KYAMTUNDU
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 1,820
- 295
Wasalaamu ndugu zangu.
Baada ya tafakuri ya muda nimeona niongee kidogo juu ya madai ya Kiongozi Mkuu (KM) wa ACT Wazalendo kwamba " ACT haipo kwa ajili ya kugawana kura MILIONI NANE za waliojitokeza kupiga kura mwaka 2010, bali wanazitafuta kura milioni 12 za wale WALIOACHA KUPIGA KURA kwa KUCHOSHWA na vyama vilivyokuwepo mwaka huo".
Nianze kwa kuonesha uchache wa fikra katika kauli hii. Kusema ACT hawatagawa kura ni kupotoka kwa sababu wanachama wao wanaohamahama kutoka vyama mbalimbali walipigia kura vyama hivyo mwaka 2010 akiwemo Kiongozi Mkuu labda naye aseme hakupiga kura kwa kuchoshwa na vyama hivyo!
Pamoja na kwamba KM hunukuu "utafiti" wa REDET kwamba wasiopiga kura walichoshwa na vyama vilivyopo, nina uhakika nukuu hiyo ina matege na kama ni utafiti ulihitimisha namna hiyo, basi watafiti wenyewe hawakujitendea haki. Kutokupiga kura hutokana na sababu kadhaa:
1. Baadhi ya waliojiandikisha kupiga kura kuaga dunia. ACT hawajasema kati ya wale 12 milioni ni wangapi waliokosa fursa kwa sababu ya kufikwa na umauti-labda watwambie ni SUFURI. Na kama wapo ni mbinu gani wataitumia kuwafufua wafu ili waipigie kura ACT?
2. Baadhi ya waliojiandikisha kupiga kura kuhama eneo la uandikishaji. Sheria za Uchaguzi zinataka mpiga kura kuwa amejiandikisha kwenye eneo analokwenda kupigia kura. ACT hawajatwambia kati ya watu milioni 12 ni wangapi walihama eneo na kukosa fursa hiyo-AU ni SUFURI?! Na kama wapo, watawezaje kuwarejesha kwenye maeneo yao siku ya uchaguzi!
3. Baadhi ya waliojiandikisha kupiga kura hupoteza shahada. ACT hawajasema kama wameziokota shahada zao au nI SUFURI. Na kama wapo, ni namna gani ACT wataibadili sheria ya uchaguzi ili aliyepoteza shahada apige kura.
4. Baadhi ya waliojiandikisha kupiga kura hukosa majina yao kwenye daftari la kudumu lakini yapo kwenye ubao wa matangazo. ACT hawajasema watafantaje kuhakikisha majina hayo hayakosekani ili wapiga kura 12 milioni wasipungue labda iwe SUFURI!
5. Baadhi ya waliojiandikisha kupiga kura hukuta majina yao yamekosewa kwenye daftari la kudumu hata kama picha zinafanana. Mfano Samson Mwigamba aweza kukutwa ameandikwa "SAMSONI MUIGAMBA" na kukataliwa kupiga kura kwa sababu hiyo! ACT hawasemi ni namna gani watahakikisha majina hayakosewi ili wapiga kura milioni 12 wawape kura zote.
6. Baadhi ya waliojiandikisha kupiga kura huacha kupiga kwa sababu husema "HATA UKIMCHAGUA NANI NI WALEWALE TU"! ACT hawajasema ni namna gani wataiondoa dhana hii miongoni mwa watoro. Kwa lugha rahisi, hata walioacha kumchagua KM mwaka 2005 na 2010 ni kwa sababuu walimuona ni walewale tu ndiyo maana kwa miaka kumi ametoa AMBULANCE wakati anamalizia uongozi wake. Ni namna gani ACT itakabiliana na watoro hawa wakati KM yumo ndani ya 'WALEWALE"?!