PreGE2025 ACT Wazalendo yaitaka serikali kuwachukulia hatua Wasira na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa CCM-Zanzibar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,777
Chama cha ACT Wazalendo kimeiomba Serikali kuwachukulia hatua viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti Bara, Stephen Wasira, na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa CCM-Zanzibar, Hamis Mbeto, kwa kupotosha umma kuhusu tukio lililotokea nchini Angola.

Wito huo umetolewa leo, Jumapili, Machi 16, 2025, na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Taifa, alipozungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, jijini Dar es Salaam.

“Niseme wito wangu kwamba hasa kwa haya ambayo yamepotoshwa na watu ambao ni waandamizi wa Chama cha Mapinduzi, naiomba sana Serikali na natoa wito serikalini kama Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo kwamba Serikali iwachukulie hatua viongozi hao, kwa sababu upotoshaji wao umeipaka matope Serikali. Upotoshaji wao umewafadhaisha wananchi kwa kiasi kikubwa, wamefanya vitu kwa namna ambayo haiendani na nafasi zao, huo ndiyo wito wetu kama ACT,” amesema Othman.

Machi 14, akizungumza Tunduma mkoani Songwe, Wassira alisema: "Leo nimesoma viongozi walikuwa wanaenda Angola lakini wamenyang'anywa paspoti huko ni Angola sio hapa, hapa hatuja wanyang'anya paspoti na hata ikimaliza muda wake tunawapa, ili waende wanakotaka alafu warudi salama.

“Wamelalamika kwa nini Serikali imekaa kimya kwani sisi tunasimamia Airpoti ya Angola? Airpoti ya Angola inasimamiwa na watu wa Angola, na pia huenda walikuwa na jambo lao ambalo wanalilitilia shaka wangeuawa tungesema kwa nini wamewaonea watu wasiokuwa na hatia," amesema Wassira.

Viongozi wa ACT Wazalendo walizuiwa kuingia nchini Angola kushiriki katika mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD), yaliandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation.

WhatsApp Image 2025-03-16 at 16.59.44_e4d138a7.jpg

WhatsApp Image 2025-03-16 at 16.59.47_c78b0252.jpg
 
Kuna kitu kimoja muhimu sana hakisemwi na wajumbe waliopata kadhia ya kuzuiliwa kuingia Angola.
Sijasikia popote mtu akitaja kuzuiliwa pamoja na kuwa na visa ya kuingilia Angola.
Hebu jitokezeni wajumbe muweke bayana hapa kama mlifuata taratibu zote za safari ikiwemo kufika ubalozi wa Angola hapa nchini kuwataarifu mwaliko wenu wa kwenda Angola na kama waliwapa idhini ya kuendelea na safari.🙄
 
Chama cha ACT Wazalendo kimeiomba Serikali kuwachukulia hatua viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti Bara, Stephen Wasira, na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa CCM-Zanzibar, Hamis Mbeto, kwa kupotosha umma kuhusu tukio lililotokea nchini Angola.
Wito huo umetolewa leo, Jumapili, Machi 16, 2025, na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Taifa, alipozungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, jijini Dar es Salaam.

“Niseme wito wangu kwamba hasa kwa haya ambayo yamepotoshwa na watu ambao ni waandamizi wa Chama cha Mapinduzi, naiomba sana Serikali na natoa wito serikalini kama Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo kwamba Serikali iwachukulie hatua viongozi hao, kwa sababu upotoshaji wao umeipaka matope Serikali. Upotoshaji wao umewafadhaisha wananchi kwa kiasi kikubwa, wamefanya vitu kwa namna ambayo haiendani na nafasi zao, huo ndiyo wito wetu kama ACT,” amesema Othman.

Machi 14, akizungumza Tunduma mkoani Songwe, Wassira alisema: "Leo nimesoma viongozi walikuwa wanaenda Angola lakini wamenyang'anywa paspoti huko ni Angola sio hapa, hapa hatuja wanyang'anya paspoti na hata ikimaliza muda wake tunawapa, ili waende wanakotaka alafu warudi salama.

“Wamelalamika kwa nini Serikali imekaa kimya kwani sisi tunasimamia Airpoti ya Angola? Airpoti ya Angola inasimamiwa na watu wa Angola, na pia huenda walikuwa na jambo lao ambalo wanalilitilia shaka wangeuawa tungesema kwa nini wamewaonea watu wasiokuwa na hatia," amesema Wassira.

Viongozi wa ACT Wazalendo walizuiwa kuingia nchini Angola kushiriki katika mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD), yaliandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation.

yaani mkamatwe nyie kwa kuvamia na kuingia nchi ya kigeni bila kufuata utaratibu kama vibaka na hatimae kua deported makwenu, halafu mnatoa wito wasiohusika na uvamizi wenu ughaibuni wachukuliwe hatua?

chama cha siasa kufikia hatua ya kuchanganyikiwa kama hii ni kitu mbaya sana aise 🤣

Mlidhani mnaenda kariakoo kununua maembe?
 
Back
Top Bottom