ACT wazalendo waipa pigo zito CCM mjini Dodoma!

ACT wazalendo waipa pigo zito CCM mjini Dodoma!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803



​
Zaidi ya wanachama 100 kutoka CCM, Kata ya Chihanga, Manispaa ya Dodoma wamejiunga na ACT- Wazalendo.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao, Ally Amanzi aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM katika kata hiyo, alisema jana kuwa wamelazimika kuhama kutokana na kufilisika kisiasa.Amanzi alisema viongozi wa vyama hawaonyeshi kama wanaweza kuleta mabadiliko, badala yake wanafikiria watakavyojilimbikizia mali."ACT–Wazalendo tunaimani nayo sisi wakazi wa Kata ya Chihanga, lazima tutapata mabadiliko ya kweli tofauti na vyama vingine vinavyojitokeza kuomba viongozi wao tuwachague," alisema Amanzi.


Alisema katika chama hicho kuna ubabaishaji mwingi, hali inayochangia wananchi wasipate maendeleo.Walence Lusingu ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Mkoa wa Dodoma, alisema ACT kimedhamiria kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wa kata hiyo.

Lusingu ambaye ni mgombea udiwani katika Kata ya Miyuji, aliwataka wakazi wa kata hiyo kutofanya makosa ya kuchagua viongozi wa vyama vya siasa ambavyo vitawageuza kuwa mitaji pindi vitakapochaguliwa kushika madaraka.

Alisema katika kipindi hiki cha kampeni, lazima wawe makini katika kusikiliza sera zinazotolewa na wagombea hao, kutokana na wengi wamekuwa wakijinadi kwa kutoa maneno matamu huku wakiwa siyo wakweli.Mgombea udiwani wa

Kata ya Chihanga ambaye alikuwa diwani kupitia CCM kabla ya kuhamia ACT- Wazalendo, Julia Mputu amewaomba wananchi wa kata hiyo, kumpa ridhaa tena ya kumrudisha madarakani ili amalize miradi iliyobaki wakati wa kipindi chake.


Mputu alisema katika kipindi chake cha udiwani, mahitaji ambayo walikuwa wamemtuma mengi ameyafanikisha na machache hajakamilisha.Aliyataja baadhi ya mambo aliyofanikisha kuwa ni barabara, afya, elimu pamoja na suala ya kilimo.Hata hivyo, alisema miradi iliyobaki ataikamilisha watakapomchagua katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao."Nawaomba mnirudishe nije tumalizie miradi iliyobaki ukizingatia kuwa kazi yangu niliyoifanya kwa kushirikiana na ninyi mmeiona kwa vitendo. Hakukuwa na ubabaishaji wowote," alisisitiza.


:

​










 
Kachama kamejitahidi, vipi dp ya mtikira ,udp ya cheyo, updp na tppt ya dotuva hivi vyama vyemye p vinamikosi havina watu, tlp, udp, ppt maendeleo vyote hali mbaya
 
Act - watu unao waona wanakuja kwenye mikutano ya Act, ni wanaccm wanakuja kwa mdogo wake ccm yaani Act wazalendo.
 
Hata akijiunga jakaya hatushangai ni mtoto wao! vijisenti wanavyo wagaramia ccm vitawatoka puani october 25
 
Kuanzia sasa tutakuwa tunasikia wanachama kutoka ccm kwenda act hii sasa ndo single mpya, eti hapo wanahisi watu watawaamini kuwa ni wapinzani wa kweli. Tulishawastukia hilo wala alisaidii tulia tuwanyooshe na ccm yenu.
 
ACT mwendo mdundo! Wanasema ni "kachama", wakati hivyo vyama vyao havina sera!
 
act-wazalendo nimewakubali kweli kweli yaan nyinyi ndiyo wapinzan wa kweli kwa ccm kazen buti. mnao sema mtoto wa ccm mnakosea saaana. kwan mtoto wa ccm ni CHADEMA kwa sababu hata mgombea wenu urais ni wa ccm pure. mgombea wenu ana miaka 62, hii ni robotatu ya maisha yake yana damu ya ccm na robo iliyo baki yuko cdm hapo unategemea nn? sis wenye uwezo mkubwa wa kufikiri tutakuambia ccm=cdm. atakayebisha aje hapa. ACT-WAZALENDO JUUUUUuuuuuuuuu.
 
Asingekuwepo Zitto hapo huo mkutano ingekuwa na watu wasiozidi kumi.ACT ni chama cha mtu mmoja!
 
shida ya ukawa ni kuona kibanzi kilichopo act lakin wao hawaon boliti lililopo ukawa.
 
act-wazalendo nimewakubali kweli kweli yaan nyinyi ndiyo wapinzan wa kweli kwa ccm kazen buti. mnao sema mtoto wa ccm mnakosea saaana. kwan mtoto wa ccm ni CHADEMA kwa sababu hata mgombea wenu urais ni wa ccm pure. mgombea wenu ana miaka 62, hii ni robotatu ya maisha yake yana damu ya ccm na robo iliyo baki yuko cdm hapo unategemea nn? sis wenye uwezo mkubwa wa kufikiri tutakuambia ccm=cdm. atakayebisha aje hapa. ACT-WAZALENDO JUUUUUuuuuuuuuu.

Kama cdm=ccm, basi ichague cdm utakuwa hujapoteza kura yako.
 
Back
Top Bottom