Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,534
- 24,079
Bwana Lukuledi alikuwa anapenda sana kunywa pombe kiasi kwamba ilikuwa akipata pesa anaondoka asubuhi na mapema kwenda kunywa pombe mpaka usiku sana anarudi kulala tu na kesho tena ataamka asubuh na mapema kwenda kunywa na kurudi usiku mkali sana.
kijijini pote walimjua ingawa yeye wala hakuwa na ugomvi na mtu akijinywea pombe zake anarudi zake nyumbani analala na wala huwa hataki maneno kwa kuwa huwa anasema akisemeshwa sana maneno yanamkata stimu maana akinywa huwa anahisi yupo ulimwengu wa mbali sana wenye raha tupu na maisha mazuri akiwa amezungukwa na wanawake kama 60 hivi wazuri na wote ni wa kwake.
jambo hili limekuwa likimuumiza sana mkewe kiasi kwamba kuna siku ambayo mzee Lukuledi hakwenda kunywa pombe kwa sababu alipata ajali alipokuwa akirudi toka ulevini na hivyo miguu yote kuvunjika vibaya sana. hakuweza kutembea. akiwa amelazwa hospital mkewe akawa akimhudumia na kwa mara ya kwanza akapata muda wa kumuuliza mambo mbali mbali na kujadiliana naye kuhusu maisha.
katika maongezi mkewe akajaribu kumuuliza swali moja aliloona ni la msingi sana maana alishaamua kuwa aondoke tu akaishi kwa wazaz wake kuliko kuendelea kuishi na Bwana Lukuledi. ili aweze kupata angalau faraja ya kubaki maana bado hakupenda sana kuondoka ila alilazimika kutokana na hali ya Bwana Lukuledi kutomjali. akaamua kumuuliza akidhani kipindi hiki Bwana Lukuledi atakuwa na majibu ya kumfariji mke wake. akamuuliza kwa Upole kabisa .
Mke: Hivi mume wangu kwa hali yako ya sasa ukiambiwa chagua pombe na mimi utachagua nini?
Lukuledi: unaanza mambo ya kijinga, ACHA KUFANANISHA POMBE NA VITU VYA KIPUMBAVU WEWE"