Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,285
Ni kweli ambaye anatakiwa kuongea ni Yule mabaya hajawahi kupata cheti cha Shule , Maana baadhi yetu akili zetu ndivyo zilivyoRaisi huyu huyu alosema raisi wa kuwait ni Sadam Hussein, hasara tupu..akae kimya tu
ACT wanahangaika na mambo yaliyowazidi kimo na ambayo huenda hawayaelewi kiundani.
Sijasikia Taifa lolote likilaani. Hata USA ambaye ni mshirika mkuu wa Qatar hajalaani! Badala yake ameomba kuwe na mazungumzo lakini pia Trump ameiambia Qatar iache kuyasaidia makundi ya kigaidi. Kauli ile ya Trump inaonesha kuwa kuna ukweli wa namna fulani kwa Qatar kuyasaidia makundi ya kigaidi.
ACT wana uhakika kuwa hizo nchi za kiarabu hawajaongea na Qatar kabla ya kuufikia uamuzi wa sasa? Kama ni kweli Qatar wanasaidia makundi ya kigaidi, ni halali kuchukua hatua dhidi yao. Tunapowaonea huruma Qatar, tuwakumbuke wale wanaopoteza maisha kutokana na ugaidi.
Jambo la muhimu ni kuwa na uhakika kama kweli Qatar inayasaidia makundi ya kigaidi. Qatar inayasaidia hayo makundi kama nchi/state au kuna raia wake wanaofanya hivyo?