Ada ya mja

LUCAS KISIMIR

Member
Sep 11, 2012
29
4
UTANGULIZI
Nimeisoma makala nyingine ya Kibanda yenye kichwa kisemacho; “KINANA NI KIMBUNGA” baada ya ile ya kwanza iliyojinadi kwa kichwa kisemacho; “NAMWOGOPA KINANA”. Mwandishi huyu ni hodari sana katika masuala yenye kuhitaji kufanyiwa uchambuzi. Ni msomi mbobezi katika fani yake, mwenye kutenda kazi iboreshwayo na kipaji cha kipekee cha kuzaliwa. Tusisubiri Mtanzania mwenzetu huyu afariki ndipo tummwagie sifa zake anazostahili. Tufanye hivyo sasa ili apate moyo zaidi wa kuendelea kujitolea kutufumbua na kutufundisha sisi tulio-tayari na wenye hamu ya kujiimarisha zaidi kifikra, ki-upeo na kimtazamo. Kwa sehemu kubwa, Kibanda ni darubini muhimu sana kwenye tasnia yake na ndani ya kizazi hiki. Namfananisha na kauli ya Kibiblia isemayo kuhusu SAUTI YA MTU ALIAYE NYIKANI kwa wale wenye msingi wa imani inayokubaliana na falsafa hiyo. Ni rasilimali muhimu kujihusisha nayo kwa majadiliano ya kina katika masuala ya kijamii. Rasilimali bora inapokuwa ng’ambo ya korongo, kuingia gharama ili uitumie kwa manufaa mapana zaidi ni jambo la busara. Kwa mantiki ya kawaida, huwezi kuichukia darubuni kwa kuwa imekusogezea taswira karibu zaidi, nawe ukapata kuona mambo kwa kiwango kilichoboreka ambacho hukipendi. Haya ni matokeo ya kujijenga na kujizoeza kukataa kuona details katika taswira, bali silhouette ili kukwepa kujishughulisha na uhalisia ambao daima ni mchakato unaochosha. Tabia hii ya kukwepa ukweli ni nyenzo ya kufanikisha kuishi kibwetekaji kama mbwekaji abwekaye bandani mwake.

Mtembea kwa miguu mwituni, asikiapo sauti ya kipekee ikitolewa na ndege kichakani au mtini, kwa vyovyote vile fahamu zake zitamwamuru kuchukua hadhari ingawa yeye mwenyewe haielewi lugha ya ndege yule. Ataubadili mwendo wake, kuyafungua masikio zaidi na macho pima, huku moyo ukimdunda kwa kasi iliyoongezeka! Kibanda sio ndege ambaye hata hivyo wenye hekima hawampuuzi, bali ni mtaalamu anayejitolea kuuelimisha umma wa leo ambao miongoni mwao, wengi hutumia masikio kama nyenzo ya kutundika hereni za kujipamba na kwa kusikiliza wanachokiamini. Kibanda endelea......, wa kukusikiliza atakusikiliza na kukuelewa na asiyekuelewa aongeze bidii kubishana nawe ili kuficha umbumbumbu wake. Huyu atafanana na aliyeuficha mwili wake nyuma ya kiganja cha mkono wake kwa kuamini kuwa ni kichaka! Achana na MADIKTETA!

Kibanda umetabiri masikio ya kufa, na hakuna dawa kwani historia imekwisha-waamulia mwelekeo wao. Wamejaliwa kuwa na muda wa kufanya maigizo yao kwa kujitolea na sasa wakipenda, watangulize makoti wakayatundike kwenye geti la Ikulu, baadaye tuyatumie kudeki viwanja vya Ikulu! Wanaukataa ukweli sio kwa kuwa hawaufahamu bali ni kwa kujifurahisha pasipo matumaini ya dhati. Wanaonesha uwepo wao kama samaki wanavyorukaruka majini. Kiashiria cha kuchoka kwao ki-hoja ni kuporomosha matusi na ukishaona hivyo ujue wamelemewa. Huwa nafurahi sana wanapotukana kwani hunidhibitishia kwamba wameishiwa na hoja, wakati waungwana tukipambanisha hoja kwa hoja na umma unaendelea kutupima kwa upeo na sio kwa kiwango kikubwa cha uongo na jazba. Uongo na jazba sio matakwa na sharti la uongozi bora bali ni nyenzo na rufani ya waishiwa (Getting a more mileage before taking a crush landing). A crush is just a crush, no matter sooner or later.

Kama sote tujuavyo, wanasiasa hawa wanaojitambulisha kwa kibandiko cha herufi za rangi nyekundu kuashiria umwagaji damu cha M4C yaani MASTERS FOR CRIMINALITY, huwashawishi wafuasi wao kupita wakiandamana kwa niaba ya magari juu ya lami ya CCM huku wakipoteza muda mwingi ambao ungefaa zaidi kutumika katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao kwa hoja zisizohitimishwa kwa tija bali damu na maumivu ya waghilibiwa wasio hatia. Maandamano yao huishia kwenye viwanja vya Serikali ya CCM, ili kukoleza porojo zao za ghilba wakipaaza sauti zao kwa teknolojia inayoendeshwa kwa nishati iliyopatikana kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo agenda yao inayosisitizwa ni kwamba CCM haijafanya kitu! Hapa ni kwamba wanazungumza kiswahili tu na sio kweli za msingi. They speak good Swahili but not the facts!

Kibanda songa mbele! Umesema; “Kama CHADEMA na mashabiki wanataka kupima kina cha maji kwa sababu tu ya ulevi wa fikra, basi wanao uhuru wa kufanya hivyo. Tusubiri fainali 2015. Huko ndiko tuendako”.

Kinana ni kiongozi mahiri, mtulivu, mbunifu na mwenye kuzungumza kwa hoja na MBOBEZI WA SIASA ZA KUONGOZA. Namwambia Kinana akaze buti aongoze mapambano nasi wanaCCM tupo pamoja naye angani, majini na nchi kavu! WanaCCM tunasema; hatukubali kubeba dhambi ya kuikabidhi nchi yetu kwa madikteta ambao hukerwa hata na tofauti ya kimawazo. Uporaji wa kikaya uliotinga mahakamani ni kiashiria tosha kwamba wakipata fursa hawaachi kitu!

CCM hivi sasa inajipanga kuongoza Awamu ya Tano kifikra na kifalsafa kwa kutumia mikakati na intelijensia ya ndani katika kufanikisha azma hiyo. Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo. Pamoja na mambo mengine, CCM ni KIINI cha kudumu cha IMANI NA MATUMAINI YA WATANZANIA.
 

wonishi

Member
Sep 18, 2012
25
5
Pamoja na nguvu yako ya hoja uliyoijenga hapa,bado hawa jamaa wa M4C na mashabiki wao watakuja na hoja za nguvu wakidhania cku hizi bado watanzania hawana upeo wa kuelewa.wameshastukiwa hawa jamaa.Automatically they have switched themselves to M4D(movement for DEATH)without there knowledge.waache waendelee wananchi wameshajua janja yao.majibu 2014 na 2015.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom