ACT yakataliwa Mbeya

ACT yakataliwa Mbeya

daniel merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
277
Reaction score
98
CHAMA cha siasa cha ACT-Tanzania kimeingia kwenye anga za CHADEMA Mbeya na kujikuta kikipoteza kadi zaidi ya 100 kilichowashawishi wanachama wa CHADEMA ambao baada ya kuzipokea, zilitupwa usiku nje ya ofisi hizo.

Kadi za ACT, zilipatikana jana majira ya asubuhi na kusababisha uongozi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, ukutane haraka katika ofisi hizo na kuzionyesha hadharani.

Kiongozi wa ulinzi na usalama wa CHADEMA Mbeya Mjini, Jamal Juma, alisema kuwa kadi, bendera na vipeperushi hivyo, vilikutwa nje ya ofisi hizo na alijulishwa haraka na wasaidizi wake kuwa wameokota nyaraka za ACT zilizosalimishwa CHADEMA.

"Bado tunachunguza nani aliyezileta ofisini kwetu, leo ni Jumapili tumekutana ili kulifanyia kazi jambo hili, tukio hili ni neema kwa CHADEMA, watu wenye nia njema wanaonyesha wanavyokipenda chama, wameidharau sana ACT, waliopewa na kuzitupa tunawapongeza mno," alisema Juma.

Kada mwingine wa CHADEMA, Thobias Sebastian, alisema kuwa habari za ndani ambazo chama hicho kimezipata jana, zinadai kuwa kadi hizo, bendera na vipeperushi zilitolewa kwenye ofisi za ACT zilizopo Uyole, ndipo waliyopewa wakazitelekeza CHADEMA.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, John Mwambigija, alipokea kadi, bendera na vipeperushi vya ACT na kuwapongeza wanachama wa chama hicho walioshawishiwa kukisaliti na kuukana usaliti huo.

"Hali hii imetutia moyo sana, ACT wamekwama watafute wanachama wengi kutoka CCM, huko wanaweza kuvuna sio CHADEMA, kwa kuwa huko tunavuna maelfu kila siku, wasihangaike na CHADEMA hawawezi kuibomoa kirahisi," alisema Mwambigija.

Hii ni mara ya kwanza katika jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na CHADEMA, kuokota idadi kubwa ya kadi za chama cha siasa cha upinzani zilizotupwa baada ya kutolewa.

Tanzania Daima ilifuatilia Uyole ili kuwafahamu viongozi wa ACT waliyogawa kadi, bendera na vipeperushi kutoka kwenye ofisi zao, lakini hakuwepo kiongozi yeyote, zaidi bendera ikipepea tu.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Danganya toto! CDM mliweka mpango wa kuzikusanya ili muibuke na agenda hiyo. ACT - Tanzania mkoani mbeya haichukiwi kwa level na picha unayotaka kutujengea humu jf.

Kila shetani ana mbuyu wake.
 
“Bado tunachunguza nani aliyezileta ofisini kwetu, leo ni Jumapili tumekutana ili kulifanyia kazi jambo hili, tukio hili ni neema kwa CHADEMA, watu wenye nia njema wanaonyesha wanavyokipenda chama, wameidharau sana ACT, waliopewa na kuzitupa tunawapongeza mno,” alisema Juma.

Kada mwingine wa CHADEMA, Thobias Sebastian, alisema kuwa habari za ndani ambazo chama hicho kimezipata jana, zinadai kuwa kadi hizo, bendera na vipeperushi zilitolewa kwenye ofisi za ACT zilizopo Uyole, ndipo waliyopewa wakazitelekeza CHADEMA.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, John Mwambigija, alipokea kadi, bendera na vipeperushi vya ACT na kuwapongeza wanachama wa chama hicho walioshawishiwa kukisaliti na kuukana usaliti huo.

“Hali hii imetutia moyo sana, ACT wamekwama watafute wanachama wengi kutoka CCM, huko wanaweza kuvuna sio CHADEMA, kwa kuwa huko tunavuna maelfu kila siku, wasihangaike na CHADEMA hawawezi kuibomoa kirahisi,” alisema Mwambigija.

Hii ni mara ya kwanza katika jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na CHADEMA, kuokota idadi kubwa ya kadi za chama cha siasa cha upinzani zilizotupwa baada ya kutolewa.

