Adhabu kali za viboko kwa watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adhabu kali za viboko kwa watoto

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mopaozi, Mar 22, 2012.

 1. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali kama humpendi utamchukia mwanawo; Ila kama unampenda utamrudi mapema …. Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.

  Kuna usemi usemao “Mkunje samaki angali mbichi” huu ni ukweli, make ukitaka kumkunja samaki mkavu anavunjika, na usemi mwingine unasema “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”.

  *Kila kunapokucha kuna ongezeko kubwa la idadi ya watoto na Vijana ambao ni mzigo kwa wazazi na jamii kutokana na tabia zao. Utasikia akina mama wanalalamika wakisema “Heri tumbo hili lisingezaa”. Kuna watoto na Vijana ambao ni Mizigo isiyobebeka. Lakini hebu tujiulize chanzo chake ni nini? Kwa sehemu kubwa, tatizo ni malezi tangia walipozaliwa.

  *

  Sasa hivi kuna haki za watoto, nchi zingine ukimpiga mtoto wako unapelekwa mahakamani, hivyo mzazi haruhusiwi kumrudi mtoto anapofanya ujinga, pia kuna sheria hadi mashuleni ya kutowachapa watoto viboko. Lakini hata majumbani wazazi wengi wamewafanya watoto kama mayai, mtoto ni usiniguse, wanadekezwa hadi wanakuwa mazezeta, utakuta mtoto analia lia ovyo bila sababu, anataka chochote wakati wowote, na mzazi anakubaliana naye, huku anaendeshwa kama gari bovu. Watoto wamejaa ujeuri, ni wasumbufu hadi kwenye majumba ya Ibada, wamejaa viburi na ukorofi, ukijaribu kuwakemea usishangae kukutana na TUSI au Kukufyonya huku akitoa jicho ka mjusi aliyebanwa na mlango.

  *

  Wazazi wengi hawana Muda wa kukaa na kuchunguza tabia za watoto, lakini kibaya zaidi ni pale wanapoona ni Ustaarabu au Maendeleo kutowarudi watoto, HIYO NI HATARI, akina mama wengi utasikia wanasema, “Nitamwambia Baba yako akirudi” huku baba mwenyewe anarudi majogoo, huo ni udhaifu mkubwa, mama chukua hatua ya kumrudi mtoto akikushinda ndipo utafute msaada. Siku moja nilisikia Binti akisema “Nitakunywa Sumu” na mama aksema “Basi mwanangu nenda usijenifia bure” alikuwa anamkataza kwemda kwa “Boy Friend” wake. Hayo sio malezi, wazazi lazima tuwe na msimamo au laa kesho ni Majuto.

  *

  TAHADHARI:

  Tumia hekima na busra unapoamua kumwadhibu mtoto, usitoe adhabu ukiwa na hasira, usimwadhibu mtoto kwa kila kosa, usimwadhibu mtoto bila ya yeye kulielewa kosa lake. Wazazi wengi ni wakali na wakorofi kwa watoto, hatimaye wamewafanya watoto kuwa Sugu. Ukali na Hasira havisaidii, wengine kosa dogo tu anamrushia stuli, mara Kofi na tusi juu, mara anamtandika na mwiko wa ugali wa moto, au chohote kilicho mbele yake, huo sio ustaarabu, unaharibu watoto. Fimbo ni hatua ya Mwisho baada ya kutumia kila njia ya kumwelimisha na kumuonya. Na umkalishe chini, umwambie kwa nini umeamua kumpa adhabu.
   
 2. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kumchapa mtoto sunna!
   
 3. A

  Ados Senior Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndg umenigusa katika , Neno lina sema 'mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha mpaka atakapo kuwa Mzee ,kwa hiyo basi mafundisho utakayompatia katika utoto wake pamoja na fimbo itakuwa kumbukumbu katika maisha yake
   
 4. papason

  papason JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Salamboko kwa kwenda mbele adi mtoto anyolokee vilivyo!
  Hiyo ndiyo sera yangu pale nitakapo jaaliwa watoto!
  Full Stop.
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  hatushangai picha ya wu-tang inajidhihirisha ulivyo mtu wa fujo:A S-baby::flypig:
   
Loading...