DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mwenyekiti wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC), Shaban Itutu, ametoa wito kwa serikali kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wamachinga, mama lishe na vijana wa boda boda na bajaji, badala ya kuwaona kama kero za mijini.
Akizungumza Juni 29, 2025, katika Mkutano Maalum wa ADC wa kuchagua wagombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar, Itutu amesema kundi hilo kubwa la Watanzania linaishi maisha ya tabu kutokana na mfumo usiozingatia hali halisi ya uchumi wao.
Itutu amependekeza kujengwa kwa masoko rasmi ya kisasa katikati ya miji mikuu kama Dar es Salaam, akisema ni kosa kuwaweka wamachinga maeneo ya pembezoni ambapo wateja hawafiki na kwamba iwapo watapewa ridhaa ya kushika dola watatekeleza hilo haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa Itutu, hali ya sasa imeathiri vibaya maisha ya familia za kipato cha chini, na serikali inapaswa kuwa na dira ya kupunguza vikwazo vya kiuchumi badala ya kuviimarisha.