adhabu ipi 'tamu'?

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,846
Hivi adhabu gani ya kifo inamfaa 'muuaji sugu', (serial killer)?... i.e mtu kamlawiti/kumnajisi mtoto/kikongwe kisha kamnyonga/kamchinja (victim wake) mpaka kufa nk... ili iwe 'funzo' kwa 'wanaotamani' kuua...?

...apigwe mawe hadi afe, (stoning)

...akatwe kichwa, (beheading)

...anyongwe hadi afe, (hanging)

Imagine;... hangman makes the noose too short a drop that the prisoner 'slowly' strangles, or too long a drop that the prisoner can be decapitated!

...apigwe sindano ya sumu afe, (Lethal injection)

...apigwe shoti ya umeme hadi afe, (Electric chair)

...apigwe risasi hadi afe, (firing squad)

...awekewe gesi ya sumu hadi afe, (poison gas)

kati ya hizo, ipi 'inafaa' sana kwa magereza yetu Tanzania?
 
Tatizo ni kwamba akishakufa hatupati tena muda wa kumsikia na kufahamu alijisikiaje. Kama kweli alijutia kosa au la. Nafikiri mtu kama huyu ahasiwe halafu akatwe mkono mmoja. Tumwache jamii imkejeli,,, hapo ataipata tamu yake!!
 

Bw. Mchongoma,

Vipi tena mzee? Mambo makubwa na yanayotisha haya! Nafikiri yanasisimua kwa kuyaongelea tu!

Anyway, I don't support death penalty. So kwa maoni yangu, adhabu zote hizo hazifai.
 

Mi naona kipimo ambacho huyo mpimaji kawapimia wenzie nae apimiwe hicho hicho, ila cha kwake kishindiliwe na kusukwasukwa. Kufuta adhabu ya kifo ndio kunafanya madhambi haya yazidikila uchao. Naweza kukosolewa kwa hili, ila naunga mkono adhabu ya kifo.
 

Mimi nadhani badala ya kujadili adhabu gani inafaa kwa watu hawa,tuanze kujadili kama adhabu ya kifo iendelee kutumika hapo Tanzania ama iondolewe.Mimi nafikiri muda na wakati muafaka wa kuifuta adhabu ya kifo "Death Penalty or Capital Punishment" kwenye nchi yetu ndo huu.Tusijirudishe nyuma,tujisogeze mbele.Adhabu ya kifo mimi sikubaliani nayo na wala siungi mkono nchi yoyote ile duniani inayotekeleza hii adhabu.
 
Bw. Mchongoma,

Vipi tena mzee? Mambo makubwa na yanayotisha haya! Nafikiri yanasisimua kwa kuyaongelea tu!

Anyway, I don't support death penalty. So kwa maoni yangu, adhabu zote hizo hazifai.

...QM, ha ha ha... unajua matendo ya ubakaji watoto yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku, au labda ndio uhuru wa vyombo vya habari? ...


...sawa Mkuu, ila ukisoma hii habari, unadhani huyo 'mtuhumiwa' sugu adhabu gani inamstahili, gerezani keshapazoea!

 

...takwimu nazo zinasemaje;...

 
Mimi nadhani badala ya kujadili adhabu gani inafaa kwa watu hawa,tuanze kujadili kama adhabu ya kifo iendelee kutumika hapo Tanzania ama iondolewe.Mimi nafikiri muda na wakati muafaka wa kuifuta adhabu ya kifo "

Nakubaliana nawe Brown..Capital punishment should be abolished is against humanity, kama hatuwezi tutengeneza uhai basi tusiutoe kwa namna yeyote ile.. adhabu kubwa iwe kifungo cha maisha ....ama miaka mingi jela ie 30-50 hivi
 
kama hamna adhabu inayostahili, Mob justice kama hii itakuwa 'kama kawaida'!...

 
Nakubaliana nawe Brown..Capital punishment should be abolished is against humanity, kama hatuwezi tutengeneza uhai basi tusiutoe kwa namna yeyote ile.. adhabu kubwa iwe kifungo cha maisha ....ama miaka mingi jela ie 30-50 hivi

...Mkuu Ushirombo, kwa mazingira ya magereza yetu, unategemea atapata 'fundisho' kwa kosa alilofanya? fikiria kama huyu;

Mwenyekiti wa Kijiji, Issah Swedi, alisema mtuhumiwa Mile aliyetoroka inasemekana alitoka gerezani hivi karibuni baada ya kumaliza kutumikia kifungo kwa makosa ya ubakaji na kwamba amekuwa na uzoefu wa kuishi gerezani kuliko uraiani

...alishamaliza kutumikia kifungo huyo, halafu kawabaka na kuwalawiti wale watoto mpaka kawaua! huyo unatarajia kifungo kitamsaidia nini?

mimi naona anafaa kupigwa nyundo kwenye korodani zake mpaka afe!!!
 
