ADHABU gani zinafaa kwa watoto? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ADHABU gani zinafaa kwa watoto?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Exaud J. Makyao, Jan 8, 2010.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na kampeni nyingi za kutetea haki za watoto mashuleni na mahali pengine popote.

  Moja kati ya suala tata katika haki za watoto ni kama watoto waadhibiwe wanapokosa ua wasiadhibiwe kabisa.

  Na kama watoto wanapaswa kuadhibiwa wakosapo, waadhibiwe je na adhabu zipi zinafaa kwa watoto hadi umri wa miaka 18.

  Naomba mawazo ya wana jamii kuhusu jambo hili tata.
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  njia mojawapo ni kumnyima ktu anachopenda kwa ahadi kuwa akijirekebisha utampa!!

  Mind you "be loving but firm"
   
 3. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It sounds good bht, but si anweza kuwa mnafiki ili apate?
   
 4. bht

  bht JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  sio rahisi, samaki mkunje angali mbichi na umleavyo mwana ndivyo akuavyo. they cant pretend for long.

  mazoea hujenga tabia!!!! mwache mtoto azoee mambo mema then atakuwa na tabia njema automatically!!
   
 5. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekupata rafiki.
  Kulea ni kugumu sana.
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  saa nyingine unahisi hakuna formula duh!!!!
   
 7. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bht, nahisi kama wewe ni mwalimu mzuri wa watoto.
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  I love children Emma ukweli toka moyoni!!! nimefundisha sana children classes nikiwa sekondari and as we are tokin mimi ni mratibu wa such classes ni my rel.community!!!

  they are so precious, very unique and pure!!!
   
 9. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bht, Nimepatia kumbe.
  Natamani ningekuona uso kwa uso.Mie bado nasoma rafiki.Nahitaji kujifunza kwa watu kama wewe.
  You must be polite and slow angered.
  I feel so.
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hahaaa!!! i have several faces kulingana na tukio na mahali si unaelewa!!!

  mind u I started doing that nikiwa bado shule na si chuo!!!! passion is all that matters.
   
 11. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mhhh,
  Thanks.
   
 12. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Changamoto kweli.
   
 13. b

  bnhai JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Na kumchapa kidogo inafaa jamani. Siyo ya kumjeruhi hapana ni kumkumbusha. Na anatakiwa atambue kwanini amechapwa. Zipo adhabu nyingine km kumnyima anachokipenda au hata kumwambia akae sehem for some minitues then aseme kosa lake na kuomba msamaha. Ila hayo yote yanafaa yaambatane na maelezo kwanini ameadhibiwa
   
 14. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mimi huwa nawa finya kidogo wale wote ambao under 8

  Wale ambao ni above 8..uso unabadilika namkazia macho mpaka anatambua kwamba sipendi jambo hilo

  Finally nampa ushauri faida na hasara za kutofanya au kufanya jambo fulani kwake na kwa jamii hasa wale ambao wako above 8!

  Note: nothing like standard measures kwasababu kinder wana differ ile mbaya kwa tabia na situation ..it is all situtianal so it depends mtoto, historia yake tabia zake etc..
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakusahuri usimnyime mwanao anachopenda utamjengea sychological problem, ni heri umadhibu vingine lakini mpe anachopenda afurahi please.

  Pili usimtenge kwa lolote ni hatari anaweza kuwa mjeuri zaidi.
   
 16. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana nawe binhai,angalia sisi tulivyokuwa tunachapwa enzi zetu,na hapa tulipo sasa,viboko vinasaidia sana kwa watoto watukutu!!!
   
 17. u

  under_age JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2010
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  panapohitajika hasira, muoneshe hasira na papohitajika kupongezwa,mpongeze. akirudia kosa mara nyingi mchape kidogo kichapo ambacho hakitomuumiza. mjengee mazingira ya mapenzi ili ajirekebishe kutokana na mapenzi yako zaidi kuliko adhabu.mtafutie marafiki wenye tabia njema ili aige tabia njema katika umri huu ambao kila mtoto analoliona anaiga na kuweka akilini.
   
 18. b

  bnhai JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Tumaini adhabu si kwa kosa linaloonekana tu. Hata kwa kutofikia target. Manweka malengo ya kufanya homework na hayafikii, ni lazima weekend moja umpumzishe nyumbani ili afikirie upya namna ya kuhandle uvivu wake.
   
 19. October

  October JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe 100% viboko vinasaidia sana na mimi ni shahidi. Viboko vilinisaidia sana kunifanya niwe nilivyo. Cha kuangalia ni usimchape mtoto wakati una hasira kwa sababu unaweza muumiza, halafu hakikisha unamuelewesha kwa nini unamchapa ili ajue kosa lake.
   
 20. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  malezi ya watoto ni complex sana, hayana formula. adhabu muafaka hutegemeana kiwango cha "umri wa akili" na si umri wa miaka. kuna watoto ambao kiakili wako mbele kiumri kushinda miaka waliyo nayo. hapa ndipo panahitaji hekima, ukikosea kidogo, mtoto atakuchukia badala ya kujirudi.

  kuna jirani yetu mmoja tulipokuwa wadogo, hadi leo baba yake anamuogopa kwa sababu alikuja kugundua kuwa makosa yote aliyokuwa akimuadhibu alikuwa anamuonea! yaani mtoto alikuwa mbele kiakili kuliko umri wake na kwa kushindwa kubaini, baba alifikiri ana kiburi hivyoo akawa namuadhibu mara kwa mara. ni baaa ya ushauri nasaha ndio baba aligundua kuwa alikuwa anamuonea mwanae kila wakati alipomuadhibu utotoni na kwa kweli mtoto wake aliathirika sana kisaikolojia ikalazimu apewe shauri nasaha.

  siku moja nitawaletea kisa hiki kikamilifu kabla sijapiga kambi jimboni
   
Loading...