Acheni kulilia mapenzi

Acheni kulilia mapenzi

Ximena

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
641
Reaction score
353
Habari zenu ndugu zangu,

Mapenzi huchukua sehemu kubwa ya maisha yetu kwa maana kwamba kila mmoja wetu hutokea kumpenda mtu na akahitaji kuwa nae kwa maisha yake yote. Si mara zote mambo huenda kama tunavyotarajia hasa kwa dunia yetu ya leo iliyojaa usaliti wa kila aina.

Sasa ushauri wangu ni kuwa tuache kulia lia, kulalamika au kukata tamaa pale utamu wa mapenzi unapogeuka kuwa shubiri. Maisha ni lazima yaendelee, after all everyone should be in charge of their own happiness.

Kuna mshauri mmoja aliwahi kuniambia, unapoachwa na mtu kaa chini utulie tafuta peni na karatasi uanze kuandika mazuri na mabaya ya huyo mtu utashangaa kuwa alikuwa na mabaya mengi kuliko mazuri ndipo utakapoona kuwa kuna mengi ulikuwa unavumilia tu ilimradi asikuache.

Tuache kujitesa, ni kweli kumsahau mtu ghafla haiwezekani ila usiruhusu starehe zake yeye zikutese wewe. Kama ulikuwa muaminifu, mkweli na mwenye upendo wa kweli kwake na bado akakuacha amini kuwa hastahili machozi yako ameshampata wa kufanana nae. Kuna msemo usemao "likuepukalo lina heri nawe"

Kuumizwa tumeumizwa wengi na tushasahau huu ni ujumbe kwa wale wanaoomboleza kuachwa na mtu miaka na miaka.

Wakati mwingine ni vigumu kujigundua kuwa ulikuwa mfungwa hadi pale utakapoachwa huru.
 
yeeeees niliachwa some months ago....
 
Kala za uso anajifariji na jf pole utapata mwingine mbona wapo wengi wazuri tu!
 
Umeona eeeh tatizo kukubali kuwa umeachwa na unatakiwa uendelee na maisha yako ndo ugumu unapoanzia hapo

inatakiwa tukubali ukweli tu, naona hapa watu washaanza kuhoji kuwa nimeachwa utadhani kuachwa ni dhambi.

Niliachwa nikakubali matokeo maisha yakaendelea, sasa kuna rafiki yangu yeye amegoma kukubali kuwa ashapigwa chini ndo nikamwambia tu mbona mie niliachwa lakini sijafa!
 
Nimekusoma sana mkuu mimi mwenyewe ni muhanga wa hilo but naamini yatapita and life must going on))>>>>>>
 
Back
Top Bottom