Adhabu ninayoipata tangu nihamie chumba cha master, nipeni maujanja

Mambo vipi,

Uzi huu ni spesho kwa waliopanga au wenye nyumba za masta tu nikimaanisha choo kipo kwenye chumba cha kulala, Hivi karibuni nimeama kutoka chumba kimoja chenye choo cha nje na kuhamia chumba cha kodi elfu50 choo cha ndani.

Sasa tatzo kila nikikata gogo harufu inarudi chumbani chumba chote kinakuwa puyaaaa daaaah nakereka sana kama kuna sabauni au Air fresh nzuri ya chooni naomba mnielekeze kukata hii harufu.
Tatizo sio choo,wewe itakua unakula sana maharage na dagaa
 
Wakati mwengine mambo kama haya unatafuta hata fundi hapo mtaani unamshirikisha ili akupe njia ya kusawazisha baadhi ya mambo otherwise utadhalilika kama inavyotokea hapa.

Siyo kwamba humwagi maji mengi uchafu ukaenda hiyo hali inatokana na mgandamizo wa hewa kwenye shimo kubwa nje,obviously tatizo lipo kwenye line ya kutoka chooni (humo ndani) kwenda kwenye septic tank hawakuweka bomba mmabadala kuzuia harufu isirudi ndani,fanya hivi.

Kama pale kwenye shimo kubwa nje imewekwa bomba moja ita fundi akuwekee lingine hapo lilipotokea bomba la kusafirisha uchafu (namaanisha hapo karibu kabisa na ukuta wa choo chako cha ndani) hiyo hali itaisha.
Mkuu, hapa mimi nimekuelewa vizuri sana.

Lakini nina mashaka kama mleta mada atakuelewa. Anyway, nafikiri mleta mada anatakiwa alete fundi ili abadilishe discharge leni kutoka ya kawaida na awekewe ile yenye kufanana na shingo ya bata.

Ile pipe ya shingo ya bata inafaa zaidi kwasababu itaweza kuzuwia hewa inayo rudi ndani kwa kubakiza masalia ya maji kidogo yatakayo tuama na kufanya mgandamizo wa hewa isirudi ndani
Ushauri mzuri kabisa huu. Pia fundi anaweza akaangalia kama kwenye sink la choo hicho waliweka P trap inayosaidia kubakiza maji unayotumia kuflash choo. Hayo maji hubaki hapo ili kuzuia harufu toka shimoni (septic tank) kuja ndani. Kama hiyo p trap ipo basi aiangalie kama iliwekwa vizuri.

Otherwise, maelezo ya ujumbe hapo juu yahusike. Inshort hilo tatizo sio lakutatua kwa sabuni. Unless huflash vizuri.
Correct, hiyo shingo ya bata huitwa "P trap"
Mafundi uchwara mara nyingi hawaiweki hiyo either kwakukwepa gharama yakuinunua, au levels za kuiset ili iendane la level ya bomba linalopeleka huo uchafu kwenye shimo. Ni muhimu sana hiyo katika zoezi la uzuiaji wa harufu kurudi ndani
Mkuu, kama ukiweza mwambie mwenye nyumba abadikishe mfumo wa maji taka na aweke hiyo pipe Kama ni choo cha kuchuchumaa, lakini kama ni choo cha kukaa aweke cha kufanana na hiyo niliyo ambatanisha pichaView attachment 1591530View attachment 1591531
Nimewaelewa vizuri sana wakuu.

Isipokua me naona kama nimemuelewa mtoa mada tofauti.
Tatizo lake sio harufu kutoka kwenye shimo kurudi ndani, maana kwa ushauri wenu hapo juu, mmemshauri kutatua tatizo la harufu kutoka septic tank kurudi ndani.

Yeye anatatizo la harufu kutoka kwenye uchafu fresh kutoka tumboni ukiwa kwenye sink, kabla yakwenda kwenye septic tank. Kawaida hii harufu haitakiwi kurudi chumbani, inatakiwa kuisha ikitokea kwenye ventilation za chooni

Amesema hivi..
Kila akitoka kukata gogo harufu inarudi chumbani, sio harufu yakutoka kwenye shimo, ni harufu ya kinyesi kipya kinachokua kwenye sink, kabla hakijaenda kwenye shimo
 
1601926921694.png

hii P-trap au S Trap ni ya dongo ulaya wengine wanaita ceramic mtaani zipo nzuri za orange na bei yake haivuki 3,000 kote kwenye maHardware, unachotakiwa unakata kakipande kengine ka bomba hilo la upana wa inchi 4 angalau urefu wa inchi 4 unabandika juu yake halafu unaweka choo cha kuchuchumaa Eastern Type, hicho kilichoongezeka kinaficha mzigo uliouweka na hakihitaji maji mengi kuuondoa mzigo unakutana na maji ambapo maji hayo yanakata harufu kabisa CHOO HIKI HAKIFAI KWA MASTER KABISA
Choo cha kukaa Western Type ndio kinatakiwa kukaa kwenye master na majengo yote ya ghorofa P-Trap yake imejengewa mumo humo ili maji yatuwame kukata harufu, sasa hapo maji lazima yawe mengi ili kuflash

S or P Trap
An S-trap or P-trap refers to the water seal at the bottom of the toilet that stops sewer gases and smells escaping into your bathroom. The set out of a toilet outlet refers to the outlet drainage point location.
 
