Acheni tabia ya kuiga mambo yasiyofaa

Acheni tabia ya kuiga mambo yasiyofaa

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,589
Hay marafiki zangu;

natumai mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na shughuli zenu na masomo kwa wale wanaosoma na biashara kwa wafanyabiashara, nawatakia kheri na fanaka naa ufanisi wa hali ya juu katika majukumu yenu

blue monday ya leo nimeonelea niongee nanyi jambo hili ambalo limenitatiza kichwani mwangu na nimeona nilitoe hapa kwenu wapendwa wangu,

wakati mwingine twajifunza vitu kwa kuona na kuiga. Na mambo mengine huwezi kufanya bila kuangalia umuhimu wa kitu unachotaka kukifanya kwa wakati huo, jamii ya sasa inajifunza vitu kwa kuona na kuiga mambo ya magharibi wanavyofanya, mpaka imepelekea kutothamini tamaduni na mila zetu. Vijana wengi wamejitumbukiza katika mambo ya kisasa na kuona hayo yanafaa na kumbe wanajidanganya wenyewe na kujiangamiza.

Hii hali ya watu, hususani vijana wengi kuiga mambo ambayo hayafai kabisa kwa jamii, wewe unangalia luninga hasa wanamuiziki wa majuu unaiga tembea, simama, uvvaaji wa nguo zao na hata kuongea pia siku hizi vijana wengi wanaiga mno, utakuta mtu kavaa nguo mpaka inasema utanidondosha chini yani iko chini ya makalio jamani kwanini lakini kwani kuvaa kawaida kutakuletea nini mpaka uvae hivyo.
Acheni kuiga fanya kile ambacho waweza fanya kwa mikono yako na nguvu zako
kwani unafikiri bill gate alimwiga nani kuanzisha microsoft ni ubunifu/ ugunduzi na kipawa alichopewa
na mungu kama nawe una kipawa/kipaji anza kukifanyia kazi usiige acha dhana ya kuiga haitakupeleka mbali mwishoe utabaki tu unashangaa na kuduwaa na mambo uliyoyaiga hayatafika mbali.

Fanya kwa uwezo na kipaji ulichonacho nawe utaona mafanikio

nawatakia siku njema na kazi njema
 
Wanasema eti wanaenda na wakati:rockon:

Wanajidanganya huwezi kwenda na wakati ila unaukomboa wakati...hakuna jipya chini ya jua Mungu huyaleta mambo ya zamani na kuonekana mapya Mhubiri 3:15,nashangaa utasikia eti tajiri wa kwanza duniani wakati tajiri wa kwanza ni Sueleman aliyekuwa na dhahabu na pesa kama mchanga,kama ni wazuri walikuwepo akina Sara,ndo maana wengine wanageuka mashoga kisa Marekani mbona kuna mashoga poleni.
 
yani umenifurahisha sana kwa comment yako imejaa upako wa hali ya juu yani ungekuwa karibu ningekupa kazawadi ila pokea zawadi hii ndogo ya keki ule na uwapendao cake1.jpeg
Wanajidanganya huwezi kwenda na wakati ila unaukomboa wakati...hakuna jipya chini ya jua Mungu huyaleta mambo ya zamani na kuonekana mapya Mhubiri 3:15,nashangaa utasikia eti tajiri wa kwanza duniani wakati tajiri wa kwanza ni Sueleman aliyekuwa na dhahabu na pesa kama mchanga,kama ni wazuri walikuwepo akina Sara,ndo maana wengine wanageuka mashoga kisa Marekani mbona kuna mashoga poleni.
 
Tunao pendelea kuvaa jeans imekula kwetu madukani zimejaa zakubana sie wengine hatuwezi mwee, yaani inakulazmisha uishushe kidogo ndo inakuwa mwake
 
Bila shaka wewe ni old timer..lady furahia..ennnh!!!mim nina kiuno kidogo kwaio nikivaa jeans sehem ya husika nachekesha vibaya mno!! Nikishusha ndo inaweza niangalia sasa unasemaje kwa hilo!! Eennhhh
 
ulimbukeni ndio tatizo kikubwa ni kujua unachokiinga kinafaida gani kwa jamii
 
Back
Top Bottom