ACT kufutwa? Mutungi anajua, Zitto anajua, Limbu anajua, Nyakarungu anajua, Mwigamba anajua, Kitila Mkumbo nk.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Ninatamani sana siku moja watu wote tuwe na uoni sawa, ufikiri sawa, na uamuzi sawa. Bahati mbaya hilo halitawezekana chini ya jua aishipo bin-adamu. Hata katikati ya msitu wa wajinga, kamwe hawatawaza na kufikiri sawa.

Lakini ikiwa siku moja tutabahatika kujifunza kitu kinachoitwa lugha za siri, ama kwa lugha ya kitumwa zinaitwa "Code Language", basi tutaishi na kuidhibiti hila na uovu wote duniani,

Kwanini Jaji Mutungi anatumia code language ngumu kiasi hiki kwa jamii dhaifu? Mutungi anajua kwanini hili, bahati nzuri Zitto anajua kwanini hili. Furaha yangu ninamuona Zitto yule niliyetamani kumuona miaka mingi nyuma, Zitto yule anayezungumza lugha ngumu ya kiukombozi yenye mamlaka na kwa hakika ukitaka kumfaidi Zitto, msikilize akiwa amekwazika sanasana.

Act inafutwa, hawa hawatanii na hawajaribu, wako serious wamejiandaa kuifuta, Mutungi ndie aliyeisajiri ACT, anajua mtego ulipo, lakini Mutungi ndie anayeifuta ACT anajua vilevile mtego ulipo. Zitto anajua, Lucas Limbu anajua, Grayson M Nyakarungu anajua, Mwigamba anajua, Kitila Mkumbo anajua, Habib Mchange anajua, na wengine wanajua. Hawa wana kura ya veto. Kinachoitwa mashitaka katika barua hii ya Mutungi ni Code Language tu.

Anayeshughulikiwa sio ACT, bali ni Maalim Seif, hili mimi nililiona mapema kabla Maalim hajahamia ACT, nikatoa angalizo ambalo kimsingi nilitumia "Code Language" bahati mbaya wagumu hamkunielewa, na baada ya maalim kujiunga ACT nikatoa tahadhari kwa vyama vyote, nikitumia code language, vilevile sikueleweka kabisa nikaishia kutukanwa na kudhalilishwa. Lakini nilifurahi kabisa.

Kama ni sehemu muhimu ambayo Chadema tunatakiwa kuungana na ACT kwahakika nikuhakikisha tunazuia uhalifu huu, tukiruhusu ACT ifutwe, tumeruhusu Chadema ifutwe pia. Wale wahafidhina wenzangu wa Chadema tuvumiliane, twendeni kuitetea ACT, tukifanikiwa kuitetea ikasalimika, tutarudi kwenye siasa zetu za vyama.

Na Yericko Nyerere

FB_IMG_1553665604186.jpg
FB_IMG_1553665586830.jpg
 
Wanachama wa ACT wazalendo watahama tena CCM
Tuvute subira
CCM ni ileile
 
Hali ya SIASA haitabiliki unaweza kusema CHADEMA ianze mapambano dhidi jaji mtungi na yenyewe ikaingia mkenge akatokea muhuni mmoja kutoka kwa lipumba akajifanya anahamia CHADEMA akajifanya anachoma bendera pamoja na kadi tukajikuta tunalimwa barua ya kijieleza kwanini CHADEMA isifutwe, kumbuka CHADEMA inawindwa kuliko tembo na faru kwa majangili tukajikuta tunaanza mapambano mengne mapya ya kukinusuru chama chetu kwa kifupi CHADEMA iwe makini kuliko umakini wenyewe,"maana sheria mpya ya vyama vya SIASA imetungwa mahususi kupambana na vyama mbadala,hasa CHADEMA na washirika wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni wakati muhimu sana kwa CDM kusimama na ZZK, ZZK ameonyesha ukomavu na ujasiri wa mapambano akiwa jeshi la mtu mmoja anayepambana na hoja. Nguvu ya Seif na wenzake ACT imeamsha harakati mpya ambazo CDM hawana budi kujiunga nazo.. Suala hili limenifanya nione CCM walivyo wepesi, CDM muongezeeni ZZK nguvu anaweza na uthubutu anao pia na pindi mkianzisha hilo vuguvugu ni vyema mkahakikisha LISSU anarudi mkiwa tayari kwenye nguvu moja na ACT..
 
Naona mpiga ramli anaendelea na kazi yake?

Yaani waliacha kuifuta CHADEMA Lowasa alivyohamia huko ndo waje waifute ACT?

Hawa hawana shida na maalimu Seif bali wanashida na wananchi wanaotaka kujiamulia kwa haki mustakbali wao kupitia sanduku la kura, hata asingekuwa ni maalim seif laiti akitokea mtu yeyote ambaye wananchi wanamuunga mkono watafanya tu mambo yao hayahaya!
 
Tunakoenda ndio mtaelewa, Chadema inamuhitaji Zitto kipindi hiki kuliko Zitto anavyoihitaji Chadema.

Mkifanikiwa kumnasa Zitto na Maalim kurudi Chadema na kukubali demokrasia huru ndani ya chama litakuwa goli la karne kuwafunga CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati huo tume ya uchagzi bado inateuliwa na Mwenyekiti wa CCM?
 
Back
Top Bottom