Mkuu, hapa mimi nimekuelewa vizuri sana.

Lakini nina mashaka kama mleta mada atakuelewa. Anyway, nafikiri mleta mada anatakiwa alete fundi ili abadilishe discharge leni kutoka ya kawaida na awekewe ile yenye kufanana na shingo ya bata.

Ile pipe ya shingo ya bata inafaa zaidi kwasababu itaweza kuzuwia hewa inayo rudi ndani kwa kubakiza masalia ya maji kidogo yatakayo tuama na kufanya mgandamizo wa hewa isirudi ndani
Sawasawa kabisa mkuu,na azingatie sana ulichokiandika hapo paragraph ya mwisho.
 
Nina mawazo ya tofauti kidogo mkuu, masink yote huwa yanasetiwa na kitu inaitwa P-trap au S -trap. Hii kazi yake ni kubakiza maji kwenye mfumo/njia nzima ya maji taka kati ya inlet na outlet(kwenye shimo au sewer). Hivyo hakuna harufu inayotoka kwenye sewer (bomba la maji taka la moja kwa moja bila septic tank) kurudi ndani ya nyumba.
Kwa ufupi ajitahidi tu usafi + perfume/air freshner. Zipo nyingi tu mbona.
Wakati mwengine mambo kama haya unatafuta hata fundi hapo mtaani unamshirikisha ili akupe njia ya kusawazisha baadhi ya mambo otherwise utadhalilika kama inavyotokea hapa.

Siyo kwamba humwagi maji mengi uchafu ukaenda hiyo hali inatokana na mgandamizo wa hewa kwenye shimo kubwa nje,obviously tatizo lipo kwenye line ya kutoka chooni (humo ndani) kwenda kwenye septic tank hawakuweka bomba mmabadala kuzuia harufu isirudi ndani,fanya hivi.

Kama pale kwenye shimo kubwa nje imewekwa bomba moja ita fundi akuwekee lingine hapo lilipotokea bomba la kusafirisha uchafu (namaanisha hapo karibu kabisa na ukuta wa choo chako cha ndani) hiyo hali itaisha.
 
Nina mawazo ya tofauti kidogo mkuu, masink yote huwa yanasetiwa na kitu inaitwa P-trap au S -trap. Hii kazi yake ni kubakiza maji kwenye mfumo/njia nzima ya maji taka kati ya inlet na outlet(kwenye shimo au sewer). Hivyo hakuna harufu inayotoka kwenye sewer (bomba la maji taka la moja kwa moja bila septic tank) kurudi ndani ya nyumba.
Kwa ufupi ajitahidi tu usafi + perfume/air freshner. Zipo nyingi tu mbona.

Mkuu upo sawa kiasi but fanya uchunguzi wako vizuri, hakuna kinachoishinda harufu ya kinyesi, septic tank likichemka kisawa sawa mchana kutwa na jua la bongo linavyowaka kama hakuna njia ya kupumulia nje ya line ya kurudi ndani tule tumaji tunakobaki kwenye sink hugeuka uchafu na kutoa harufu mbaya kama shimo la choo limehamia ndani.

Na siku hizi ukikutana na mafundi wazuri wanashauri kuwekwa pipe line mbili kwa ajili ya shimo kupumua, moja kwenye shimo lenyewe na nyingine katikati ya chamber A&B, au hizi nyumba za kisasa tunazojenga zenye vyoo ndani bomba za kutoa harufu nje iwekwe moja kwenye septec tank yenyewe na moja katikati ya choo cha master na choo cha public au kama vyumba vyote vina choo pipe iwekwe kwenye chamber ndogo zinapokutana line zake pamoja na kwenye sink ziwekwe hizi P/S trap,hapo inakuwa shwari mno!
 
Tena wakati mwengine bila hata harufuu dawa ni maji mengi kama choo hakina tatizo
Kwanza shida kuu hapo hakuna P trap ya kudaka maji ili harufu from septic tank isije ndani. Pili kama ni choo cha kuchuchumaa jitahidi uwe kila mzigo ukidondoka mwaga maji ili harufu isisambae. Hapa ndiyo utaona faida ya choo cha kukaa maana mzigo ukishuka unatua kwenye maji kabla harufu haijasambaa.
 
Wengi hawajaelewa mada.

Anyway, suluhisho hapo ni kujitahidi kula matunda na maji kwa wingi. Pia jitahidi kupunguza kiwango cha chumvi kwenye chakula. Nadhani itasaidia
Acha uwongo, bora ungesema ale mbogamboga kwa wingi...
 
Tumia maji mengi Ku flash choo na pia nunua sabuni za chooni zinatosha tuu , Kama unaishi sehem maji ni ya shida, hama hapo haraka
ahsante mkuu japo nilitaman kujua aina ya sabun mnayotumia ninyi ili nami niitafute maana natumiaga deto ila naona kama sijarizika nayo.
 
Back
Top Bottom