Acha niseme ukweli ili nipate kuwa huru

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
987
1,912
Ilikua mwaka 2017 nilipata kazi sehem flan kufika nikakutana na kaka mmoja mpole Sana asie na makuu alikua akisifika ofic nzima kwa hekima zake. Nilitokea kumpenda Sana Sana nikajisogeza karibu kiurafiki tukawa friends tunapiga story nikaja gundua yupo single mtoto nikajitongozesha tukawa wapenzi.

Baada ya miezi 6 akanipeleka kwao akaja kwetu akanitolea mahari tukapanga ndoa mzazi wake akadai ajipange Kwanza ndio atufanyie sherehe. 2018 wakati mipango inaendelea akahamishwa kikazi kwenda mkoa mwingine nami Dec 2018 nikamfata tukaanza kuishi pamoja.

Nikapata changamoto ya kuchelewa kubeba mimba lakini namshukuru Mungu ninamtoto wa miezi. Kilichonifanya nije humu jamaa mapenzi kidogo aliyokua nayo kwangu yameisha kabisa. Yaani hana hata kidogo.

Tunaweza maliza hata mwezi hatujasex na nikimuuliza sababu kibao, tukipishina kauli nikijinunisha hana muda na Mimi kabisa
Anaweza safiri hata wiki zaidi ya kutuma sms wazima? Labda nimpigie Mimi. Nikimwambia niondoke hataki anadai kaa kwenye mji wako.

Yes hajanifukuza, hanipigi, hanitukani, sio mkorofi, familia anahudumia japo huduma zangu binafsi nikimbembe. Bt mapenzi hamna nikimuuliza anadai wasiwasi wangu tu. Nikiomba ruhusa kwenda kusalimia nyumban hajali hata nikae mwaka mzima.

Nahisi kudata nifanyeje?
 
Ilikua mwaka 2017 nilipata kazi sehem flan kufika nikakutana na kaka mmoja mpole Sana asie na makuu alikua akisifika ofic nzima kwa hekima zake
Nilitokea kumpenda Sana Sana nikajisogeza karibu kiurafiki tukawa friends tunapiga story nikaja gundua yupo single mtoto nikajitongozesha
Nipe namba zako nikushauri. Ogopa ushauri feki wa wadau
 
Go with the flow, jiulize kwanza ni kwanini uko hapo, ukipata jibu lizingatie. Kusema ukweli kuzaa watoto baba tofauti haipendezi, hata kama una mpango wa kuondoka jitahidi upate watoto wawili wa baba mmoja.

Hii hua inawatafuna wanawake wengi maisha yao yote, wanakuja kushtuka washazaa watoto kwa Baba tofauti halafu analoose kote maana automatically anaemzalisha mara ya pili sidhani atakua na realy love kwake.
 
Kwahiyo hoja ni kwamba unataka jamaa abutue kitumbua? Hapo jiangalie je baada ya kujifungua mtoto umekua mchafu? Hauna usafi wako tena hivo anavumilia tu kusogeza siku.
Hii huenda ndiyo sababu kubwa wanawake wengi wakijifungua huwa wanajisahau katika suala la usafi binafsi huwa sipendezewi sana na harufu ya mikojo na harufu nyinginezo hapa mudi inakata kabisa
 
Tatizo lilianza ulipojitongozesha. Acha mwanaume akutake yeye mwanamke tulia uringeringe
Value inashuka hasa kwa jamii zetu za kiafrika pia inawezekana na mabadiliko baada ya kujifungua nayo yakachangia jamaa kuloose interest ie jamaa alikuta demu kipotabo sasa demu kawa ka simtank😆. Atulize akili kabla ya kumface mskaji ajifanyie self assessment toka wanakutana je yeye alikuaje na Sasa yukoje kuanzia tabia,maumbile, mtazamo,saikolojia etc Kisha amcheki na mskaji kila angle ya maisha inawezekana anajistukia tu kumbe jamaa ndivyo alivyo sema hakupata nafasi kumchunguza alipofushwa na mapenzi
 
Back
Top Bottom