ACT presha ya nini!

ACT presha ya nini!

laigwenan

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
325
Reaction score
80
Hiki ni chama kipya cha siasa inchini katika kujitambulisha sehemu mbalimbali ,ACT kinajipambanua kama wapigania democrasia wa kweli na wao ni wawazi na kimekuwa kikiwananga wapinzani wenzake hasa CHADEMA eti huko hakuna democrasia wala hakuna uwazi hii imenishangaza kwelikweli,kinajaribu kuwa ambia watu wajiungenacho kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli wala uwazi huko Chadema hapa ndipo ninapo washangaa zaidi,

Nilicho kitegemea mimi viongozi wa chama hichi wangetuuzia sera,itikadi ,dira,mipango,malengo na ilani zoa nilitegemea kuona sera za mazingira,afya,maji,kilimo,uwekezaji ,elimu,uchumi,usawa ,haki na nyingine nyingi kutoka ACT ambazo hazilingani na vyama vingine hasa CHADEMA, lakini mambo ni tofauti wanatuambia tujiungenacho tu kwa kuwa CHADEMA hakuna demokrasia! wala UWAZI haya ni maajabu .Kwa kuwakumbusha tu Chadema kimekuwa sauti ya wasio kuwa na sauti inchini hasa bungeni kimekuwa wasemaji wa watanzania maskini wasio na pa kusemea wamekuwa wawakilishi wa watanzania .

Napenda niwakumbushe ACT kuwa hutukuanza kuipenda CHADEMA hivihivi ila walitenda tukawaona,ACT acheni maneno bila vitendo kwani hizo ni taarabu tu,Napenda kuwa ambia ACT waTZ kwa wingi wao ni maskini wa kutupwa wengi wa walio maliza chuo kikuu wapo mtaani wakirandaranda hakuna ajira, wakulima wengi wanalima kwa jembe la mkono AFYA mbovu elimu inazorota ,barabara mbovu,maji hakuna na mabadiliko hakuna nilitegemea ACT watazungumzia sera hizi na si mapambano walio yaanza,ninapenda kuwaambia ACT hakuna democrasia duniani isiyo na mipaka hakuna.Na napenda kuwa kumbusha wa Tanzania waikumbuke CHADEMA wakati mwingine watakapo piga kura.
 
kawaida haki haichangamani na batili,hivyo kwa kadiri haki inavyochipua:ndivyo batili nayo inazidi kuchepuka! tatizo tunasahau Mwisho wa ubaya aibu, na ni bora lawama kuliko fedheha!
 
Betlehem Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT hapa JF.
 
kawaida haki haichangamani na batili,hivyo kwa kadiri haki inavyochipua:ndivyo batili nayo inazidi kuchepuka! tatizo tunasahau Mwisho wa ubaya aibu, na ni bora lawama kuliko fedheha!

demokrasia ipi hiyo unayoiongelea??? ya kuhongwa pesa? au ya kutumikia mabwana wawili??? act ishakufa hata kabla haijapata usajili wa kudumu!!
 
Act ndo mkombozi wa watanzania,cdm ni ukoo wa mtei,ni saccos ya mbowe na genge la wachaga.
 
shida act wanajidanganya kuwa wao ni maarufu sana kuliko chama walichokihama.imekula kwao.
itawagarim miaka 20 ijayo iwe kama cdm
 
Hiki ni chama kipya cha siasa inchini katika kujitambulisha sehemu mbalimbali ,ACT kinajipambanua kama wapigania democrasia wa kweli na wao ni wawazi na kimekuwa kikiwananga wapinzani wenzake hasa CHADEMA eti huko hakuna democrasia wala hakuna uwazi hii imenishangaza kwelikweli,kinajaribu kuwa ambia watu wajiungenacho kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli wala uwazi huko Chadema hapa ndipo ninapo washangaa zaidi,

Nilicho kitegemea mimi viongozi wa chama hichi wangetuuzia sera,itikadi ,dira,mipango,malengo na ilani zoa nilitegemea kuona sera za mazingira,afya,maji,kilimo,uwekezaji ,elimu,uchumi,usawa ,haki na nyingine nyingi kutoka ACT ambazo hazilingani na vyama vingine hasa CHADEMA, lakini mambo ni tofauti wanatuambia tujiungenacho tu kwa kuwa CHADEMA hakuna demokrasia! wala UWAZI haya ni maajabu .Kwa kuwakumbusha tu Chadema kimekuwa sauti ya wasio kuwa na sauti inchini hasa bungeni kimekuwa wasemaji wa watanzania maskini wasio na pa kusemea wamekuwa wawakilishi wa watanzania .

Napenda niwakumbushe ACT kuwa hutukuanza kuipenda CHADEMA hivihivi ila walitenda tukawaona,ACT acheni maneno bila vitendo kwani hizo ni taarabu tu,Napenda kuwa ambia ACT waTZ kwa wingi wao ni maskini wa kutupwa wengi wa walio maliza chuo kikuu wapo mtaani wakirandaranda hakuna ajira, wakulima wengi wanalima kwa jembe la mkono AFYA mbovu elimu inazorota ,barabara mbovu,maji hakuna na mabadiliko hakuna nilitegemea ACT watazungumzia sera hizi na si mapambano walio yaanza,ninapenda kuwaambia ACT hakuna democrasia duniani isiyo na mipaka hakuna.Na napenda kuwa kumbusha wa Tanzania waikumbuke CHADEMA wakati mwingine watakapo piga kura.

naamini ulikimbia umande wewe, kajifunze kuandika kwanza ndio urudi hapa...
 
ACT ni chama makini sana cha siasa. ni mkombozi wa watanzania . Watanzania wote wanaipenda sana ACT
 
Back
Top Bottom