Acha kujilaumu unadanganywa

Acha kujilaumu unadanganywa

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,303
Reaction score
4,998
Trust me!

Mitandao ya kijamii inadanganya sana, sana sana! Ukitazama picha watu wanazopost, nguo wanazovaa, sehemu walizopo n.k Mara nyingi huwa sio uhalisia kabisa wa maisha yao....

Yaani mtu anaweza mpost mume wake,mke wake akaonesha kuwa wana life fulani hivi amazing, wana mapenzi moto moto, kumbe jana katoka kupewa kipondo cha uhakika, na nyumbani hakuna amani kabisa (Sina maana kuwa ni Sawa kumpiga mkeo).

Ukiishi kwa kujilingalisha na picha au maisha ya watu kwenye mitandao yaani utajiona upo nyuma sana.

Utajiona wewe sio mzuri, huna fedha na huna maisha kumbe wenzako na wenyewe wanasota tu kama wewe. ISIPOKUWA wao wanachagua vitu gani vya kukuonyesha!

Kuna vitu kuhusu wao hauvijui na Hawawezi kukuonyesha! Hawawezi kukuonyesha namna wanavyohustle, kukimbizana huku na kule! Yeye anakuonyesha matokeo chanya tu. Hatakuonyesha Jana alivyogombezwa na boss wake,

hawezi kukuambia kuwa jana alilala njaa, au hata alikosa pesa ya nauli...jana alifumuliwa malinda ndio akapata hiyo hela ya kununua chakula

Point yangu hapa ni kwamba, social media zisikufanye ujione umechelewa. Yaani wewe upo nyuma. Wala hata usiyumbishwe na posts za social media, ukijua UNACHOKITAFUTA zingine huwa zinabaki kelele tu.

Acha kudharau na kuchukia maisha yako eti kwa sababu umejilinganisha na mtu fulani halafu unaona kama amekuzidi vile.

Kwanza sio Sawa kujilinganisha na mtu mwingine, sio social media tu Hata kwenye maisha ya kawaida. Wewe ni John, utabaki kuwa John! Yule ni Joseph. Wote ni wazuri kwa jinsi zenu, mmepewa talanta tofauti,

uwezo tofauti, hobbies tofauti, personalities tofauti kulingana na namna alivyopenda MUNGU. Wote mnatumika tofauti kuleta tofauti chanya! Kwanini ujilinganishe naye?

Unajua mafanikio yake yametokana na nini?

Jifunze kwa mtu usijilinganishe naye!

Sisi wote ni wazuri kwa jinsi zetu[emoji8] jiamini kuwa unaweza hata wewe

sent from toyota Allex
 
Back
Top Bottom