Acheni kuponda wanaume wa Dar kuficha udhaifu wenu

Kumekuwa na trend nzuri ya kuponda wanaume wa dar. Nafikiri wengi hawajui uhalisia wa wanaume wa dar
Sifa zao ni hizi
1. Wengi wasomi na wanajua kutunza afya zao ndio maana hawali hovyo kama wana mapepo. Siku tulizonazo hizi wanga ni tatizo kubwa sana. Hizi ndio sababu wanaume wengi wa mikoani wana vitambulisho tofauti na wanaume wa dar ambao angalau wana nidhamu ya kula
2. Ni wastaarabu. Dar mambo ya kupigana pigana tumewaambia kuku na wanaume wa mikoani. Tunapigania na maisha na sio kupiga mtu

3. Wanaume wa dar hawapigi wake zao na hawaui sababu ya kusalitiwa. Visa vya mauaji vikosi sana mikoani. Wanaume wa mikoani wakatili sana. We ona mtu anajua mke wake na kumfukia kwenye shimo la choo.

4. Wanaume wa dar hawanaga masifa ya kijinga jinga. Sijui eti nimemkomoa au kujisifia kulala na wengi ujinga mtupu. Dar ni wastaarabu sana.

5. Wanaume wa dar hawadharirishi wanawake sababu ya uvaaji wao. Nimeona mikoani jitu zima linaanza kumzome mwanamke sababu ya alivyovaa. Wewe Mungu amekukupa macho na kope za nini?
Usipopenda tazama kwingine. Dar tunaheshimu uhuru na uchaguzi wa watu.
6. Wanaume wa dar ni wachakarikaji sana na wanajua maisha ni nini labda mateja. Angalia hao wa mikoani utajua tofauti.

Proud to be mwanaume wa dar
Huwezi kula ugali uliotiwa hamira ukafikiri sawasawa
 
Back
Top Bottom