ACT au CHADEMA jiimarisheni mapema for 2020!

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,556
2,000
Kwa hali ilivyo sasaivi, serikali madarakani ina miaka miwili tu (2017 na 2018) ya kufanya kazi kututhibitishia kama wana uwezo wa kuchaguliwa tena 2020. kwa mwaka mmoja huu, hali imekuwa mbaya zaidi kuliko hata kipindi cha nyumba. hali ni mbaya kwenye uhuru wa habari (Melo amewekwa ndani bila kujali kama jf ndio imeisaidia serikali kwa kufichua uovu wanaojifanya wametumua watu), vyombo vyote vya habari havina amani, sheria kandamizi kwenye uhuru wa kuongea na umasikini unazidi.

Ofisi za umma hakuna pesa, sio pesa za kuiba, bali pesa za kuendesha nchi. nasema hivyo kwasababu kuna malimbikizo makubwa sana ya mishahara na madai, watu wengine wanadai hadi miaka mitano hadi saba. Waalimu wana madai hayatekelezwi, wafanyakazi wengine wengi wana madai hadi leo hawajalipwa na hawategemei kulipwa, tunaambiwa hela ya kuendesha ofisi za umma inapelekwa kidogo sana hivyo watu wanashindwa kufanya kazi.

ACT WAZALENDO au CHADEMA, au chama chochote kipya kitakachoundwa, mnachotakiwa kufanya kwa sasa ni kujijenga na kujenga mikakati, CDM jisafisheni mafundofundo yenu, act sambaeni maeneo ambayo hampo wengi, CUF nachelea kusema kwasababu zenji imewasambaratisha, hata hivyo jisafisheni kabla ya wakati. 2020 mtakuwa na kazi ndogo sana katika kampeni kwasababu watu wana machungu moyoni, yale waliyoahidiwa hawayaoni, maisha yamekuwa magumu kuliko hata kipindi cha mafisadi, biashara ni ngumu, mabenk yanauza nyumba za rehani watu walichukua mikopo na hata wakiuza wateja wa hizo nyumba hawapatikani. Bandari imepunguza utendaji kama zamani, bandari kavu hazina biashara tena, biashara ya usafirishaji haina faida tena, watu walikuwa na malori mengi hata mia, wameajiri madereva mia kwa mfano hapo na makondactor mia, kama biashara ya kusafirisha mizigo imepungua kwasababu ya utendaji wa bandari, that means hao wote hawana kazi, familia ngapi hizo? kuna kampuni ngapi za kusafirisha mizigo tz, hizo hali zao zikoje kwa sasa?

TUNAHITAJI MBADALA WA UONGOZI. kwanza kabisa, hatutaki serikali inayobana uhuru wa kuongea kama tupo Rwanda au North korea. hatutaki serikali ambayo utendaji wake unasababisha maisha magumu kwa raia (mafisadi wapate tu shida, ila sasa hata wasio mafisadi ndio wanaoumia zaidi). unawezaje kung'oa mti ndani ya nyumba bila kuangalia kama utadondosha na nyumba yote au la, hapo utafanya kwa polepole na kwa awamu.

FAIDA YAKE, 2019 serikali haitafanya kazi, bali itakuwa inajiandaa kwa kampeni tu. muda umeshaisha, na 2020 sio mbali, na nina uhakika, tutafika tukiwa na hali hii hii na kuna watu watashindwa cha kuonyesha walichokifanya miaka yote mitano 5....

wapinzani mtakuwa na kazi rahisi sana. tunawategemea. tafadhali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom