Acha kutafuta ajira

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Habari za wakati huu,

Miaka zaidi kadhaa iliyopita nilihitimu masomo yangu ya sekondari.Baada ya kuhitimu nilirudi nyumbani na tukakutana marafiki kadhaa ambao wote tulikuwa tumehitimu tukisubiri matokeo.Katika kipindi hicho nakumbuka siku moja katika majadiliano ya hapa na pale tuliulizana swali kuhusu matokeo yetu kwani kipindi hicho kulikuwa na suala la kufanya m,atriculation na kuchagua chuo cha kwenda kusoma.Chuo maarufu kabisa kilikuwa ni UDSM aka MLIMANI.Basi tukajiuliza JE matokeo yakitoka na hatujafaulu itakuwaje? Kila mtu alikuwa na JIBU lake,ila mimi katika uelewa wangu niliwaambia tua "MAISHA LAZIMA YAENDELEE."Kweli matokeo yakatoka na kila mmoja akawa amepa alichopata wakufeli akafeli na wakufaulu akafaulu na wakwenda chuo akaenda chuo na wa kuendelea na maisha akaendelea na maisha.

Wale walioendelea na maisha kuna walioenda migodini,kwenye biashara ndogogo na wengine wakaamua kurudia mitihani kujaribu tena.

Baada ya miaka 20 hali zetu za maisha zikawa hivi.Wale walioendeea na elimu wakahitimu,wakafanya wakaendelea na maisha wanakula mishahara mizuri tu.Wale waliorudia wakafaulu wakaendelea na masomo wakafaulu wakaajiriwa maisha yanaendelea

Wale waliongia field nao walikuwepo wengine bado wakibangaiza na maisha yanaendelea. Nilipobahatika kuzungumza nao hawa rafiki zangu nilijaribu kujadili net worth yao wote amapo kwa wote netw worth yetu ilikuwa na wastani wa kati ya TZS 50,000,0000 hadi TZS Bilion 3.Klilichonishangaza ni kwamba wenye Networth kubwa zaidi ni wale ambao waliwahi kuingia FIELD. Lakini kilichonivutia zaidi ni kwamba kati ya hawa waliowahi kuingia field wana kiwango kizuri kabisa cha maarfia na wengine baada ya PESA kukaa vizuri waliamua kurudi shule kwa ajili tu ya kuongeza maarifa kidogo katika maeneo fulani.

Ninchotaka kusema ni nini? Kama huna ajira basi STOP making your life about AJIRA na KUAJIRIWA. It is not worth it ila kama umeajiriwa kama SISI endelea kufanya kazi kwa bidii huku ukiendelea kumuibia mwajiri wako muda wake kwa aajili ya kuchat JF na INSTAGRAM badala ya kumuibia muda na kuutumia kujenga Biashara na UWEKEZAJI.

Ninachotaka kukwambia ni kwamba kama unatafuta kazi na hupati basi JIAJIR.SIKU hizi sio kama Zamani, kuna FURSA nyingi sana za kujikwamua na kutengeza ajira kwa ajili yako na wengine. Hata hivyo usidanganyike kwamba ni rahisi. Kila njia utakayochagua ni ngumu.

