Acheni kulialia na mapenzi

Ulichokisema ni sahihi na mimi ni shahidi. Ukiwa na pesa,hata kulia kwako si kama kwa asie nazo, ni rahisi kurecover. Mtu akikutibua,unajipa likizo ya siku 7 unaenda mbugani au nchi jirani kuzurura,ukirudi uko timamu maisha yanaenda. Au ukiona haifai kutumia pesa nyingi, kwa sisi wenye watoto,unawapeleka shopping ya nguvu watoto, kuona furaha yao tu usoni ni faraja tosha. Sasa umwagwe ukiwa huna hela, huna mipango ya kupata pesa halafu sharobaro, ndio wale tunaowasikia wakiingia kwenye kampeni ya kumtangaza mwanamke ubaya wake kwa kila mtu ili nafsi zao ziridhike kwa hiyo leverage. Nimegundua pia,kilio kikubwa na reaction anayokuwa nayo mtu baada ya kumwagwa,huwa ni indication ya namna alivyomthamini huyo mpenzi aliemwacha na kumtegemea kihisia. Kwa maneno mengine ni kuwa, mtu ambae alikuwa anaamini kuwa mpenzi wake ndie anaemkamilisha kwa kila kitu, siku akiachwa,huwa anajiona kama ukamilifu wake umekwisha na hata kama atajibaraguza kuwa hajaumizwa, matendo yake yataashiria hayo bila hata yeye kujua kuwa matendo yake yanaakisi namna ambavyo hajitoshi bila mpenzi aliemwacha. Hata kwa wanawake,utasikia wanatangazia ushoga ma ex wao au uathirika ili mradi tu wawachafue na wao wapate nafuu. Wengine watasingizia mimba ili wasiachwe. Lakini kwa mtu alie na msimamo na maisha yake, hutamwona akitetereka sana na kulialia ovyo na huwa ni wepesi wa kusamehe.
Tafuteni pesa, mapenzi yapo tu.
 
Ulichofanya ni kuchanganya mbivu na mbichi mkuu, mapenzi na pesa. Penye pesa hakuna mapenzi, ni ununuzi wa ngono, bidhaa kama bidhaa nyingine, hapo hutokuwa unapendwa wewe ila wallet. Mapenzi hayana macho/hayachagui hayaangali uwezo wa mtu kiuchumi hasa kipesa, mtu anapenda mtu na sio kitu, wala mapenzi sio ngono.
 
Hujashka pesa z ukwel ww,,,, iv umewah kuw na pesa alaf unae mfukuzia humpati???? na akija hadum hata sex huambulii??? Waulize wanaolia watakwambia
Sio kwa miaka hii ambayo imejaa wasichana warembo kila kona, ukiwa na pesa ukipiga tu chafya hawa hapa lukuki, kwanini nisumbuke na mwenye pozi ilihal wa dizain yake wamejaa?
 
Ukiona Kijana/wakiume analialia na mapenzi..
Huyo ni Dhaifu na hasipo shtuka ataangamia
 

YANINI KURUNDIKA SUMU MWISHO ZIKUUWE ?? UKIACHWA LIA SANA TENA KWA SAUTI NYIKANI
WAAFRICA TUNAJIFANYA WAGUM HATULII AISEE BINAFSI NALIA SANA TU KUONDOA SUM MOYONI JIWEKE HURU TENA UKIACHWA NDIO LIA MPAKA KAMASI LIISHE ASEE SIJUI HUWA KAMASI LINATOKEA WAPI DU
 
Tatizo wanaangalia sana tamthilia za kifilipino na kilatin na kuwatamkia wachumba Please baby....Com on baby n.k

Btw ni wanaume wa Dar,
Ni wanaume wengi tu japo wa dar wanaongoza
Kuna jamaa kugombana na mkewe akaanza kusema harudi nyumbani anamuogopa mkewe labda apewe security ndo atarudi ha ha ha ha ha ha Maskini wanaume
 
yap bora ulie maana kuna siri kubwa sana kwenye machozi mimi huwa nikilia nakuwa mwepesi sana ata kama nilikuwa na tatizo kubwa kiasi gani nahisi kama nimeshalitua baada ya kulia
 
Ni wanaume wengi tu japo wa dar wanaongoza
Kuna jamaa kugombana na mkewe akaanza kusema harudi nyumbani anamuogopa mkewe labda apewe security ndo atarudi ha ha ha ha ha ha Maskini wanaume
mh huyo kweli wa dah lakini mimi nilie kulia nzega subutu...napiga napiga nusu ya kuua
 
Ukiona Kijana/wakiume analialia na mapenzi..
Huyo ni Dhaifu na hasipo shtuka ataangamia
hayaja kukuta mzee mwenzangu na kama kweli hayajakukuta muombe Mungu akuepushie maana kilio cha mapenzi mara nyingi hukosa m'bemberezaji
 
Ni wanaume wengi tu japo wa dar wanaongoza
Kuna jamaa kugombana na mkewe akaanza kusema harudi nyumbani anamuogopa mkewe labda apewe security ndo atarudi ha ha ha ha ha ha Maskini wanaume
Sasa kama aliolewa yeye atarudije? Hiyo ni sawa na kupigwa talaka.
 
Tatizo wanaangalia sana tamthilia za kifilipino na kilatin na kuwatamkia wachumba Please baby....Com on baby n.k

Btw ni wanaume wa Dar,
ila enzi zetu mzee mwenzangu unaenda shamba ukirudi unarundo la kuni begani ukitoka hapo unafukuzana na ng'ombe...siku ya kukimbizana na nyani shambani nayo si mchezo thats why wazee walimudu kudumu na ndoa zao...
 
aisee ila tumetofautiana ila kama huamini usifanye kazi uone kama hutoachika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…