Adam Malima na RAS wako hapo Mara mjitathmini

Adam Malima na RAS wako hapo Mara mjitathmini

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
6,035
Reaction score
15,064
Mhe.Adama Malima kaka yangu mkubwa, WanaMara huwa hawana maneno mengi. Mimi nikwambie wiki hiii inayoisha leo 20/10 imekuwa Chungu sana kwa WanaMara. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba yametangazwa rasmi.

Mkoa wako wa Mara kwa mara ya Tatu mfululizo umekuwa wa 26 yaani umekuwa wa MWISHO KITAIFA kuanzia 2017, 2018 na sasa 2019. Kuna maswali meeengi sana kichwani, Je mmekuja kudidimiza Elimu, au na nyie ndio kazi kama ya yule RAS wa Morogoro kuhamishia Walimu wa kike Mjini.

Wakati mikoa kama Mtwara, Simiyu nk ikiingia kwenye Database ya Maafisa Elimu wanaofanya vizuri na kuwavuta kwenye Mikoa yao nyinyi hamueleweki Maofisini na wala hamuoni soni Mkoa wenu kuwa wa Mwisho. RC upo na RAS yupo wala hamuoni shida miaka mitatuuuuu!

Real mnatunyima Usingiziiii.
MKOA WA MARA HAUNA VILAZA, kama Mkuu wa Mkoa unabisha waulize watangulizi wako waliohakikisha Mkoa wa MARA UNAKUWA TANZANIA ONE KATIKA ELIMU;
Mrejee;
Mhe. NIMROD LUGOE
Mhe. JOSEPH BUTIKU
Mhe. Nsa Kaisi
Mhe. Stephen Wasira nk nk
Mnachofanya wewe na RAS wako kama mtaalamu hamuwatendei haki Watu wa Mara, kuna masuala ya Uongozi hayako vizuri.

Angalieni kwa jirani yenu SIMIYU Mhe.Mtaka kavuta kifaaa AFISA ELIMU MKOA sasa yupo TOP TEN kutokea nyie mlipo.

Nenda Mtwara waliokuwa Mkiani, Wamevuta Maafisa Elimu wa kazi toka Mbeya nk sasa wapo njema.

Mjitathmini sana kwa aibu mnazouletea Mkoa wenu, au kama ndiyo ajenda iloyowaleta kudidimiza Elimu imetosha sasa na inakera.

Kazi njema.
 
Mtoto wa kwanza na wa pili wote wametoka Serengeti

Unataka RC akawafanyie mtihani hao watoto
 
Kuanzia Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya(Butiama,Musoma, Serengeti), makatibu tawala(mkoa na wilaya zilizotajwa), wabunge na viongozi wengine katika mkoa wetu wajitathimini
 
Wewe unataka kamati za udanganiyifu kama wanavyofanya mikoa mingine?
 
Naona mmepata pa kusingizia....waandaeni vijana wenu kuanzia nyumbani...sasa nyie endeleeni kusubiri mkuu wa mkoa...
 
Mm siongei Mengi.

Namtaka Bw. Anthony Mtaka awe mkuu wa Mkoa wa MARA, JPM sikia kilio changu.

Au awanie Ubunge Musoma Vijijini.

Hao akina Adam Malima ukuu wa Mkoa ni vyeo vya fadhila kwa Baba zao vyeo serikalini na CCM. Unakuta akili za ki uongozi ni sawa na Bashite.

Kazi kunenepeana mitumbo tu!
 
Mm siongei Mengi.

Namtaka Bw. Anthony Mtaka awe mkuu wa Mkoa wa MARA, JPM sikia kilio changu.

Au awanie Ubunge Musoma Vijijini.

Hao akina Adam Malima ukuu wa Mkoa ni vyeo vya fadhila kwa Baba zao vyeo serikalini na CCM. Unakuta akili za ki uongozi ni sawa na Bashite.

Kazi kunenepeana mitumbo tu!
Mbunge wa Musoma vijijini/Butiama ni bonge la mzigo
 
Kuwa wa kwanza au wa mwisho sio ishu, ishu ni watoto wajue kusoma na kuandika na wafaulu mtihani,

Yawezekana wamepata maksi mazuri sana ila kwenye rank ni wa mwisho.

Mimi nilikuwaga nashika namba za mwisho mwisho darasani ,watoto wa walimu ndio walikuwa wakiongoza,Mimi naenda kuchunga ng'ombe na mbuzi naacha vipindi darasani.

Nilikuwa na nidhamu sanaaa, nilikuwa napenda kujisomea vitabu huko machungoni , nilichokitaka bi kujua kuhesabu ,kusoma na kuandika tu.

Mtihani wa la saba nilitoboa , nikaenda olevel- adv- chuo kikuu mzumbe- sasa hivi niko idara nyeti .

Sasa nyie komaeni na kuwa wa kwanza tu. Badala ya kuwafundisha watoto kuelewa masomo.

Sent from my TECNO CA6 using JamiiForums mobile app
 
hivi unategemea mtu kama Malima na Ule mtumbo wake kama mtungi wa gesi alete maendeleo yoyote kwenye ule mkoa?
 
Back
Top Bottom