Acheni majungu! Waziri Luhaga Mpina ang’aka baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki eka 1,000 za ardhi

wogakuria

JF-Expert Member
Aug 15, 2018
743
1,223
Mpina ang’aka sakata la kumiliki eka 1,000 Moro

Morogoro/Dar. “Acheni majungu.” Hiki ndicho alichojibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki eka 1,000 za ardhi.

“Hayo unayouliza ni majungu, acha majungu bwana na kama katibu mkuu (wa CCM, Dk Bashiru Ally) ameongea si muulize yeye?”
Waziri huyo alipoulizwa kama ardhi hiyo ni ya kwake alikata simu.

Juzi, Dk Bashiru wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Wanawake la CCM (UWT) mjini Dodoma, alisema atamwita waziri mmoja (hakumtaja) anayemiliki eka 1,000 za ardhi mkoani Morogoro ili aeleze amezipata wapi.

“Lakini hivi karibuni imezuka tabia miongoni mwetu, wengine ni viongozi wetu kuhodhi ardhi au kuwageuza Watanzania kuwa vibarua kwa kuwakodisha,” alisema katibu mkuu huyo.

Awali, Juni mwaka huu, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro walimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuingilia kati mgogoro uliodumu kwa miaka saba baina ya Mpina na wananchi wa vijiji vya Dala na Kongwa.

Katika mgogoro huo, wananchi wanadai waziri huyo amechukua mashamba yao eka 700 katika kijiji kimoja na nyingine 300 katika kijiji kingine.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani, mwenyekiti wa baraza la madiwani la halmashauri hiyo, Kibena Kingo alisema kuna mgogoro kati ya waziri huyo na wananchi.

Kingo alisema hayo baada ya mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Morogoro, Jasmine Tiisekwa kuitaka halmashauri hiyo kutoa taarifa ya namna mgogoro huo unavyoshughulikiwa.

Katika kikao hicho, Tiisekwa alidai taarifa alizonazo zinaonyesha kwamba mgogoro huo umefikia hatua mbaya kwa kuwa baadhi ya wakulima wameharibiwa mazao yao ukiwamo mpunga na mahindi na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi wa shamba hilo la Waziri Mpina lenye ukubwa wa eka 700.

“Nikiwa kwenye uzinduzi wa Kituo cha Mabasi cha Msamvu uliofanywa na Mheshimiwa Rais, nilifuatwa na mama mmoja ambaye ni mlemavu huku akilia na kuniambia kwamba shamba lake la mpunga la eka tano limeharibiwa na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi wa shamba la Waziri Mpina, hivyo naomba kupata majibu mgogoro huu umetatuliwa vipi?” aliuliza Tiisekwa katika kikao chao cha madiwani.

Mbunge huyo, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii alisema Sheria ya Ardhi hairuhusu halmashauri za vijiji kutoa maeneo zaidi ya eka 50 na kwamba, mwenye mamlaka ya kutoa eka hizo 700 ni kamishna wa ardhi.

Awali, akitoa ufafanuzi wa mgogoro huo, aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Sudi Mpili alisema mgogoro wa kwanza ulitokea baada ya Mpina kujenga tuta kwenye Mto Mbwade kwa ajili ya kuelekeza maji katika shamba lake la eka 300 lililopo Kata ya Bonye ambalo nalo umiliki wake una shaka.

Alidai waziri huyo alitumia ujanja kwa kuandika majina sita ya watu tofauti na kuomba eka 50 kwa kila jina kwa lengo la kumiliki eka 300, jambo ambalo ni kinyume cha sheria kwani hata alipotakiwa kuwapeleka watu hao kwenye serikali ya kijiji kuwatambua alishindwa kufanya hivyo.

Mpili alidai walinzi wa shamba la waziri huyo wamekuwa wakilinda tuta hilo usiku na mchana huku wakulima waliokuwa wakitegemea maji hayo kwa kilimo cha umwagiliaji wakiyakosa.

Alidai kuwa mgogoro mwingine ulitokea katika Kijiji cha Dala, Kata ya Mvuha baada ya waziri huyo kuiomba serikali ya kijiji shamba la eka 700.

Hata hivyo, kabla ya maombi hayo kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji, anadaiwa kuwa alianza kulima na baadhi ya wanakijiji waliokuwa wakilima kufukuzwa katika shamba hilo na wengine kuharibiwa mazao yao.

Alidai kuwa wakulima walirubuniwa na baadhi ya wajumbe wa serikali ya Kijiji cha Dala ambao walikubali kumuonyesha eneo la eka 700 bila ya kushirikisha mkutano wa kijiji jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Diwani wa viti maalumu, Kata ya Mvuha, Rehema Jongo alimshauri mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuandaa mkutano wa kijiji na kumshirikisha Mpina ili mgogoro huo utatuliwe kwa njia ya mazungumzo.

Jongo alisema kitendo alichokifanya waziri huyo ni uvunjaji wa sheria akidai ametumia madaraka yake vibaya na kwamba baraza la madiwani litahakikisha mgogoro huo unatatuliwa kwa mujibu wa sheria na si cheo cha mtu.
 
Mpina awe msafi kwenye hili. Hatutaki double standard katika hili.
Nadhani nimemuelewa Waziri,Katibu Bashiru angemuita kwenye vikao vya Chama ili amfinyie huko huko ili wananchi waone manyoya ya waziri...hehehe.
 

Kuna mtu nimeona ameandika kwamba,kipindi cha JK waliiba wengi ila kipindi hiki wanaiba wachache na ni kama vile wapendwa fulani hivi.
 
hayo mashamba yalinunuliwa wakati akiwa mbunge tu enzi za ikwete.
Gervase


Kuna mtu nimeona ameandika kwamba,kipindi cha JK waliiba wengi ila kipindi hiki wanaiba wachache na ni kama vile wapendwa fulani hivi.
 
Yanalindana hayo maCCM. Angekuwa Sumaye angeshanyang'anywa siku nyingi. Hata huyo Bashiru amekuwa professional propagandist.
 
Naomba mnipe jina la mwanaCCM mmoja tu ambaye ni msafi humo kwenye genge lao. Ukianza na muuza nyumba za serikali na kugawa kwa mahawara zake.
 
hayo mashamba yalinunuliwa wakati akiwa mbunge tu enzi za ikwete.
Gervase
=====
Kumbe. Je. Taratibu zilifuatwa?
 
Kweli ni majungu mnataka wao wasimiliki chochote ili wakifukuzwa wafe njaa
 
Back
Top Bottom