DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Leo tarehe 30 Disemba, 2025 Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu Dodoma ikiketi chini ya Jaji Ephery Kisanya imetoa uamuzi wa muhimu katika kesi dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuhusu Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalumu iliyofunguliwa na ACT Wazalendo. Katika uamuzi huo mdogo, Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi la Serikali na kuagiza kesi iendelee katika hatua ya kesi ya msingi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia maombi ya kimahakama (Application for Leave) yaliyowasilishwa na ACT Wazalendo tarehe 19 Novemba, 2025 kupitia shauri la Mahakama Kuu namba 28632 la mwaka 2025 kuomba kibali cha Mahakama Kuu kufungua kesi ya msingi ya kupinga Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalumu uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 7 Novemba, 2025 uteuzi ambao ulionekana kukiuka Katiba na kukosa misingi ya haki.
Awali, katika hatua ya shauri la Maombi ya Kibali cha kufungua kesi ya msingi, Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu iliweka mapingamizi ikidai kuwa Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi inayoombwa kufunguliwa na ACT Wazalendo. Mahakama katika uamuzi wake uliotolewa leo imeona kuwa mapingamizi hayo hayana msingi na imeyatupilia mbali na imetoa ruhusa kwa kesi ya msingi kufunguliwa na kusikilizwa.
Katika madai yetu, ACT Wazalendo tunapinga utaratibu uliotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalumu kwani kwa maoni yetu tunaona kuwa Tume imevunja vifungu vya Katiba na Sheria ya Uchaguzi. Vilevile, tunataka Tume ya Uchaguzi ikaeleze Mahakama ilitumia utaratibu gani kupata idadi ya Viti Maalumu vya Ubunge ilivyovitoa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliopata viti 113 na CHAUMMA waliopata viti 2 ilhali fomula ya idadi ya viti kwa kila chama kinachostahiki inayopatikana chini ya sharti la Ibara ya 78(1) ni viti visivyopungua 6.
Aidha, tunakusudia kuomba Mahakama iitake Tume kueleza ni matokeo yapi ya Uchaguzi wa Ubunge waliyotumia kukokotoa idadi ya Viti vilivyostahiki kwa kila chama kilichoshiriki Uchaguzi kwani kwa mujibu wa Matokeo tuliyokusanya, ACT Wazalendo tuna kura 2,222,162 ambazo ni sawa na 6.77% ya kura za Ubunge.
Baada ya uamuzi huu wa Mahakama, sasa kesi ya msingi kwa ajili ya kuhoji masuala hayo na mengineyo iko wazi kufunguliwa. Tayari Mawakili wa Chama wamekamilisha hatua zote za kufunguliwa kwa kesi hiyo.
Pia Soma: Sakata la wabunge wa viti maalumu, ACT Wazalendo yatinga mahakamani