UNAWEZA KUACHA KUTAFUTA AJIRA NA KUJIAJIRI?
  1. Anza kwa kuanza kusoma kursa zinazotangaza TENDERS kwenye magazet badala ya kukimbilia tu KURASA zinazotangaza AJIRA
  2. Anza kwa kudefine kabisa aina ya cheo na majukumu unayotaka kufanya badala ya kusubiri tangazo la kazi liandika linataka mtu mwenye PHD ndo unagalia kama una PHD
  3. Anza kwa kuanza kutengeneza Business Cards na Business Profile na kuzisambaza badala ya kusambaza CV kila Siku.
  4. Anza kwa kujenga network yako ya watu ambao unaweza kufanya nao biashara badala ya watu ambao mnapiga stori na kutiana moyo
  5. Anza kwa kutembelea benki mbalimbali na kufahamu product ambazo wako nazo na namna ambazo zinazweza kukusaidia wewe kuanzisha biashara yako.
  6. Anza kwa kuandika Business plans and proposals badala ya kupoteza muda kuchangia nyuzi za kula tunda kimasihara na kucomment urojo mitandaoni
  7. Anza kwa kujifunza skills mpya ambazo hukufundishwa shule kama vile,udereva,computer,communication na skills nyingine nyingi ambazo ni muhimu katika kuhakikisha unafanikiwa katika maisha
  8. Anza kwa kutembelea TRA na kufahamu utaratibu wa kodi kwa aina mbalimbali za biashara
  9. Anza kwa kutembelea maduka ya JUMLA kariakoo na kuuliza bei huku ukilinganisha BEI hizo na za ALI baba pamoja kufahamu iwapo zinatofauti kubwa
  10. Anza kwa kutembelea mitandao na kuagiza bidhaa nje ya nchi (Bila kulipia na kisha unaenda Benki ufahamu jinsi ya kulipia na unaenda TRA ufahamu kodi yake ni kiasi gani na kisha unaenda kwa wasafirishaji kufahamu shipping cost za DHL na UPS na wengine wengi
  11. Anza kwa kusoma vitabu na maandiko ambayo yanahusu watu waliofanikiwa katika biashara na maisha na ungaliwe sana sababu ya kuanguka kwao kwani humo kuna somo kubwa.
Kuna mengi ambayo unaweza kufanya ili kufikia malengo yako kwa kuamua kujiajiri na kuachana kutafuta ajira.Kama ajira ipo ipo tu.Ukiitwa DODO kwenda kufanya interview unaweza tumia hadi 500k kwa interview moja ambayo PESA hio inatosha kusajili kampuni na kuanza kufanya BIASHARA zai aina tofauti.Unaweza kuanzisha kampuni yako lakini usijipe Cheo cha Managing Director bali unajipa Cheo cha kazi ya Ndoto zako.Mfano kama wewe ni Mataalamu wa Masoko unajiita Senior Sales Officer n.k na kadiri biashara inavokuwa basi na wewe unajipromote.Ni ujinga kujiita Managing Director and CEO wa kampuni ambayo haina hata Cashflow ya kuzugia.Jiite basi Business Development Officer.

IKO hivi.Probability ya kufanikiwa katika Biashara ni kubwa sana kuliko kufanikiwa ndani ya ajira.Ili ufanikiwe katika ajira inabidi na BOSI wako naye afanikiwa zaidi yako ila kwenye BIASHARA you keep everything.


Sasa nirudi kwenye HOJA ya MSINGI maana hizo nyingine ni Mbwembwe tu.

Kuna Project mpya inaitwa MVP ( Managed Venture Program); ambayo ninataka kuiingiza sokoni.Hii product ni kwa ajili ya wale ambao wanao uwezo wa kifedha na wanataka kuanzisha kampuni lakini hawataki kuingia katika STRESS za kushughulika na STARTUP maana kusimamia Startup ni kichefuchefu.Sasa hii MVP ni kwa ajili ya watu kama hao.SIFA ya kushiriki katika MVP ni kwamba ni lazima uwe na NIA ya kuanzisha BIASHARA katika maeneo ya Technolgy and ICT tu.

Kwa nini maeneo haya ICT na Teknolojia??Ni kwa sababu haya ndio maeneo ambayo hutahitajika kununua mzigo mkubwa na wala hutahitaji kuwekeza mtaji mkubwa.Vile vile ni aina ya biashara ambayo ukitaka kutoka ni rahisi sana kwa ni unaamua tu kwamba sasa sitaki kuweka hela yangu huku na inakuwa ndio mwisho wa kazi/biashara.Vile vile biashara za ICT na teknolojia zina uwezekano mkubwa wa kuwa scaled UP(Mfano) Ukishatengeneza Platform kama JF kitu pekee unafanya ni kuhakikisha inakuwa hewani wakati wote na watumiaji wapo.Ukiweza hilo basi unachofanya ni kutafuta namna ya kutengeneza PESA kwa kutumia JUKWA hilo lakini kuhusu Marginality unakuwa na uwezo wa kukukua tu..

