Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ADA-TADEA, Juma Ali Khatib, amesema chama chake hakina dhamira ya kumpinga Rais wa sasa, Dk. Hussein Ali Mwinyi, bali kinalenga kupata nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu za kugombea urais katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa Mwenyekiti wa Tume, Jaji George Kazi, Khatib alisema chama chake kimeamua kuwania urais ili kutimiza matakwa ya kisheria yanayowezesha mgombea kupata nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
“Sisi katika chama ADA- TADEA tumeamua kugombea urais wa Zanzibar kwa lengo la ,kupata nafasi ya pili, kuwa makamu wa kwanza wa rais" amesema Khatib, akisisitiza kwamba ADA-TADEA haina sababu ya kumpinga Rais Dk. Mwinyi.
Chanzo: BBC