Tanzania Daima ilifuatilia Uyole ili kuwafahamu viongozi wa ACT waliyogawa kadi, bendera na vipeperushi kutoka kwenye ofisi zao, lakini hakuwepo kiongozi yeyote, zaidi bendera ikipepea tu.
 
Act wanajijenga tu kwenye majimbo ya cdm, zzt siasa zimekushinda kabisa
 
Chama chochote cha siasa huwa hakianzishwi kwa style hii, wakuu kama kuna chama cha siasa kilianziswa namna hii na kinadunda naombeni mnitajie.

Kama hakipo basi na ACT haipo sababu haitakuwepo.
 
hili gazeti la mboye bwana, linajaribu kutengeneza mambo ili ugali usimwagike
 
CHAMA cha siasa cha ACT-Tanzania kimeingia kwenye anga za CHADEMA Mbeya na kujikuta kikipoteza kadi zaidi ya 100 kilichowashawishi wanachama wa CHADEMA ambao baada ya kuzipokea, zilitupwa usiku nje ya ofisi hizo.

Kadi za ACT, zilipatikana jana majira ya asubuhi na kusababisha uongozi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, ukutane haraka katika ofisi hizo na kuzionyesha hadharani.

Kiongozi wa ulinzi na usalama wa CHADEMA Mbeya Mjini, Jamal Juma, alisema kuwa kadi, bendera na vipeperushi hivyo, vilikutwa nje ya ofisi hizo na alijulishwa haraka na wasaidizi wake kuwa wameokota nyaraka za ACT zilizosalimishwa CHADEMA.

"Bado tunachunguza nani aliyezileta ofisini kwetu, leo ni Jumapili tumekutana ili kulifanyia kazi jambo hili, tukio hili ni neema kwa CHADEMA, watu wenye nia njema wanaonyesha wanavyokipenda chama, wameidharau sana ACT, waliopewa na kuzitupa tunawapongeza mno," alisema Juma.

Kada mwingine wa CHADEMA, Thobias Sebastian, alisema kuwa habari za ndani ambazo chama hicho kimezipata jana, zinadai kuwa kadi hizo, bendera na vipeperushi zilitolewa kwenye ofisi za ACT zilizopo Uyole, ndipo waliyopewa wakazitelekeza CHADEMA.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, John Mwambigija, alipokea kadi, bendera na vipeperushi vya ACT na kuwapongeza wanachama wa chama hicho walioshawishiwa kukisaliti na kuukana usaliti huo.

"Hali hii imetutia moyo sana, ACT wamekwama watafute wanachama wengi kutoka CCM, huko wanaweza kuvuna sio CHADEMA, kwa kuwa huko tunavuna maelfu kila siku, wasihangaike na CHADEMA hawawezi kuibomoa kirahisi," alisema Mwambigija.

Hii ni mara ya kwanza katika jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na CHADEMA, kuokota idadi kubwa ya kadi za chama cha siasa cha upinzani zilizotupwa baada ya kutolewa.

Tanzania Daima ilifuatilia Uyole ili kuwafahamu viongozi wa ACT waliyogawa kadi, bendera na vipeperushi kutoka kwenye ofisi zao, lakini hakuwepo kiongozi yeyote, zaidi bendera ikipepea tu.

Chanzo: Tanzania Daima

Kwakua Lengo lake ni Ovu basi hakitapata nafasi kwa Chama cha Mpango wa Mungu Chadema
 
ACT wanahangaika bure,hawa wanachama wa chadema ni wale waliokuwa NCCR MAGEUZI kisha wakamfuata Mrema TLP walipoona Mrema ni hohe hahe na amerudi ccm walikataa kwenda ccm na kuamua kwenda chadema so hawatatoka chadema.
 
cha cha misikitini wapi na wapi kule mbeya mwandiga wamekikataa itakuwa nyanda za juu kusini ha ha
 
Nao ni wajinga,utaendaje sehemu ambayo tayari mwasisi na mwenyekiti mtarajiwa alishazikwa rasmi??
Walikurupuka.
 
Unajua Prof. Paramagamba alisema ni afadhali ukaduwaa kuliko ukashupaa. Ushupavu huu unakusaidia nini? Unaweza kutuambia walizikusanya kutoka wapi? Kama ni hivyo ACT haina dira. Mwenye akili huwezi kuprint cadi halafu ukazitupa ili CDM wazikusanye.

Tafiti kabla hujajidhalilisha.

Back
Top Bottom