Utapata nini ukishiriki katika MVP?
Ukishiriki katika MVP unakuwa mmiliki wa biashara ambayo itakuwa imesajiliwa na inalipa kodi itakuwa na wateja wake na product zake.Wewe utakuwa ndio mkurugenzi mkuu na utakuwa na Account Manager Wako ambaye Ndiye Mfanyakazi wako Pekee.Gharama za wafanyakazi wengine kama vile Developers,Marketers,Accountants,Lawyers,Sales Personel,Call attendants na wengine hazitakuwa katika kampuni yako bali kila kitu tutafanya sisi. So ukimiliki MVP utapata faida nyingi kama vile:
  1. Wewe utakuwe ni Muendeshaji mkuu wa akaunti kuu za Kampuni
  2. Wewe utakhusika katika kusaini mikataba yote ya kampuni
  3. Wewe utahusika katika maamuzi yote ya msingi ya kampuni.
  4. Kampuni itakuwa ni ya kwako na sisi tutakuwa ni wasimamizi tu.
  5. Tutaisimamia kampuni yako kwa kipindi cha kati ya miezi sita hadi 24 kwa kutegemea performance ya biashara na baada ya hapo tutakusaidia sasa kuiweka biashara yako ili ijiendeshe chini ya usimamizi wako.
Vile vile MVP itahusisha gharama zifuatazo:
MVP iniahusissha Huduma ya USajili wa kampuni ambayo gharama yake itategemea kiwango cha mtaji
Gharama ya EFD Machine pamoja na address ambayo itategemea na location yako
Gharama ya Kufungua akaunti Benki kwa ajili ya Kampuni ( Salio ni lako)
Gharama ya Wafanyakazi ambayo itategemea na aina ya biashara na italipwa kwa miezi mitatu
Gharama ya Website pamoja na mfumo wa utunzaji kumbukumbu na mawasiliano ya wafanyakazi

Zingatia.Katika huduma hii ya MVP wewe ndio mmiliki wa kampuni na biashara na utapatiwa taarifa za siku,wiki,mwezi,miezi mitatu n.k. kwa kutegemea na utendaji wa kampuni yako.
 
Kumbe hili ni tangazo la kutafuta fursa?
Inategemea unalisomaje? Lakini mwisho wa yote nothing comes for free.Hata ushauri kama huu nispotafuta namna ya kuufanyia monetization nitakuwa sitoi ushauri practical
 
Maelezo mazuri, lakini ukisoma katika mistsri unaona hapa mtu anatafuta fulsa kwa kutumia wengine, kwani wewe unatoa huduma gani! Hii yako imekaa kama deci, au kuku project.
 
Maelezo mazuri,lakini ukisoma katika mistsri,unaona hapa mtu anatafuta fulsa kwa kutumia wengine,kwani wewe unatoa huduma gani!!hii yako imekaa kama deci,au kuku project.
Hapana mkuu,huduma yetu sio DECI wala SIO MR.KUKU.

Katika huduma yangu utamiliki Biashara Kamili ambayo imesajiliwa kisheria yenye akaunti benki,wafanyakazi na product.Utakuwa msimamizi na maamuzi yote yatakuhsu wewe kutoa approval ama kwa maandishi au kwa mifumo maalumu ya approvals.Na vile vile sisi tunataka kuwekeza kwenye TECH.So unaona tofauti yetu na DECI.Hatukuahidia faida ya haraka kwa sababu sisi hatukp na model ya kutengeneza FAIDA ila tunakuondolea stress za kusimamia STARTUPS hasa pale mwanzoni kabisa.
 
"Net worth yetu ni bilioni 3" mtumish wa Tanzania hii hii awe na net worth hio.
Kwa wafanyabiashara nakuunga mkono.
Kuna msemo humu JF kuwa ukimuona mtu anakuita kwenye fursa jua wewe ndio fursa
 
"Net worth yetu ni bilioni 3" mtumish wa Tanzania hii hii awe na net worth hio.
Kwa wafanyabiashara nakuunga mkono.
Kuna msemo humu JF kuwa ukimuona mtu anakuita kwenye fursa jua wewe ndio fursa
Mkuu Kuna ambao kwa asset zao walizo nazo zinafika 3Billions.Na hio ni kwa General assessment tu na wala sio muajiriwa.All in all Ukiitiwa firsa wewe ni fursa
 
Umenena yoteeee yakuvutia na kumotivate xx tuliotupa vyetu baada ya kuajiriwa xaxa ndo tunaona chungu ya Ajira, umelonga yote ila sijaona cost zako mkuu hilo ndilo jambo la mbolea kushinda yote ili nijipange na haka ka plan nakotaka kikaanzisha ,Thanks in advance mkuu mybe future tutafanya ki2....
Enzi za kikwete zinerudi yan full madli ya paleee bandarin....
 
Back
Top Bottom