya kufanya Kwa mwanafunzi mkosefu.

Katika Zama hizi ambazo mwalimu anakabiliwa na shida nyingi za kipato, madeni, malazi, maladhi, usafiri, uhaba wa vifaa vya kufundishia, ongezeko kubwa la wanafunzi darasani na ongezeko la tegemezi (ndugu, jamaa,) na kupanda Kwa gharama za maisha walimu hawako fit kimwili na kiakili. Kosa dogo tu la mwanafunzi linaweza kuwasha (trigger ) mitambo ya msululu wa shida za mwalimu na kumtoa kwenye control ya balance kati ya nguvu zake,majukumu yake, wajibu wake na akili yake. Hii ikitokea mwalimu anaweza kutoa adhabu kwa mtoto asiyoijua aina yake, ukubwa wake na matokeo yake.

Katika zama hizi za walimu kuandamwa na shida nyingi, na maendeleo ya kijamii adhabu ya viboko mashuleni iendelee kutumika?
 
fimbo ni lazima
wachapwe tu kama mtoto wako umemshindwa wewe haimaanishi atashindwa na wote

walimu chapeni tu mpaka akiolewa akamuoneshe mumewe alama za ujinga wake shuleni
 
Wakati mnaangalia stress zinazomkabili mwalimu msisahau pia aina ya watoto wa siku hizi ambao ni watundu kupitiliza, wenye viburi na wajuaji.

Viboko sio adhabu nzuri katika mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ila mazingira ya shule zetu yanalazimu hii adhabu itumike. Fikiria mwalimu ampe mwanafunzi adhabu ya kumwagilia kiunga cha maua kila siku kwa muda wa wiki moja, halafu mwanafunzi huyo anaacha kuja shule kwa wiki 2, mwalimu anampa adhabu ya kubaki kujisomea shuleni kwa mwezi lakini mwanafunzi anaondoka vinginevyo asimamiwe na mwalimu husika, wakati huohuo huyu mwalimu anatakiwa akajishughulishe baada ya kazi ili kujiongezea kipato.

Mazingira kama hayo na mengineyo ndio huwalazimu walimu kutumia fimbo kuwaadhibu wanafunzi. Msilinganishe mazingira ya shule binafsi na shule za umma ambazo mzazi hana hata muda wa kumfuatilia mwanae maana hana uchungu wa pesa (elimu bure)
 
Viboko ni muhimu na vitaendelea kua muhimu maisha yote

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Viboko/mijeredi vimetumika kwa miaka mingi kama nyenzo muhimu ya kufundishia mashuleni hasa katika elimu za msingi na secondary. Mwalimu haamini kama kuna njia ingine nzuri ya kufanya Kwa mwanafunzi mkosefu.

Katika Zama hizi ambazo mwalimu anakabiliwa na shida nyingi za kipato, madeni, malazi, maladhi, usafiri, uhaba wa vifaa vya kufundishia, ongezeko kubwa la wanafunzi darasani na ongezeko la tegemezi (ndugu, jamaa,) na kupanda Kwa gharama za maisha walimu hawako fit kimwili na kiakili. Kosa dogo tu la mwanafunzi linaweza kuwasha (trigger ) mitambo ya msululu wa shida za mwalimu na kumtoa kwenye control ya balance kati ya nguvu zake,majukumu yake, wajibu wake na akili yake. Hii ikitokea mwalimu anaweza kutoa adhabu kwa mtoto asiyoijua aina yake, ukubwa wake na matokeo yake.

Katika zama hizi za walimu kuandamwa na shida nyingi, na maendeleo ya kijamii adhabu ya viboko mashuleni iendelee kutumika?
Ndio
 
Atakaye mchapa mwanangu atakiona cha mmeza kuni.
 
Viboko ni adhabu nzuri sana ukiitoa toto linanyooka ila walimu na wazazi inatakiwa kuitoa kwa uangalifu sana fimbo mbili za matako ambazo unajua ataumia kidogo lakini hata pata tatizo sio kuchapa kwa sifa na nguvu kama unapiga mnyama matokeo mtoto roho inaacha mwili unaingia kwenye matatizo.
 
Sure
 
Wakati mnaangalia stress zinazomkabili mwalimu msisahau pia aina ya watoto wa siku hizi ambao ni watundu kupitiliza, wenye viburi na wajuaji.

Viboko sio adhabu nzuri katika mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ila mazingira ya shule zetu yanalazimu hii adhabu itumike. Fikiria mwalimu ampe mwanafunzi adhabu ya kumwagilia kiunga cha maua kila siku kwa muda wa wiki moja, halafu mwanafunzi huyo anaacha kuja shule kwa wiki 2, mwalimu anampa adhabu ya kubaki kujisomea shuleni kwa mwezi lakini mwanafunzi anaondoka vinginevyo asimamiwe na mwalimu husika, wakati huohuo huyu mwalimu anatakiwa akajishughulishe baada ya kazi ili kujiongezea kipato.

Mazingira kama hayo na mengineyo ndio huwalazimu walimu kutumia fimbo kuwaadhibu wanafunzi. Msilinganishe mazingira ya shule binafsi na shule za umma ambazo mzazi hana hata muda wa kumfuatilia mwanae maana hana uchungu wa pesa (elimu bure)

Tazizo wala sio watoto wa siku hizi bali wazazi wa siku hizi ambao hawana muda wa kukaa na watoto wao, wanaolala chumba kimoja na watoto wao, wanaowatuma watoto wao kwenda kuwaletea sigara, pombe na vileo vingine. Kwani mwl lazima amchape mtoto wa watu, hana adhabu nyingine zaidi ya kiboko? Kwani mtoto sipofaulu mwl hapati mshahara wake? Mbona wazungu wameshaachana na adhabu za kijinga hizo?
 
Unaamini bakers inafuta ujinga ujinga?

Nilidhani tunawaadhibu baada ya kugundua makosa yao na wayaache
Nilijibu kwa utani.

BTW, Suala la viboko linahitaji debate kubwa na kufanya tafiti za kueleweka na liwashirikishe wadau wa elimu hasa Wanafunzi, Walimu, Wazazi.

-Ujinga wa mtoto haufutiki kwa viboko.

-Ujinga wa mtoto unaweza kutokana na uzembe wake.

-Uzembe wa mtoto unaweza kufutwa kwa adhabu zinazofanana na fimbo au fimbo.

-Kuna shule Nazijua zinachapa na kuna nazozijua hazichapi. Ndani ya hizo hakuna jibu la moja kwa moja linaloonyesha mtoto akichapwa anafaulu au asipochapwa anafaulu.

[haki za mtoto] hili ni kubwa zaidi kwenye macho ya walio wengi kuliko wengi wanavyoliangalia kielimu]
 
Kudos
 
Back
Top Bottom