ACT-Wazalendo kushiriki SUK: Maoni ya Tundu Lissu

Mtu anayeandika hivi ndio alitaka kuwa Rais wa Tanzania! Ndio maana Tundu Lissu anapuuzwa na kila mtu anayejielewa.
Lissu alikuwa anafanya vizuri sana alipokuwa mwanaharakati, lakini baada ya kuingia kwenye siasa akayeyuka. Yeye alishindwa kutofautisha siasa na uanaharakati.
 
Kwa maoni yangu, ACT wame-surrender kwa Magufuli na maCCM. Hakuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoamuliwa na Wazanzibari wenyewe; bali ile inayoruhusiwa na Watanganyika, yaani Magufuli na maCCM ya Tanganyika.

Sisi Watanganyika ndio waamuzi wa kitu gani kifanyike Zanzibar, sio Hussein Mwinyi na Maalim Seif. Sisi Watanganyika ndio tunaotaka muafaka ambao utamtuliza Maalim Seif na kuituliza dunia ili isituwekee vikwazo vya kiuchumi kwa sababu ya dhulma zetu dhidi ya Wazanzibari.

Tumemtupia Maalim Seif mfupa mtupu (Makamu wa Kwanza wa Rais hana mamlaka yoyote ya maana kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar!) ili atulie na awatulize Wazanzibari wanaomuunga mkono na jumuiya ya kimataifa iliyochukizwa na dhulma zetu Zanzibar na Tanganyika.

Maalim Seif atalipwa mshahara na marupurupu mengine na kupigiwa saluti na mapolisi waliokuwa wanaua watu wake juzi. Zaidi ya hapo hatakuwa na chochote.

Serikali hii ya sasa ni tofauti na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Amani Karume na Maalim Seif. Ya mwanzo ilileta mabadiliko makubwa ya Katiba ya Zanzibar; kwa sababu Karume alikuwa anaunga mkono jitihada za Wazanzibari za kujivua kwenye ‘koti linalobana’ la Muungano.

Hussein Mwinyi ni kibaraka wetu moja kwa moja; tumemweka madarakani kwa bunduki na vifaru vya Bara na kura za Watanganyika waliopelekwa kupiga kura Zanzibar wakati Wazanzibari halali wanakataliwa kupiga kura.

Kibaraka wetu huyu hajampa Maalim Seif na ACT yake chochote zaidi ya vyeo visivyokuwa na mamlaka yoyote. Sasa Maalim Seif atatumika kujaribu kuhalalisha uharamia wa October 28. Atatumika kama toilet paper ya kusafishia uchafu wa maCCM na madhambi yao dhidi ya Wazanzibari.

Mimi naamini hatafanikiwa. Masikitiko yangu ni kwamba amekubali kutumika namna hii katika uzee wake. Baada ya miaka karibu arobaini ya kusimamia maslahi ya Wazanzibari, sasa amekubali kutumikia maslahi ya Tanganyika!
Pumba tupu
 
Kwa UFINYU wa akili yako. Umeshamsikia kiongozi gani wa Chadema kampongeza huyo mchumia tumbo na msaliti kwa kurushiwa fupa na maccm? Umeshawahi kumsikia kiongozi gani wa Chadema anatoa kauli kama hizi kisha hata alichoomba kifanyike hakijafanyika akaungana na hao dhalimu aliowashtaki? 😳😳

Ya nn uwe karibu na mnafiki?

Ndege wanafananao huruka pamoja.
 
Tumekuwa na ushabiki tu. Lakini aliyoyazungumza tundu lissu yana ukweli sana someni aliyoyasema mara tatu ili muielewe hii sio simba na yanga
 
Katika dini yetu ya kiislamu huwa tunaomba mtu mwisho wake uwe mwema yaani mauti yamkute kaacha pombe kaacha umalaya umauti una mkuta akiwa kwenye ibada ndio mwisho mwema. Maalim seif alianza na mema anaishia mwisho mbaya
 
Je babu kwa umakini wako na ujasiri wako hivi kweli wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani hawajui kuandika na kujaza fomu ccm wote wanajua wao hawajakosea. babu kweli hili unasemaje
 
Wapemba hata akiwa rafiki yako wa dammu usimwamini huwa wanabadilika na hasa kama wewe sio mpemba mwenzao ndio kabisaa anakurukaa
Maalim seif hajawahi kuwa mwanasiasa amejaaliwa kupendwa tu na wapemba wenzake lakin si mtu wa kumuamini kabisa
 
Huyu mzee wa MIGA angepewa nchi basi tulikuwa tunapelekwa pabaya sana, ana uchungu mkubwa, anaumia roho, ana chuki za wazi kwa wananchi ndio maana hawaiti kwa jina la kistaarabu, utasikia "Ma CCM"

Inahitaji akili ‘ya kiroho’ kumuelewa TAML. Bila shaka wewe na wengine wengi hamuwezi juu muelewa au hamtaki kumuelewa!
 
Kwa maoni yangu, ACT wame-surrender kwa Magufuli na maCCM. Hakuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoamuliwa na Wazanzibari wenyewe; bali ile inayoruhusiwa na Watanganyika, yaani Magufuli na maCCM ya Tanganyika.

Sisi Watanganyika ndio waamuzi wa kitu gani kifanyike Zanzibar, sio Hussein Mwinyi na Maalim Seif. Sisi Watanganyika ndio tunaotaka muafaka ambao utamtuliza Maalim Seif na kuituliza dunia ili isituwekee vikwazo vya kiuchumi kwa sababu ya dhulma zetu dhidi ya Wazanzibari.

Tumemtupia Maalim Seif mfupa mtupu (Makamu wa Kwanza wa Rais hana mamlaka yoyote ya maana kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar!) ili atulie na awatulize Wazanzibari wanaomuunga mkono na jumuiya ya kimataifa iliyochukizwa na dhulma zetu Zanzibar na Tanganyika.

Maalim Seif atalipwa mshahara na marupurupu mengine na kupigiwa saluti na mapolisi waliokuwa wanaua watu wake juzi. Zaidi ya hapo hatakuwa na chochote.

Serikali hii ya sasa ni tofauti na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Amani Karume na Maalim Seif. Ya mwanzo ilileta mabadiliko makubwa ya Katiba ya Zanzibar; kwa sababu Karume alikuwa anaunga mkono jitihada za Wazanzibari za kujivua kwenye ‘koti linalobana’ la Muungano.

Hussein Mwinyi ni kibaraka wetu moja kwa moja; tumemweka madarakani kwa bunduki na vifaru vya Bara na kura za Watanganyika waliopelekwa kupiga kura Zanzibar wakati Wazanzibari halali wanakataliwa kupiga kura.

Kibaraka wetu huyu hajampa Maalim Seif na ACT yake chochote zaidi ya vyeo visivyokuwa na mamlaka yoyote. Sasa Maalim Seif atatumika kujaribu kuhalalisha uharamia wa October 28. Atatumika kama toilet paper ya kusafishia uchafu wa maCCM na madhambi yao dhidi ya Wazanzibari.

Mimi naamini hatafanikiwa. Masikitiko yangu ni kwamba amekubali kutumika namna hii katika uzee wake. Baada ya miaka karibu arobaini ya kusimamia maslahi ya Wazanzibari, sasa amekubali kutumikia maslahi ya Tanganyika!
Acha hayo bro. Wewe unaraha zako huko. Tuache tusonge mbele
 
Back
Top Bottom