bhikola
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,133
- 1,668
Inawezekana kwamba kuna mambo yanayoendelea na hayako sawa nchini kwetu, lakini naanza kuamini pia kuwa kuna watu kwa makusudi tu wanamuonea kabisa Rais wetu.
1. Nimesikia watu wakiongea kila kinachofanyika Chato, as if kuleta maendeleo Chato ni tatizo. Wakati huohuo kuna mambo kibao yanaendelea Ruangwa, lakini yanaonekana ni sawa.
2. Kuna kipindi askofu Niwemugizi alihojiwa kuhusu uraia wake. Watu wakajenga hoja kuwa inakuwaje miaka yote hiyo mpaka amekuwa askofu lakini hawajui uraia wake? Lakini hawataki kujiuliza swali lile lile wanalojiuliza kwa askofu.
3. Leo nimeona watu wakimponda Pengo kwa alichokisema wakati akiongoza ibada ya leo. Lakini ni hao hao walioongea kuhusu waraka wa Pasaka wa Maaskofu wa KKKT. Hawajiulizi kwamba, uhuru waliotumia maaskofu wa KKKT ndo huo huo anatumia askofu Pengo?
Naanza kupata shaka kama kweli Watanzania wanajua kile kitu hasa wanataka kupata.
Ni hayo tu kwa Leo