ACT yatua Tarime kwa staili ya kipekee

ACT yatua Tarime kwa staili ya kipekee

USTAADHI

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
1,516
Reaction score
136
CHAMA cha siasa kinachojulikana kama ACT jana kilianza kazi rasmi ya kuvuruga mwenendo wa kisiasa ndani ya mji wa tarime imefahamika

Taarifa za kuaminika zilizotufikia zinaonesha kuwa jana wajumbe wasiojulikana nyadhifa zao waliotambulika kwa majina tu walionekana majira ya saa 11 jioni mpaka usiku wa manane wakipanga mikakati katika hotel moja (jina tunalo)wakiongozwa na mwenyekiti wao wa muda wa taifa

aliyeongozana na ndugu MSHUMBUSI (aliyekuwa katibu wa CHADEMA MWANZA) wengine walikuwa DAVID KATIKIRO (aliyekuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa mara (bavicha) aliyekula rushwa ya kuuza jimbo la musoma vijijini wengine waliofahamika kwa haraka ni mke wa marehemu CHACHA WANGWE ambaye anashiriki kumuandalia kijana wake nafasi ya kugombea pia aliyekuwa mwenyekiti wa CUF wilaya badae akahamia ADC mapema mwaka jana kabla hajaibukia ACT ( HUYU ANA SIFA YA KUWAHI KUWA NA KADI ZOTE ZA VYAMA ) maruufu kama THOMA FUNDI HALI ILIVYO KWA SASA;

kwa sasa taarifa zinasema wako kwenye hotel ya AMA iliyopo mjini wakigawa tsh 2000 kwa kila anayekubali kupokea kadi ya chama hicho tutaendelea kuwaJUZA zaidi mpango zaidi jambo la kipekee linaloshangaza wanatarime ni hii staili ya vikao vya usiku
2 ni hii staili ya chama kutumia fedha tena kubwa kiasi cha 2000 kupata mwanachama
3 nia aina ya wanachama ama viongozi kinaokusanya wenye sifa za kuchumia matumbo waliowahi ama kuhama hama bila ukomo ama wanaouza hata majimbo kwa sababu ya fedha
swali je hichi kitakuja kuwa chama cha kukomboa WATANZANIA? ama ni SACCOS ya CCM?
TUNAOMBA WALE MLIO NA UZOEFU WA KISIASA MTUSHAURI KAMA NI CHAMA CHA UKWELI AMA TUJIHADHARI?
 
mi naamini mienendo ya chama hichi cha ACT na staili yake ndiyo itakayoonesha kama ni cha wananchi ama ni intarahamwe
nasikitika pia kuhusu hii familia ya ndugu wangwe kwa nini wanaaibisha jina lao?
 
mi naamini mienendo ya chama hichi cha ACT na staili yake ndiyo itakayoonesha kama ni cha wananchi ama ni intarahamwe
nasikitika pia kuhusu hii familia ya ndugu wangwe kwa nini wanaaibisha jina lao?

Wanajiaibisha kwa lipi? Mbona chadema imemterekeza mjana na watoto wake wakati walimuua wangwe? Mbona hata chama hakimkumbuki marehemu kwenye mikutano ya chama hata dk 2 za kumuombea? Acheni unafiki.
 
Wanajiaibisha kwa lipi?
Mbona chadema imemterekeza mjana na watoto wake wakati walimuua wangwe?
Mbona hata chama hakimkumbuki marehemu kwenye mikutano ya chama hata dk
2 za kumuombea? Acheni unafiki.

We gamba umewahi kuwaona Ma Intarehamwe wakitumia walau dakika moja kumkumbuka Kolimba waliyemuua hadharani tena akiwa amenyosha mikono kuashiria amesarenda.?

BACK TANGANYIKA
 
Sasa na nyie kama mna wanachama wanaoweza kununuliwa kwa Sh. 2,000/= mjue man hali mbaya. Poleni sana. Ndio maana miCCM inaendelea kushinda.
 
Kuleni pesa zao kisha waacheni kwenye mataa.

Unajidanganya. Tayari ACT imeshapita Tarime. Wananchama 211 wameshahakikiwa. Leo Katavi, Shinyanga na Unguja kukamilisha zoezi. Poleni mnaoitakia mabaya.
 
Kiukweli habari hizi ni upotoshaji wa makusudi unaoendeleza watanzania wazidi kuielewa chadema wamezoea kuishi kwa uongo,jana chama cha ACT TANZANIA Kilikuwa kinafanya zoezi la uhakiki wa wanachama wao wadhamini,je unawapa watu kadi na kuwapa 2000 inakuaje hapo?wakati zoezi la uhakiki wa wanachama wadhamini hawa kadi mara ya mwisho walijazia mwezi wa pili na form ya kisheria ya udhamini kutumwa kwa msajiri na kadi hiyo anabaki nayo mwanachama,kwahyo zoezi hilo ni mwanachama kuja na kadi yake mbele ya msajiri na msajiri kuhakiki je kadi namba na jina linaendana?je mwanachama huyo aliyedhamini ndio yeye?na ili chama kipya kipate usajiri kinaitaji watu 200 katika mikoa 10 ya Tanzania.Taarifa nikupe mkoa wa Mara wamefanikisha zoezi la usajiri kwa muda mchache kuliko sehem nyingine yeyote zoezi lilianza sa3 hadi saa7 likawa limeisha na likapitiliza lengo la wadhamini 200 na chama mapema kikabidhiwa ithibati kuwa zoezi la uhakiki wa Usajiri wa wadhamini wa chama cha ACT TANZANIA ni halali na kweli walikuwepo,Elewa humuwezi kuishi kwa uongo maisha yenu yote ila ukweli utadhihirika na mtazidi umbuka tu,uongo huo mdangany mtu asioenda shule au ile misukule ya chadema
 
jamii forum imekua asehem ya wapuuzi siku hiz kueneza uwongo wao wa kiuchunguzi....
 
Hiki Chadema kimekuja kuifuta Chadema ukitaka kujua angalia pro-Chadema wanavyoweweseka.
 
Back
Top Bottom