GE2025 ACT Wazalendo yasisitiza Mpina ni mgombea urais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,600
Wakati Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikisisitiza kuwa kuwa Luhaga Mpina sio mgombea urais wa.Jamhuri ya Muungano kwa kuwa alienguliwa, chama cha ACT Wazalendo kimesema bado Mpina ni mgombea wao mpaka kesi mbili zilizofunguliwa ziamuliwe.

Mpina alienguliwa Septemba 15, 2025 baada ya INEC kukubali pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari kati ya mapingamizi matatu.

Hata hivyo, Mpina amefungua kesi mbili kupinga kuenguliwa kwake iliyoanza kusikilizwa leo Septemba 22 katika Mahakama Kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam.

Akizungumza leo Septemba 22 katika uzinduzi wa ilani ya ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema Mpina bado mgombea wao wa urais atakayeinadi ilani hiyo.

"Ilani hii ina wanadi wake. Japo tuna wapiga kura, tunao wagombea ambao ni madiwani wote, wengine ninwabunge wetu.
"Kundi la tatu ni wagombea wetu wa urais wa Jamhuri ya Muungano. Sisi ACT kwenye mkutabo tulimchagua mgombea wetu Luhaga Mpina na mgombea umakamu ni bibi Fatma Fereji.

Amesema kupitia kauli mbiu yao ya "It's not done until it's done" ambayo alisema wengine hawaipendi, bado wanaye mgombea urais.

"Sisi tunaye mgombea wetu, kwa sababu kesi inaendelea mahakamani.

"Luhaga Mpina anaendelea na kesi, kwa sababu tumefungua kesi mbili, kwanza kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Kesi ya pili Msajili wa vyama vya siasa," alisema Ado.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha uzinduzi huo wa ilani, Naibu Katibu Mkuu Uenezi na Uhusiano wa ACT wazalendo, Shangwe Ayo amesema, hawaiogopi barua waliyotumiwa bali wanaendelea mbele.
"Niseme nisiseme? Tumeamka na barua, lakini tunasonga mbele, maana walidhani tunaogopa barua," alisema.
Amesema katika mkutano wa hadhara unaofanyika Vingunguti, viongozi wote wa chama watakuwepo akiwamo aliyemtaja kuwa ni mwanachama wao.

Pia Soma: GE2025 - Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yasisitiza kuwa Act- Wazalendo hawana mgombea Urais
 
Upuuzi mtupu..
 
Back
Top Bottom