Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,539
ACT, Kwa nini mmetulia bado? mnaogopa mtashindwa? Mnajiona wanyonge? msiogope jaribuni mtaweza. Kama mkifeli msiogope jaribuni tena na tena. Msiogope changamoto; changamoto zipo tu ndivyo Ulimwengu ulivyo, kinachotakiwa ni kukabiliana nazo kwa kadiri zinavyojitokeza na kisha kusonga mbele. Msipo amua sasa na kutenda, mtakuwa mshajichakulia kushindwa! Mnapenda kushindwa? kama hampendi kwa nini mchague kushindwa sasa?
Amkeni muda ni huu ndugu zangu. Amueni kufanya vitu vikubwa sasa kwa manufaa ya nchi hii na Watanzania wote. Msijione wanyonge sana; Hakuna chama kilichoanzia juu, vyote vilianzia chini na kwa taabu nyingi.Msifikiri mtaibuka na kujikuta tayari mmefanikiwa, Never!.
Msijilinganishe na CCM, CCM tayari ni chama kikubwa na chenye historia pana na ndefu, na kila Chama kinaanzia katika mazingira yake kikiwa na fursa na changamoto tofauti na kingine. Msitegemee kupata fursa na changamoto sawa na wengine. Wala msipende kuwaiga chadema; CHADEMA ni chama chenye misingi, mienendo, malengo na kilichoanzishwa katika mazingira na muda tofauti na ninyi. Simameni ninyi kama ninyi na mshirikiane na wengine inapofaa kwenye mambo ambayo yanaweza kuwasaidia watanzania.
Ninyi ni watu wa muhimu na mna uwezo wa kufanya vitu vya maana vinavyoweza kuchangia kuipeleka nchi hii kwenye level nyingine. Hii ni kama mkiamua lakini! amueni kuwa tofauti in a positive way. Dunia ya sasa tunashindana kufanya vitu vya maana, sio kubishana na kushindana kwenye mambo yasiyo na faida, sio kwa kurudishana nyuma. Msiombee vyama vingine vikwame, hiyo haitawasaidia kitu wala haitawasaidia watanzania. Pambaneni kuji upgrade muwe bora zaidi ya wengine; hicho ndicho kinachotakiwa. Msituambie CCM hawajafanya nini, tuambieni ninyi mmefanya nini ambacho CCM na CHADEMA hawajafanya.
Mnafanya nini sasa ndugu zangu? je! Mmejaa wasiwasi ndani yenu? mnatakiwa mfahamu ninyi ni watu kamili na mnao uwezo mkubwa tu ndani yenu ila hamjaamua kuutumia ili matokeo yake yaonekana hadharani na kuchipua matunda ambayo yatawanufaisha watanzania.
Muda ni sasa ndugu zangu. Msiendelee kusubiri kwani hakuna cha kusubiri. Tanzania ni hii hii, watanzania ni hawa hawa. Muda uliopo ni ule ule masaa 24 kwa siku. msikubali sekunde, dakika, masaa na siku sikasogea wakati hamfanyi kitu. Msikubali ikapita hata dakika hamjafanya kitu ambacho kitakuwa na positive impact kwa watanzania. Jijengeni hivyo kisaikolojia kwamba kuanzia sasa hamtakiwi kupoteza muda mnashangaa tu.Matamko yanasaidia nini? by the way watoa matamko tayari tunao wengi, mnaweza kufanya nini cha zaidi? Hamtakiwi kusubiria Mtu mwingine afanye kitu halafu ndio muibuke kutoa tamko. Lengeni kufanya vitu vikubwa through out and keep such Discipline in you. Nawasihi fanyeni hivyo sasa.
Nawatakieni kila la heri.