Wale wote wanaopinga adhabu ya Kifo aidha wanategemea au wana hofu kuwa kuna siku wanaweza kubaka au kuuwa kwa kukusudia. Kwao wanaona ni bora ukibaka au ukiuwa kwa kukusudi, jamii ikuonee huruma na kukumbatia kwa machafu na dhurma uliyoifanya...! je unaweza kupima adhari anayopata m'bakwaji.. au adhari anayopata mfiwa kwa kufiwa na Baba, Mama au mtoto...?!

Umepoteza uhai wa mtu kwa kumuondolea uhai wake au umebaka kwa tamaa zako za mwili, kisha unategemea ukale na kulala bure JELA huku ukilindwa na kupewa matibabu kila inapobidi...!?

Je wewe ukibakwa au kupoteza Mtoto au Dada, au Mke na kisha hukumu ikapitishwa kuwa muuwaji amefungwa miaka 10 jela na baada ya kutumikia miaka 6 akapewa parole na yupo mtaani anaendelea na maisha utafanya nini?
Fikiri kabla ya kujibu, siku moja unaweza kuwa Mhanga wa kubakwa... au unataka ukipigwa shavu hili ugeuze na la pili?
 
huwezi kujua uzito wa jambo mpaka liwe limekupata. mungu akuepushie mbali.ila jaalia una mwanao au mke,au mama kipenzi na akaja jamaa akamtoa roho mbele ya macho yako huku unaangalia ,aidha kwa kumchinja au kumbaka au namna yeyote ile. je zungumza kiukweli kabisa . kipi kitakata kiu ya kisasi chako?. nadhani hata akiuliwa basi utaona haijatosha. unasema unayoyasema kwasababu halijakukuta wewe, hivyo , "mzigo wa mwenzio unauona kanda la usufi".
 

...kifungo cha maisha Bw Kisigi anaona hakimu anamuonea! yeye alipokuwa 'kamkunja' binti wa miaka mitano na kilio chote kabinti hako kalivyokuwa kanaugulia maumivu kwa 'kuchanwa chanwa' sehemu zake za siri...

imagine; uchungu, na woga ulokuwa umemkabili huyo binti maskini!

...inaelekea 'asingefumwa' angekatoa roho hako kabinti kupoteza ushahidi, na DNA testing ilivyo 'ghali' kwa forensic examination Bongo... labda Bw Kasigi angeendelea 'kutesa' tu mtaani!

huyu adhabu ambayo ingemfaa ni ile ya 'kutwangwa' mawe hadi afe!
 
Mama na mwana watoa ushahidi dhidi ya Nguza

...lakini twendeni mbele tukirudi nyuma, hivi ni kweli Babu Seya na wanawe wote walikuwa na haka kamtindo wajemeni?... au 'ushahidi haukutosha'?


...hawa wamefungwa maisha vile?

...halafu Mzee Maumba fundi cherahani wa Ilala yeye alifungwa miaka 30? yuko wapi, au keshakufa!?
 

Nakubaliana nawe Brown..Capital punishment should be abolished is against humanity, kama hatuwezi tutengeneza uhai basi tusiutoe kwa namna yeyote ile.. adhabu kubwa iwe kifungo cha maisha ....ama miaka mingi jela ie 30-50 hivi

...sawa wakuu, lakini mnaposoma habari kama hii;


...hamuoni haja ya adhabu 'inayostahili' kwa wauaji walofanya ukatili huu ni kifo tu?
 

...nahitimisha;



...bado naamini hukumu ya kifo bado inastahili Tanzania haswa kwa kuzingatia jinsi vitendo vya mauaji baada ya ubakaji, kama 'vinavyoripotiwa', vinazidi kuongezeka haswa 'victims' ambao wengi wao ni watoto wadogo na vikongwe.

Mbaya zaidi, vitendo hivyo vina'rutubishwa' zaidi kutokana na imani potofu za ushirikina ikiwemo 'kujiongezea' bahati ama 'kujiponya' UKIMWI!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…