ACT Wazalendo yaitaka serikali ilaani vikwazo vya kinyama dhidi ya nchi ya Qatar

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Screenshot_2017-06-24-11-48-51.png
Screenshot_2017-06-24-11-59-30.png
 
yaani raisi wetu ndo alaani hivyo vikwazo,nahisi kwanza hajui hata kinachoendelea
 
Raisi huyu huyu alosema raisi wa kuwait ni Sadam Hussein, hasara tupu..akae kimya tu
 
Ni kweli ambaye anatakiwa kuongea ni Yule mabaya hajawahi kupata cheti cha Shule , Maana baadhi yetu akili zetu ndivyo zilivyo
 
ACT wanahangaika na mambo yaliyowazidi kimo na ambayo huenda hawayaelewi kiundani.

Sijasikia Taifa lolote likilaani. Hata USA ambaye ni mshirika mkuu wa Qatar hajalaani! Badala yake ameomba kuwe na mazungumzo lakini pia Trump ameiambia Qatar iache kuyasaidia makundi ya kigaidi. Kauli ile ya Trump inaonesha kuwa kuna ukweli wa namna fulani kwa Qatar kuyasaidia makundi ya kigaidi.

ACT wana uhakika kuwa hizo nchi za kiarabu hawajaongea na Qatar kabla ya kuufikia uamuzi wa sasa? Kama ni kweli Qatar wanasaidia makundi ya kigaidi, ni halali kuchukua hatua dhidi yao. Tunapowaonea huruma Qatar, tuwakumbuke wale wanaopoteza maisha kutokana na ugaidi.

Jambo la muhimu ni kuwa na uhakika kama kweli Qatar inayasaidia makundi ya kigaidi. Qatar inayasaidia hayo makundi kama nchi/state au kuna raia wake wanaofanya hivyo?
 
Hawa Qatar wanapewa jeuri na Iran. Iran na Saudi Arabia haziivi kihivyo. Ila nimegundua kitu ACT na Iran wanamfumo wa kiungozi wenye cheo cha kiongozi mkuu. Sasa unganisha nukta nundu mwenyewe.

Na washawasha!
 
ACT wanahangaika na mambo yaliyowazidi kimo na ambayo huenda hawayaelewi kiundani.

Sijasikia Taifa lolote likilaani. Hata USA ambaye ni mshirika mkuu wa Qatar hajalaani! Badala yake ameomba kuwe na mazungumzo lakini pia Trump ameiambia Qatar iache kuyasaidia makundi ya kigaidi. Kauli ile ya Trump inaonesha kuwa kuna ukweli wa namna fulani kwa Qatar kuyasaidia makundi ya kigaidi.

ACT wana uhakika kuwa hizo nchi za kiarabu hawajaongea na Qatar kabla ya kuufikia uamuzi wa sasa? Kama ni kweli Qatar wanasaidia makundi ya kigaidi, ni halali kuchukua hatua dhidi yao. Tunapowaonea huruma Qatar, tuwakumbuke wale wanaopoteza maisha kutokana na ugaidi.

Jambo la muhimu ni kuwa na uhakika kama kweli Qatar inayasaidia makundi ya kigaidi. Qatar inayasaidia hayo makundi kama nchi/state au kuna raia wake wanaofanya hivyo?

Mkuu huo ndiyo msimamo wao, usiwalazimishe wafanane na wengine!
 
kwahiyo ACT haiwezi kulaani ikatosha mpaka serikali ifanye hivyo?
 
Back
Top Bottom