Acheni kulilia mapenzi

Acheni kulilia mapenzi

Habari zenu ndugu zangu,

Mapenzi huchukua sehemu kubwa ya maisha yetu kwa maana kwamba kila mmoja wetu hutokea kumpenda mtu na akahitaji kuwa nae kwa maisha yake yote. Si mara zote mambo huenda kama tunavyotarajia hasa kwa dunia yetu ya leo iliyojaa usaliti wa kila aina.

Sasa ushauri wangu ni kuwa tuache kulia lia, kulalamika au kukata tamaa pale utamu wa mapenzi unapogeuka kuwa shubiri. Maisha ni lazima yaendelee, after all everyone should be in charge of their own happiness.

Kuna mshauri mmoja aliwahi kuniambia, unapoachwa na mtu kaa chini utulie tafuta peni na karatasi uanze kuandika mazuri na mabaya ya huyo mtu utashangaa kuwa alikuwa na mabaya mengi kuliko mazuri ndipo utakapoona kuwa kuna mengi ulikuwa unavumilia tu ilimradi asikuache.

Tuache kujitesa, ni kweli kumsahau mtu ghafla haiwezekani ila usiruhusu starehe zake yeye zikutese wewe. Kama ulikuwa muaminifu, mkweli na mwenye upendo wa kweli kwake na bado akakuacha amini kuwa hastahili machozi yako ameshampata wa kufanana nae. Kuna msemo usemao "likuepukalo lina heri nawe"

Kuumizwa tumeumizwa wengi na tushasahau huu ni ujumbe kwa wale wanaoomboleza kuachwa na mtu miaka na miaka.

Wakati mwingine ni vigumu kujigundua kuwa ulikuwa mfungwa hadi pale utakapoachwa huru.

Big up mkuu!
 
Maneno yako yatawasaidia sana wale wasiojua kusahau na kuendelea na maisha mapya
 
Back
Top Bottom