Wananchi wamewapuuza ccm na uchaguzi kwa ujumla. Kundi kubwa la wananchi haliridhishwi na ccm tena, kwa ujumla ccm iko nje ya muda bila wao kujua. Ukitaka kujua ccm imechokwa usiangalie ushindi, bali angalia idadi ya wapiga kura. Kama idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni zaidi ya laki 3 sehemu zote kilipokuwa na uchaguzi leo, kisha wanatokea watu chini ya 50,000 hapo inabidi mjiulize. Ccm kwa sasa ni kama mwanafunzi anayepata division IV toka division I, lakini anajivunia kuwa wakwanza kwenye hiyo division IV! Kama mna akili na mnaamini mnakubalika, jiulize ni kwanini hamna wapiga kura kama zamani? Hebu weka idadi ya wapiga kura iliyojitokeza tujue inavyokubalika na sio kutangazwa washindi na tume yenu.