Musundi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 1,583
- 2,600
Nisamehewe bure kama nitaonekana nasukumwa na umaskini wangu kuandika haya ninayoandika.
Kiukweli nimeshangaa na kukwazwa kusikia kuwa kuna shule hapa hapa bongo inayotoza Tshs. 34 milioni kama ada ya mtoto wa chekechea tu na Tshs. 70 milioni ada ya mtoto wa sekondari.
Mwenzenu najiuliza maswali kadhaa:
1. Hivi ni wabongo wenzetu wa humu humu wanaosomesha katika shule hii?
2. Hivi mtoto anayesomeshwa hapa anapewa elimu kwa Mtaala tofauti na huu wa Wizara ya Elimu ya Tanzania?
3. Hivi mtoto anayesomea hapo anaandaaliwa kuja kuishi maisha hapa hapa bongo au mahali pengine ulimwenguni?
4. Hivi ni nini hasa cha ziada kinachohalalisha ukubwa wa ada kiasi chote hiki?
5. Hivi serikali yetu inayofahamika kutetea wanyonge imeridhia na kubariki utozaji wa ada wa kiasi hiki?
Kama kuna mwenye kunisaidia majibu ya maswali yangu, natanguliza shukurani kwa msaada.
I'm really puzzled, mwenzenu!
Sent using Jamii Forums mobile app