ACT-Wazalendo yashinda Lyabusinde Kigoma

ACT-Wazalendo yashinda Lyabusinde Kigoma

karama kaila

Senior Member
Joined
Jan 30, 2015
Posts
122
Reaction score
60
Leo ni furaha na nderemo katika kijiji cha Lyabusinde ni ushindi mkubwa kwa wanyonge dhidi ya mafisadi.

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa Chama cha ACT-wazalendo leo kimeibuka na ushindi mkubwa dhidi ya kupinga mfumo unaomfanya Mtanzania kuwa masikini.

Baada ya ACT-Wazalendo kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Lyabusinde Mkoni Kigoma CCM wakakimbilia mahakamani na leo Hakimu kamaliza kesi kwa kuipa ACT-wazalendo haki yake waliyopewa na wanakijiji wa Lyabusinde katika boksi la kura.

Huu ni muendelezo wa ushindi wa wanyonge.
More to come.
 
kumbe hata act wakishinda ccm hukimbilia mahakamani
 
Mmmh.... Wasaliti mpo kazini...

Yaani act na ccm mnawalaghai watanzania kwa kujifanya mmeshitakiwa kumbe maigizo..... Baba na mwana?
 
Hakuna anaeweza kuwaingilia,ACT iko nyumbani kwake.
 
Hii imekaaje,Ccm kuipeleka ACT mahakamani tena!!.Ndo kusema hata baada ya matokeo ya uchaguzi wa oct.2015 Chadema inaweza kuipeleka C.U.F, NCCR au NLD mahakamani?.Mimi nijuavyo,ushindi wa ACT ni ushindi wa CCM.Period!
 
Sasa ccm na act kunatofaut gani? Tuweni wawaz tu jamani mnamdanganyaga nan sasa? Watanzania waleo sio waleeee
 
kakijiji kamoja hakawezi kuinyima ccm usingizi

Ukizingatia kuwa kilichofanyika ni sawa na kubadilisha mfuko wa kuweka fedha,kuzitoa mfuko wa kulia na kuziweka mfuko wa kushoto,wakati yote ni mifuko ileile.
 
Kwahiyo chadema wameamua kuwashitaki ACT kwa malengo gani sasa.
 
kakijiji kamoja hakawezi kuinyima ccm usingizi
Umenikumbusha mkuu. Wakati Masumbuko lamwai aliposhinda udiwani kata ya manzese dsm Kingunge NM alisema kata moja haiwezi kuinyima ccm usingizi. Kesho yake gazeti moja likaandika kichwa cha habari kikuuuubwa.
CCM KUENDELEA KUUCHAPA USINGIZI: KINGUNGE.
Mzee akaitwa kujieleza akasema alinukuliwa vibaya. Na wewe mkuu angalia usije ukanukuliwa vibaya!
 
Hahahaha
 
Back
Top Bottom