mambomengi
JF-Expert Member
- May 16, 2009
- 829
- 242
Nikiwa mwana mabadiliko nje ya ccm.. yaani mwana Ukawa halisi.. . roho imeniuma sana baada ya kusoma Kifo cha Mh. Filikunjombe Deo kwenye akaunti ya tweeter ya Mh. Jerry Silaa.... sababu ziko tele kwa nini nimeumia sana kwani kila mtu anazijua (mapambano ya haki kwa watz)... kifupi, wapenda mabadiliko nje ya ccm hawachukii chama (ccm) bali yatendwayo ndani ya ccm.
Tukiwa bado tuna majonzi ya wapambanaji wengi kama Mtoi, Makaidi, Mtikila na pia kina Selina, Kigoda... Mgombea ubunge wa ACT Arusha n.k.... kwa kweli uchaguzi wa mwaka huu umeleta shida kubwa...... wapo pia walio nusurika ajali wengi tu kama mh. Lembeli...
Zimebaki siku 8 kabla ya kampaini kufungwa, nakuomba sana Mh. Raisi ajaye wa Ukawa, mzee wa anga Mh. Mbowe msitumie chopa kwa kipindi hiki..... tujaribu kupunguza risk iliyo mbele maana japo vifo vya walio wengi havijatokana na chopa ila chopa ni habari nyingine ikiwa na hitilafu au ikifanyiwa mambo..... ( hope waconect dots mtanielewa)
Nawakilisha....
Ni mmoja tu anajua uendako! Cha muhimu ni kuombeana.