Zitto Kabwe: ACT - Wazalendo kilianzishwa na watu watatu tu; Mimi, Kitila Mkumbo na Mwanaharakati mmoja wa kike

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
217
500
Akiongea mapema leo asubuhi katika kipindi cha Joto Kali la asubuhi kinachorushwa na vyombo vya habari vya TVE na Efm Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, ameongea mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na ameichambua bajeti kuu ya Serikali iliyowasilishwa week iliyopita Bungeni.

Kwa upande wa kuanzishwa kwa chama chake amesema chama chao kilianzishwa kutokana na mchango mkubwa wa Professor Kitila Mkumbo (ambaye amesema ndiye mwandishi wa katiba ya ACT-WAZALENDO), yeye mwenyewe (Zito) na Mwanaharakati mmoja mwenye jinsia ya kike ambaye aligoma kumtaja!.

Zito alijibu hivyo baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa kipindi hicho, Jeradi Hando, alilomuuliza ni vipi chama kiliathirika baada ya viongozi wakuu wa chama chao kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali serikalini katika awamu ya tano. Miongoni mwa viongozi alikuwa ni Anna Mgwira, ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Pia kuna Kitila Mkumbo(Phd), alikuwa mshauri mkuu wa chama, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya maji na umwagiliaji. Zito aliamini hakukuwa na ulazima kwa Kitila Mkumbo kuondoka katika chama alichokianzisha yeye mwenyewe na kwenda CCM badala yake angefanya kazi zake za Serikali ilihali akiwa bado mpinzani.

Swali langu ni, kwanini Zito aliogopa kumtaja huyo Mwanaharakati wa kike? Na anaweza akawa ni nani? Au Fatma Karume aka Shangazi, maana kuna kipindi alikuwa karibu na ACT - Wazalendo ata kwenye mkutano wao mkuu Shangazi alionekana ku-engineer mambo fulani fulani katika harakati za kutafuta kuingia "White House".
 
Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,877
2,000
Zito ni dramma queen. Hicho Chama wala hawakikusnzisha wao bali walihamia tu.

Nilipofukuzwa nilitamani kujiunga NCCR -Zitto​

JUMATANO , 6TH MEI , 2015

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa alipofukuzwa wanachama katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alitamani kujiunga na Chama Cha NCCR-Mageuzi kwani ndicho chama ambacho kilikuwa
kinaendana na itikadi yake anayoifuata na kuiamini ambayo ni itikadi ya Ujamaa. Zitto Kabwe amefunguka haya leo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha KIKAANGONI ambacho kimeanza upya katika msimu wa pili na kitakuwa kikifanyika kila Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka kumi Alasiri.

Zitto Kabwe alisema kuwa alishindwa kujiunga na Chama hicho cha NCCR-Mageuzi kutokana na kuwepo kwa matatizo hivyo aliona siyo vyema kujiunga nacho, ndiyo maana alifikiri kuwa na chama cha siasa ambacho kitakuwa na misingi na itikadi ambayo yeye anaiamini na kuisimamia. katika hili moja ya shabiki alitaka kujua kwanini aliamua kujiunga na ACT Wazalendo na kuacha kujiunga na chama kilichokomaa kisiasa kama TLP,NCCR-Mageuzi,CUF, au CCM na majibu ya Zitto yalikuwa kama hivi.

"Nilifikiria hivyo pia lakini nikaona kuwa ni vema sasa kuwa na chama cha siasa ambacho kina itikadi ninayoifuata na kuiamini nayo ni itikadi ya Ujamaa. Chama cha NCCR-M mageuzi pekee ndio kinakaribia kuwa na itikadi hiyo lakini napo kulikuwa na matatizo ambayo kujiunga kwangu nao ingekuwa sio vema. Pili mimi ni mpiganaji.

Wengine wananiita jeshi la mtu mmoja! Sio kweli lakini. Hivyo kwenda chama kichanga ni ujasiri wa hali ya juu. Mungu atasaidia hakitakuwa chama kichanga baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2015".

"Mimi sio mwanzilishi wa ACT Wazalendo isipokuwa waanzilishi walikuwa watu ninaoshabihiana nao kwenye itikadi kama Prof. Kitila Mkumbo na Ndugu Mwigamba" Aliongeza Zitto Kabwe.

Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo ambaye kwa sasa amekuwa akiitwa majina mengi ya ajabu ajabu kama msaliti,Yuda, kibaraka wa CMM na mengine mengi amesema kuwa hilo ni suala la kawaida katika siasa maaana hayo ni maneno tu ambayo hata baadhi ya viongozi wakubwa katika vyama vya siasa walishaitwa majina hayo ila anasisitiza jambo
 
Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,877
2,000
Naweza kukubaliana na wewe. Kwasasa ni lecturer UDSM, nadhani pia kaepuka kumtaja kwasababu ni mtumishi wa umma.
Anaogopa nini sasa?
Screenshot_20210614-115710_Google.jpg
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,741
2,000
Siyo Nilipofukuzwa nilitamani kujiunga NCCR hapana kuwa mkweli Mr. Zitto sema hivi nilipotaka kuupindua uongozi halali wa CDM uliokuwepo kikagundulika na ndipo nikatamani kujiunga NCCR Mageuzi kuficha aibu.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
17,977

Vijana wa chaggadomo hamjawahi kuwa na akili. Punguzeni bange
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,741
2,000
Vijana wa chaggadomo hamjawahi kuwa na akili. Punguzeni bange
kwa kawaida ukweli huwa unauma !!

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
17,977
2,000
kwa kawaida ukweli huwa unauma !!

Ndani ya CHADEMA kila mtu ni msaliti mtarajiwa isipokuwa Mbowe tu.
 
nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
901
500
Zito ni dramma queen. Hicho Chama wala hawakikusnzisha wao bali walihamia tu.

Nilipofukuzwa nilitamani kujiunga NCCR -Zitto​

JUMATANO , 6TH MEI , 2015

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa alipofukuzwa wanachama katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alitamani kujiunga na Chama Cha NCCR-Mageuzi kwani ndicho chama ambacho kilikuwa
kinaendana na itikadi yake anayoifuata na kuiamini ambayo ni itikadi ya Ujamaa. Zitto Kabwe amefunguka haya leo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha KIKAANGONI ambacho kimeanza upya katika msimu wa pili na kitakuwa kikifanyika kila Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka kumi Alasiri.

Zitto Kabwe alisema kuwa alishindwa kujiunga na Chama hicho cha NCCR-Mageuzi kutokana na kuwepo kwa matatizo hivyo aliona siyo vyema kujiunga nacho, ndiyo maana alifikiri kuwa na chama cha siasa ambacho kitakuwa na misingi na itikadi ambayo yeye anaiamini na kuisimamia. katika hili moja ya shabiki alitaka kujua kwanini aliamua kujiunga na ACT Wazalendo na kuacha kujiunga na chama kilichokomaa kisiasa kama TLP,NCCR-Mageuzi,CUF, au CCM na majibu ya Zitto yalikuwa kama hivi.

"Nilifikiria hivyo pia lakini nikaona kuwa ni vema sasa kuwa na chama cha siasa ambacho kina itikadi ninayoifuata na kuiamini nayo ni itikadi ya Ujamaa. Chama cha NCCR-M mageuzi pekee ndio kinakaribia kuwa na itikadi hiyo lakini napo kulikuwa na matatizo ambayo kujiunga kwangu nao ingekuwa sio vema. Pili mimi ni mpiganaji.

Wengine wananiita jeshi la mtu mmoja! Sio kweli lakini. Hivyo kwenda chama kichanga ni ujasiri wa hali ya juu. Mungu atasaidia hakitakuwa chama kichanga baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2015".

"Mimi sio mwanzilishi wa ACT Wazalendo isipokuwa waanzilishi walikuwa watu ninaoshabihiana nao kwenye itikadi kama Prof. Kitila Mkumbo na Ndugu Mwigamba" Aliongeza Zitto Kabwe.

Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo ambaye kwa sasa amekuwa akiitwa majina mengi ya ajabu ajabu kama msaliti,Yuda, kibaraka wa CMM na mengine mengi amesema kuwa hilo ni suala la kawaida katika siasa maaana hayo ni maneno tu ambayo hata baadhi ya viongozi wakubwa katika vyama vya siasa walishaitwa majina hayo ila anasisitiza jambo
Nafahamu hivyo pia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom