Adha ya "maji" UDSM ni...

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Ni siku ya nne leo maji hayapatikani udsm, kweli mambo hayaendi, vyooni na hakuingiliki!
Shukrani hata kwa haya maji ya clean water yanayoletwa.
Najua na ndugu zetu wengine waliopo nje ya Udsm wanapata adha kama ye2 POLENI PIA.
USHAURI: Dawasco mkiweza kurekebisha haraka itakuwa vyema. KWANI KUNA KILA DALILI ZA KURIPUKA MAGONJWA hasa Hall 5 na 2!!
 
Hili ni tatizo sugu. Hebu fikiria hata sisi tuliopitia hapo mwanzoni wa miaka ya 80's tulisota na tatizo la maji. Yaani mpaka leo ufumbuzi haujapatikana. Tutafika kweli?
 
Chukua hatua za haraka za Kuichukia ccm kwa kuipa Sapoti CDM ili tatizo hili la maji iwe historia
 
kazi mnayo na migorofa ilivyo mirefu vile inabidi mkajihelp vyoo vya ground halafu unarudi juu kupiga msuli...
bora yenu lakini sie uswazi tulishasahau hata kama kuna kitu kinaitwa clean water
"CCM OYEEEEEEEEEEEEE"
 
Chukua hatua za haraka za Kuichukia ccm kwa kuipa Sapoti CDM ili tatizo hili la maji iwe historia

Hii ni aina ya ahadi ambazo huleta mgongano kwa wananchi baadae. Watu waambiwe ukweli. Sio kwamba CDM ikiingia madarakani tu, ghafla nchi inakuwa ya maziwa na asali. Tuambieni kwamba maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe - kwa kufanya kazi na kujituma, sio kwa kukaa vijiweni.
 
Back
Top Bottom