Adakwa kwa kunajisi mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adakwa kwa kunajisi mtoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Kijiji cha Mawenjeni Kata ya Mwika Kusini, aliyetambulika kwa jina la Msafiri Msuya (36) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka 9 na kumsababishia maumivu na kutokwa damu.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Yusuf Ilembo alisema mtuhumiwa huyo alimdanganya mtoto huyo wa darasa la pili kuwa atampatia fedha mnamo Januari 12 mwaka huu majira ya saa nane mchana kabla ya kumfanyia unyama huo.

  Alisema mara baada ya kumdanganya mtoto huyo, alimpeleka kwenye shamba la migomba na kumfanyia kitendo hicho ndipo mtoto huyo alipopiga kelele baada ya kusikia maumivu makali.

  Kwa mujibu wa Kamanda Ilembo wananchi wa eneo hilo walimkuta mtoto huyo akitokwa na damu nyingi na mtuhumiwa alikuwa amekimbia.

  Alisema wananchi walijitolea kumtafuta na walifanikiwa kumkamata na kumfikisha katika kituo kidogo cha Polisi Himo.

  Kaimu Kamanda Ilembo alisema mtoto anaendelea na matibabu katika Hospitali Teule ya St. Joseph iliyopo katika Manispaa ya Moshi.
   
Loading...